Nilimshauri lakini hakunisikia kosa langu nini?

Nilimshauri lakini hakunisikia kosa langu nini?

monaco

JF-Expert Member
Joined
Oct 13, 2012
Posts
2,184
Reaction score
1,779
Wadauuuu
ni mimi mzee wa Monaco tena.....
poleni na majukumu,kuna tukio limetokea wiki chache zilizopita,kuna jamaa yangu tulikuwa nae tumepanga nyumba moja,tulikuwa vijana 3,tusiooa na 2 walikuwa wameoa,Bwana mmoja kiumri alikuwa ametuzidi,kweli alikuwa anatuheshimu sana,alikuwa na watoto 2,ni kama 37yrs hivi,wote sisi ni wafanyakazi,jamaa anafanya kampuni moja ya Mabati hapa Dar.mimi pia nipo kiwanda fulani,jamaa alikuwa anaingia shift Rotation,wenyekujua mambo ya shift wanaelewa,siku hiyo jamaa akawa anaingia saa 19:30 jioni mpaka saa 07:30 asubuhi,Huyu kijana mwenzangu age mate alikuwa anamla uroda mke wa huyu brother,na brother hakuwahi sio tu kujua bali hata kuhisi chochote,siku moja mimi nikamwambia jamaa yangu,acha kutembea na huyu dada,jamaa akijua haitakuwa picha nzuri hata kwangu,jamaa alikuwa anakataa kata kata,mtindo ulikuwa unaendelea,jamaa akiondoka tu jamaa huingia chumbani na kuanza kula uroda,siku nikamwambia kama hutaacha tabia hii,mi nahama,sitoweza kuvumilia aibu itakayo kuja hata kama hutaki kukubali.
Siku moja jamaa ameingia saa 19:30 jioni na kutoka 07:30 asubuhi,jamaa akaondoka,mimi nilikuwa kazini nahangaika na mimi,mimi nilitoka saa 11jioni,nikawa nimepumzika ndani,ilipofika saa 23:30 usiku nikaona jamaa anagonga mlango wangu,huwa ni kawaida yake kwa kuwa mimi ni mshikaji wake hunigongea na kumfungulia,kisha kwenda kwake chumba cha mbele,jamaa alivyonigongea tu muda huo nikanyanyuka kwenda kwanza kugonga kwa yule dada,nilipogonga akafungua mwanamke nikamwambia huo mchezo wenu utawafikisha pabaya,mumeo amerudi,mdada akaaanza kutetemeka na kumwambia mjamaaa wake atoke,walipomaliza kutoka nikaenda kumfungulia jamaa mlango akaenda kwake,kumbuka alitakiwa atoke asubuhi,akaja kidole kimekatika mfupa amejikata na machine ya kukatia bati,alipelekwa Muhimbili saa 20:30 usiku,akatibiwa,wakaona jeraha sio kubwa wakamruhusu aende nyumbani,ndipo alipokuja na kumfungulia,na ndio mkasa ulivokuwa,sikukaa muda nikahama ile nyumba,siku moja jamaa akasikia fununu kwa watu kuwa yule jamaa mwingine alikuwa anammega mkewe,akanipigia simu kwanini nilikuwa namficha siku zote hizo? Jamani wadau je mimi nina kosa hapo?mimi nilikuwa namwambia jamaa yetu mwingine aacha kamchezo hako.
 
Kosa lako hukumwambia jamaa mwenye mali kama mali zake zinaliwa
Sometimes as you make your bed so you must lie upon it.....
 
Kosa mbona liko wazi, ungetumia njia yoyote kustopisha haya mahusiano, hata ingebidi ungenunua new line(ujidai sio wewe) uwatumie sms huyo mwenzio na pia mke wa bro kuwa kila kitu kipo open na wasipoacha mh, watakiona cha moto.
 
Mkuu hapa una kosa huna jinsi ya kuepa...Ulijua jamaa anakula mke wa jirani yako hukumwambia wakati weye ndio mfungua mlango na mlikua mnaheshimiana???
Omba radhi kwa mme mtu... na utafute lugha nzuri ya kujitetea....haina jinsi
 
JF Shalom!
Je, mtu aweza kutia moto kifuani pake,
na nguo zake zisiteketezwe?

Je, mtu anaweza kukanyaga makaa ya moto,
na nyayo zake zisiungue?

Ndivyo alivyo aingiaye kwa mke wa jirani yake,
kila mtu amgusaye huyo atakuwa na hatia.

Mithali 6:27-29

Mtu aziniye na mwanamke hana akili kabisa;
afanya jambo litakalomwangamiza nafsi yake

Atapata jeraha na kuvunjiwa heshima,
wala fedheha yake haitafutika;

maana wivu ni ghadhabu ya mtu,
wala hatahurumia siku ya kulipiza kisasi;

hatakubali ukombozi uwao wote,
wala hatokuwa radhi, ujapomlipa vitu vingi

Mithali 6:32-35
 
Du, mkuu kwa hiyo wewe ukiona mwizi anavunja nyumba ili aibe utamwangalia tu? Njia za kuzuia uhusiano huo mbovu, zilikuwepo nyingi sana. Lakini pole unapaswa kulaumiwa.
 
Mwanamke malaya asiye na haya aingizaye wanaume ndani ya nyumba ya mumewe ni janga la maisha. Naye huyo aliyefanya hivyo alikosa hekima. Mtu mwenye mkewe akikukamata, nani ajuaye ni nini atafanya?

Ukiona mwanaume anakubaliana na mwanamke malaya kufanya ufuska, basi huyo mwanaume ni mpumbavu. Maiti ya mwanamke huyo inamualika na yeye kufa ila yeye hajui.

