msani
JF-Expert Member
- Jun 13, 2011
- 1,800
- 1,194
Sijui ni tamaa au ujinga au ndio style yake.
Ninafanya kazi Wizara fulani mkoani Arusha alikuja dada mmoja ofisini kuja kunisalimia maana tulisoma naye na ni rafiki yangu wa karibu sana.
Kwenye hiyo ofisi bosi ni kiwembe balaa na tulikuwa tunajua kuwa ameathirika na ukimwi. Kila binti mrembo akiingia pale alikuwa anatongozwa na wengi waliingia mkenge. Siku hiyo akaingia huyo binti mrembo rafiki yangu na alipotoka tu nikaitwa ofisini na kukawa na maongezi ya kikazi lkn moyoni nilijua kuna la ziada maana namfahamu.
Kweli mwisho wa mazungumzo akiniulizia yule binti nikamwambia ni rafiki yangu na kuhusu uhusiano nikajibu ni rafiki yangu pia. Akaniomba namba yake nikamwambia nitampa baada ya kuomba ruhusa.
Nikamwambia binti na kumweleza nilivyobanwa huku na bosi,binti akasema we mpe,nikatekeleza! Ila jioni ila baada ya siku 2 tukaonana na yule binti nikamwambia kuwa pale sio salama na kwamba kumwambia vile sio kwamba namuona ni mwepesi la hasha bali kumtahadhalisha na binti akasema anajua jinsi ya kumuhendo na kwamba atakwama mwenyewe.
Siku moja baada ya wiki 3 nipo kwenye hoteli moja ghafla macho yangu yakawa yanakataa kuamini kilicho mbele yangu na mara bosi naye anakutana na macho yangu na kunisalimu na kuniambia wapo hapo wanapumzika kidogo na binti yule yule rafiki yangu.
Sasa sijui kamwambia bosi niliyomueleza au kaamua kunyamaza?
Sijui ni tama au nini?
Huyu binti kaingia cha kike maana wamekuja wengi wanalia hapa ofisini na nimefuta na namba yake.
Sijui nilifanya kosa anyway ngoja nisubiri wiki ianze nitaona mwelekeo utanipa majibu kama kaambiwa au la.