Nilioyaona Moshi Mjini

zanku

Member
Jun 9, 2020
69
149
NI ZIARA YA SIKU TATU-NILIYOYAONA MOSHI MJINI

Katika safari/Ziara yangu ya siku Tatu ya Moshi Mjini nimetembelea kata Takribani tisa na nimekutana na watu wengi na kujadili Masuala ya kisiasa na nimejifunza mengi sana, hasa wakati huu wa kutafuta nani atapeperusha bendera ya CCM?.

Idadi kubwa ya watu wamekua na Imani kubwa na mgombea aliyepeperusha bendera ya CCM mwaka 2015 kuwa ndiye hasa anayestahili kuja kupeperusha bendera ya CCM na wana imani Atajitokeza kwenye kura za maoni na hatimaye kushinda, ibaki kazi ya wananchi kufutwa machozi baada ya kuhangaika na upinzani usio na Dira.

Niliwauliza watoa maoni kwanini yeye na si mwingine?, Wamenipa sababu lukuki lakini nitaainisha sababu chache.

Kuwa Mgombea huyo wa mwaka 2015, aliweza kuleta mshikamano, kwa wananchi na walimkubali kutokana na uwezo wake wa kimaendeleo na jinsi alivyojishusha kwa wananchi na kushiriki nao katika msuala mbalimbali ya kimaendeleo, hapa alishiriki harakati za maendeleo bila kubagua watu.

Katika chama hasa Moshi mjini, Alirudisha Uhai wa Chama mara dufu na ilikuwa ni jimbo ambalo ni nadra sana mwanachama wa chama cha mapinduzi kuvaa sare ya chama na kupita bila kufanyiwa fujo na wachama wa upinzani hasa chadema, Yeye aliweza kuzuia hilo na kuwapa wanachama wa CCM nguvu ya kutembea kifua mbele na nguo zao za chama.

Mtaji wake kisiasa ni Mkubwa sana, ambao wapo mpaka wapinzani wanaoshindwa kuficha jinsi wanavyomkubali, Kwani ndiye Mgombea pekee wa ccm (toka vyama vingi vianze) kupata kura nyingi na hii inadhihirisha hata wapinzani walimpigia kura.
Kwa hiyo Mgombea huyo anamtaji wa kisiasa katika jimbo la Moshi Mjini.

Wananchi wanasema tatizo CCM imekua ikibadili wagombea wapya kila baada ya uchaguzi na kupelekea kila uchaguzi mgombea anatumia muda mrefu kujitambulisha kwa wananchi.

*Tatizo liko wapi*
Pia nikataka kujua iwapo mgombea huyo wa 2015 ana nia ya kurudi tena kuendeleza nia yake ya maendeleo kwa kushirikiana na watu wa Moshi.
Nilichogundua nia ya Mgombea huyu wa 2015 ni Maendeleo kwa Jimbo la Moshi na kutaka kurudisha Maendeleo nyumbani kwao, baada ya kutafuta nje ya nyumbani, Nia yake ya dhati ilizuiwa na Baadhi ya wanachama wa CCM (Yuda Akiwemo) waliojinasibu wao ndio wenye dhamana ya kuongoza Moshi na si mwingine.

Ni hivi baada ya Mchakato wa Kura za Maoni kushinda, wanachama hao walishindwa kuvunja Makundi na kugeuza kuwa kundi la kuipinga ccm na Mgombea wake.

Kwa sasa CCM ngazi ya Mkoa ina viongozi ambao walisimama wima kuipinga CCM mwaka 2015 na kusababisha CCM kupoteza Jimbo, Na sasa viongozi hao hawataki hata kusikia Mwanachama huyo wa CCM na aliyekua mgombea mwaka 2015 anafika Moshi.
Ni hivi Kuna Wakati fulani alishiriki Msiba wa aliyekua Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kilimanjaro, viongozi hao na washiriki wao ambao wamepanga ndio watagombea Ubunge na wameanza kampeni na kujiita wabunge toka Mwaka jana, wakaanza kumpinga na kumchafua kuwa ameanza kampeni kisa tu kaonekana Msibani.
Baada ya uchunguzi wa tuhuma hizo zikionekana si za kweli.

Nilichogundua, katika Siasa huwezi zuia hisia za Wananchi waliokuchagua iwe uliishinda au hukushinda wao wana haki ya kuonesha hisia zao japo tu wasivunje sheria na taratibu ya nchi na za chama.

Kwa hili hivi huyu Mgombea atakua na nia ya kurudi kweli kama anapingwa waziwazi na viongozi wenye Mamlaka katika chama na washiriki wake katika Mkoa?-Tusubiri.

Nahitimisha kwa kusema, Wananchi wa Moshi wanahitaji maendeleo ya kweli na ya kudumu, Ni vema CCM ikaona kuwa kuna haja ya kukomboa jimbo ambalo lipo upinzani kwa miaka 25, Wananchi hawahitaji Msaada wanahitaji mtu wa kushirikiana nae kuleta Maendeleo.

Tuwasaidie wananchi wa Moshi Mjini na Chama cha Mapinduzi katika kulikomboa jimbo.

MOSHI KWA SASA HAKUNA UPINZANI KWANI CHADEMA ILISHAJIFIA, UPINZANI UPO NDANI YA CHAMA
 
Huyu mgombea mwaka 2015 alitumia zaidi ya 2 bilion kwenye kampeni zake Kama rushwa.kwa Sasa hatumwitaji ni mpenda rushwa chama kilisha kuwa safi.akienda CHADEMA watamchukua sio CCM.
 
Sehemu zenye neema sana hapa Tz nipamoja na uchagani vijijin ,wamepata umeme na maji miaka mingi huku barabara zikipitika vzru.
 
Hii unayoisimulia itakuwa Moshi ya Kenya lakini kama ni ya Tanzania basi tusiandikie mate bali nenda kamuulize Davis Mosha atakutoa tongotongo
 
Sehemu zenye neema sana hapa Tz nipamoja na uchagani vijijin ,wamepata umeme na maji miaka mingi huku barabara zikipitika vzru.
Mimi nina zaidi ya miaka 50 na nilikuta lami na umeme. Hivyo hatuhongeki ili tuuze kura.. Waende Lindi.
 
Uchagani hakuna shida kama makabila mengine we pompoma
Karibu moshi
Screenshot_20200610-210338.jpeg
 
Mnadanganyika hapo na mnapaswa kutenganisha shamrashamra za wagombea na zile za wananchi. Ccm ikishinda Moshi ni kwa kuiba kura na kwa kutumia hongo kubwa.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom