bongo-live
JF-Expert Member
- Jul 3, 2013
- 1,140
- 1,292
Katika harakati za kutafuta mume ilikuwa hivi:
Nilipendana na kaka mmoja wa Singida. Huyu kaka aliniambia anataka nimpeleke kwa wazazi ili akajitambulishe na tufunge ndoa kwakuwa mwanzo nilimweleza nataka tufunge ndoa kwanza ndipo nitampa penzi na kwakuwa nilikuwa bado bikra akakubali.
Akaniambia nijiandae nimpeleke kwa wazazi, nikawaza ni wanaume wachache sana watakubali ndoa bila kutest dyudyu. Siku moja nikamwomba niende kwake kumtembelea, akasita kidogo halafu akaniambia usijali kwa leo sitaweza ila nitakualika siku rasmi.
Siku ikafika nikaenda kwake jioni kwenye saa moja hivi nikakaa kwa kiti, macho yngu yanazunguka kuangalia mazingira ya hapo ndani. Nikaona sehemu ukutani pameandikwa 1,3,2,7. Jamani nyumba iliyoishi mtoto haijifichi, nikawazaa nikaona nimtume dukani anifuatie chipsi na soda nina njaa, akakubali.
Kitendo cha kwenda dukani, nikasuburi dakika 5 nikafunga mlango kwa hofu. Nikakagua kabatini, nikakagua uvunguni, ile nimenyanyua godoro nikakutana na chupi za kike tena chafu na kanga. Ile kanga nikaitoa nikaiweka kitandani, aliporudi toka dukani akaikuta akahamaki eti "nilinunua kanga kwa ajili ya kuogea". Nikamwambia poa, hata mimi nataka niwahi nyumbani kaka ni mkali.
Hata kula sikuweza nikaondoka. Jamaa alikuwa kafukuza mke, ningeuvaa mkenge.
Akili ni nywele.