Nilishaamua, Nitabaki Kuwa Mjamaa... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nilishaamua, Nitabaki Kuwa Mjamaa...

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by maggid, Aug 26, 2012.

 1. m

  maggid Verified User

  #1
  Aug 26, 2012
  Joined: Dec 3, 2006
  Messages: 1,084
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Ndugu zangu,

  Kwa siku mbili mfululizo nilikuwa kijijini Mahango, Kata ya Madibira, Mbarali, Mbeya. Huko niliongozana na wageni kutoka Uingereza waliokwenda kushiriki kazi ya ujenzi wa Maktaba ya Kijamii kijijini Mahango.

  Uzoefu nilioupata kijijini Mahango ni elimu yenye gharama kubwa. Hakika nimejifunza mambo mengi. Kijijini Mahango niliuona kwa karibu sana umasikini wa watu wetu. Kwa mfano, kwenye moja ya kitongoji nilimshuhudia mama anayelindia maji kwenye kisima chenye chemchemi yenye kutoa maji ya kujaa bakuli moja kila baada ya robo saa.

  Mama yule kwa kauli yake alitamka huku akiwa ameshika tama; " Hali yetu ni mbaya sana, hapa ndoo moja kujaa inaweza kunichukua saa moja na nusu". Wakati akitamka hayo nilimwona binti wa mama huyo asiyezidi miaka kumi akiwa amesimama akimwangalia mama yake. Niliziona pia ndoo zilizopanga foleni bila wenye nazo. Bila shaka wamekwenda kujihifadhi na jua kali la mchana, na kufanya kazi nyingine pia.

  Hali kama hiyo niliikuta pia kijijini Mapogolo. Kwenye ofisi ya Mtendaji Kata ya Miyombweni kilipo kijiji cha Mapogolo nilifanya mazungumzo na Diwani wa Kata Bw. Lokelo pamoja na Mtendaji wa Kata Bw. Filipo. Nao wakawa wamekunja mikono wasijue la kufanya, maana, bajeti ya Halmashauri ya kushughulikia na tatizo la maji haitoi matumaini ya kutatua tatizo la wananchi katika muda mfupi ujao. Fedha hazitoshi.

  Kwenye Mkutano wa hadhara kijijini Mahango, Mwenyekiti wa Kijiji alinipa nafasi adimu ya kuzungumza machache na wananchi. Nilisimama na kuwaangalia wananchi wale walioonyesha kwenye nyuso zao, kiu ya kutaka kunisikiliza; niliwaangalia akina mama na watoto migongoni, niliwaangalia watoto wale waliokaa mbele yangu. Niliwaangalia akina baba na vijana. Kwa jinsi watu walivyoitikia wito wa kukusanyika kushiriki kazi ya ujenzi wa Maktaba, kushiriki jambo la elimu, basi, nami niliyaona matumaini kwenye kusanyiko lile.

  " Mahango Oyee!"
  Nilitamka na nikaitikiwa kwa sauti kubwa. Haraka nikaamua niongelee umuhimu wa Ujamaa na Kujitegemea; kufanya kazi kwa ushirikiano. Nikaanza hotuba yangu fupi kwa kumnukuu Mwanafalsafa David Hume kwa maneno yake haya;

  "MBEGU yako imekomaa leo, yangu itakomaa kesho. Ni jambo la manufaa kwetu sote kama nitalima pamoja nawe leo, na wewe unisaidie kulima kesho. Siwezi kuwa na urafiki nawe kama naona kuwa hujengi urafiki nami. Msimu utapita, nasi tusipoaminiana na kushirikiana, basi, sote tutakula hasara." (Mwanafalsafa David Hume)

  Nikasisitiza pia umuhimu wa kuzingatia ‘K' tatu ili kufanikiwa katika tuyafanyayo; Kujitambua, Kujiamini na Kuthubutu. Pale Mahango nikasisitiza pia umuhimu wa kuitanguliza Tanzania kwanza katika yote tuyafanyayo. Tusiendekeze sana tofauti zetu za kisiasa. Tuwajue maadui tunaopambana nao, tuyajue malengo yetu kwenye vita iliyo mbele yetu. Tukubaliane kupambana kwa pamoja kwa maana ya kufanya kazi kwa pamoja ili kuyafikia malengo yetu.

  Maana, hii ni nchi yetu. Ni nchi yetu sote. Hatima yetu kama watu binafsi, kama vikundi vya watu na kama taifa, inatutegemea sisi wenyewe. Umasikini wa watu wetu ni umasikini wetu.

  Naam, sijawahi kuficha imani yangu ya kisiasa, kwa maana ya itikadi yangu. Na imani yangu inaimarika zaidi kadri ninavyozidi kutembelea na kukutana na watu wa vijijini.

  Kiitikadi mimi ni Mjamaa ninayeamini katika uwepo wa demokrasia na kutanguliza maslahi ya walio wengi katika jamii- I am a Social Democrat. Na bado naamini kuwa hata sasa, mfumo wa enzi za Mwalimu wa Ujamaa na Kujitegemea bado una nafasi katika jamii yetu. Misingi ya Ujamaa na Kujitegemea bado ni muhimili wa maendeleo ya nchi na watu wake. Ni udhaifu na kutokujiamini kwa kuionea haya misingi iliyoijenga jamii yetu na ambayo bado ina nafasi ya kuifanya nchi yetu kuwa ya kisasa zaidi kama itaimarishwa.

  Maana, mfumo wa Ujamaa na Kujitegemea uliofanyiwa mabadiliko ya kimsingi unaweza kutuhakikishia ulinzi wa maslahi ya nchi yetu. Ni kwa sera zenye kuhakikisha usawa wa watu. Sera zitakazohakikisha kodi inakusanywa na kutumika katika yaliyo muhimu na yenye kumsaidia pia mwananchi wa chini katika nchi yetu. Mwananchi aweze kupata elimu bora na huduma bora za afya, maji, miundo mbinu kati ya mengineyo ya msingi.

  Tuazimie sasa kuwajibika kwa pamoja kwa maslahi ya nchi yetu. Na tukifanya ajizi, tutaigeuza nchi yetu kuwa ' nyumba ya njaa'.

  Naam, Nilishaamua nitabaki kuwa Mjamaa.


  Maggid Mjengwa,
  Iringa.
   
 2. Kunta Kinte

  Kunta Kinte JF-Expert Member

  #2
  Aug 26, 2012
  Joined: May 18, 2009
  Messages: 3,660
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Aheri yako wewe mwenye uthubutu wa kutetea ujamaa, viongozi wetu hivi sasa wengi wao wanaona aibu hata kuutaja ilihali hata huo ubepari wenyewe hawaujui!
   
 3. T

  Tata JF-Expert Member

  #3
  Aug 26, 2012
  Joined: Dec 3, 2009
  Messages: 4,729
  Likes Received: 645
  Trophy Points: 280
  Maggid ukweli ni kuwa ujamaa na kujitegemea ndio sera sahihi kwa hizi jamhuri ndizi (banana republics) kama hii ya kwetu. Ila ujamaa tunaoutaka ni wa vitendo zaidi na sio ule wa imani na porojo tuliokuwa tukihubiriwa mashuleni enzi zile za zidumu fikra. Kuna wananchi ukiwaacha wajiondoe wenyewe kwenye umaskini hawatakaa waondokane nao mpaka mwisho wa dunia.

  Ujamaa wa vitendo ni pamoja na kuwashughulikia vikali (ikiwepo kuwapiga risasi mara inapothibitishwa) mafisadi na wezi wa mali za umma ambao wanatumia dhamana waliyopewa kujinufisha wenyewe badala ya kuondoa umaskini wa wananchi wasio na msaada kama hao uliokutana nao kijijini Mahango.
   
 4. F

  Fitinamwiko JF-Expert Member

  #4
  Aug 26, 2012
  Joined: Aug 13, 2012
  Messages: 4,810
  Likes Received: 255
  Trophy Points: 180
  Mh Maggid nimesoma maelezo yako yote, roho imeniuma mno. Kweli miaka zaidi ya 50 ya Uhuru bado watu wanaishi maisha magumu kiasi hiki? Angalia gap between viongozi wa serikali na wananchi, kweli tuliwachagua watudhulumu? Maana hata enzi za mkoloni, kulikuwa na afadhali. Ukisema ukweli, watakimbilia kusema eti wewe ni CDM. Hao wananchi wanaoishi vijijini ndio mtaji wa CCM ktk chaguzi zote. After uchaguzi, CCM inawatelekeza na kuwanyanyasa. Muda umefika tuwaelimishe na kuwaambia ukweli kuhusu ADUI yao ni CCM na VIONGOZI WAKE. 2015 tuwatose ccm, nchi imewashinda
   
 5. t

  tenende JF-Expert Member

  #5
  Aug 26, 2012
  Joined: Jan 10, 2012
  Messages: 6,560
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Nani atarudisha ujamaa?!, CCM kwa maneno na maandishi ni wajamaa, lakini kwa matendo ni mabepari wa kutupwa!, CDM, CUF n.k. ni mrengo wa kati!.. Katiba yetu ni - inatambua itikadi yetu ni ujamaa, lakini inpractice - UBEPARI, ambao awali ulipingwa kwa nguvu zote!!!.
   
 6. m

  maggid Verified User

  #6
  Aug 26, 2012
  Joined: Dec 3, 2006
  Messages: 1,084
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180

  Ndugu Tata,
  Ahsante kwa mchango wako.

  Ni kweli kabisa, kuwa Ujamaa unaohitajika sasa uwe ni wa vitendo zaidi. Ni lazima tuonyeshe kwa vitendo kuwa tunachukia ufisadi. Ni lazima tuonyeshe kwa vitendo kuwa rasilimali za umma zinalindwa. Kuwa tunakusanya kodi na matumizi ya fedha za umma yanadhibitiwa.

  Na kwa kweli, siamini kabisa kuwa watu wetu wale ninaokutana nao vijijini watakombolewa kwa sera za Kibepari, abadan!

  Maggid,
  Iringa.
   
 7. Nicholas

  Nicholas JF-Expert Member

  #7
  Aug 27, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 25,132
  Likes Received: 2,351
  Trophy Points: 280
  Suala kama hilo ni ujinga wa viongozi wa eneo hilo na jamii kukosa sheria ndogondogo za kuwasaidia fanya mambo ya jamii kwa pamoja.

  hao jamaa wangejaribu fanya marekebisho madogo katik hichi kisima maji yangejaa usiku, mchana wakija wangekuwa na uwezo wa kupata maji kwa haraka.Pia wangeweza jiwekewa seheeria ya kuchukua maji kidogo n akwa mpango ili kisima kijae maji na baadaye rate ya kuchukua iwe ndogo kuliko rate ya maji kujikusanya.

  Hawa ndio watu mtaji wa wapuuzi wa ccm.
   
 8. a

  andrews JF-Expert Member

  #8
  Aug 27, 2012
  Joined: Mar 28, 2012
  Messages: 1,680
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  hawa watu kwa sababu ccm na ye mwenyewe wamekuwa wakiwatumia waislamu kwa manufaa ya ccm sasa anogopa siri kuwekwa hadharani tumeone waislamu wengi viongozi mzee mwinyi aliwadhibiti akina ponda mzee makamba aliwadhibiti pale magomeni sasa kikwete kwa nini tusikuone wewe ni swahiba na unawafurahia kwa sababu wanafanya kazi abayo ndani ya moyo wako unachekelea lakini kumnuka vita ya kidini haitamuacha salma ridhiwani wala ndugu yako yeyote acha udini ongoza nchi nyerere aliyuonya watanzania kukuchagua sasa tunaona faida zake
   
Loading...