Mwanaume kushauriwa na mwanamke ni UPUMBAVU. Yeye anayekwambia mume wangu hayupo na wewe unakuwa mjinga zaidi yake, siku ya fumanizi lako majuto yako yatakurutubisha motoni.
 
Kosa mbona liko wazi, ungetumia njia yoyote kustopisha haya mahusiano, hata ingebidi ungenunua new line(ujidai sio wewe) uwatumie sms huyo mwenzio na pia mke wa bro kuwa kila kitu kipo open na wasipoacha mh, watakiona cha moto.

kUMBUKA NILIMWAMBIA SANA,SANA Jamaa,age mate wangu,ingawa alikana bt ukweli nilimwambia,hufu yangu ya kumwambia bro mkubwa ni kwamba ningemwambia sijui angelipokea vipi na kumwelezaje mkewe coz nilikuwa nini hofu ya kumpenda sana mkewe,je mkewe labda angeambiwa kisha mkewe akanigeuzia kibao kuwa nilimtaka akanitolea nje ndo maana namponda....sikutaka hiyo kabisa,coz pia sikukaa kimya pia nilimwambia jamaa yangu aache mchezo ingawa alikana,siku ya siku ndo ikatokea,pia nilikuja kumwambia ingekuwaje kama ningemfungulia direct jamaa bila kuja kugonga....niliyajua yote hayo.Anyway jamaa bado ananilaumu,coz ilituchukulia kama wadogo zake,haswa mimi kuwa kimya.
 
Kosa lako hukumwambia jamaa mwenye mali kama mali zake zinaliwa
Sometimes as you make your bed so you must lie upon it.....

niliogopa kaka,tena sana,huwezi jua watu wanapendana vipi,je mimi ningekuwa chanzo cha kuachanisha ndoa yao? sikutaka hayo yote yanikute....sikumfuata mwanamke kumwambia nilimfuata jamaa yangu mwanaume mwenzangu,ingawa alinikatalia....bt nilimweleza,kumweleza mwenye mali...ahaaa watu hawa huenda likanigeukia mimi,ili niwe huru niliamua kuhama nyumba ile,pia kama akizidi kunitafuta kunilaumu,napanga kumtafuta mtu mzima kwenda kwa jamaa ili akamueleweshe ramira yangu na hatua nilizochukua,ingawa yeye anaweza kutoamini kama nilichukua hatua,coz mwizi hakuacha kuiba,so hatua zangu zaweza zisijulikane au kuaminika/au kuzaa matunda.
 
Kosa lako hukumwambia jamaa mwenye mali kama mali zake zinaliwa
Sometimes as you make your bed so you must lie upon it.....

hivi ni rahisi kusema eee?
Mimi ningemjibu "sijakwambia sababu hayanihusu yale ni mambo yenu binafsi.
Malizana wewe na mkeo tena ukome ku niuliza mambo ya kifala"
 
hii ni kweli?
Aisee ni kweli kabisa mkuu,niliwaza sana kwanini jamaa alijikata kazini kidole na mashine na kuwahi kurudi home badala ya kesho yake,then akaja mapema mfupa wa kidole chake ukiwa nje.namshukuru Mungu mkuuu after 3 months to come,sitokuwa naingia shift rotation.like night,evening,morning.
 
niliogopa kaka,tena sana,huwezi jua watu wanapendana vipi,je mimi ningekuwa chanzo cha kuachanisha ndoa yao? sikutaka hayo yote yanikute....sikumfuata mwanamke kumwambia nilimfuata jamaa yangu mwanaume mwenzangu,ingawa alinikatalia....bt nilimweleza,kumweleza mwenye mali...ahaaa watu hawa huenda likanigeukia mimi,ili niwe huru niliamua kuhama nyumba ile,pia kama akizidi kunitafuta kunilaumu,napanga kumtafuta mtu mzima kwenda kwa jamaa ili akamueleweshe ramira yangu na hatua nilizochukua,ingawa yeye anaweza kutoamini kama nilichukua hatua,coz mwizi hakuacha kuiba,so hatua zangu zaweza zisijulikane au kuaminika/au kuzaa matunda.

tena kaa mbali kabisa bora utuambie sisi wanammu kuliko kumwambia mjamaa
 
Nawe ulkua mmoja wao kwa usali huo, ingekua mimi ningemfungulia jamaa bila kuwashtua kwa sababu alikataa kukuambia ukweli ilhali wewe unaujua ukweli, ungejifanya hujui km jamaa yupo ndani kwake.
 
Mkuu hapa una kosa huna jinsi ya kuepa...Ulijua jamaa anakula mke wa jirani yako hukumwambia wakati weye ndio mfungua mlango na mlikua mnaheshimiana???
Omba radhi kwa mme mtu... na utafute lugha nzuri ya kujitetea....haina jinsi

Kaka ilikuwa ngumu,mazingira,hujui ni kwa kiasi gani jamaa anampenda mkewe,na jinsi ge hayo yanikuteani atamweleza,niliogopa jee lingeweza kunirudia mimi,mkewe anaweza kumwambia mimi ndo nilikuwa namtaka akanitolea nje,ndo nikaanza kumchongea kwake,sikutaka yote hayo yanikute,sikutaka niwe chanzo cha either kuvunja ndoa yao.niliona nimwambie tu huyu jamaa mwizi,ingawa alikana mwanzoni.unaweza kumwambia kwa uzuri mwenzio akifika kitandani anakumbatiwa na kuambiwa kuna watu wambea na wachochozi kwa ndoa yetu,kesho kibao kinanigeukia,sikutaka kabisa,angekuwa ni kijana mwenzangu ningejua hata namna ya kumuingia,ningesha msoma...labda ningemweleza.
 
Back
Top Bottom