Nilimpenda sana Samia alipoingia madarakani

Luca Paguro

JF-Expert Member
Joined
Mar 26, 2023
Posts
476
Reaction score
1,060
Kiukweli Magufuli alipofariki niliumia sana, lakini pia nilifurahi kuona Tanzania inapata Rais mpya wa kike. Nilikuwa niko curious kujua uongozi wake utakuwaje na nilikuwa na matarajio makubwa sana juu yake
Kwa kuwa Magufuli alikuwa anapenda sana kuanzisha megaprojects nyingi za kutatua matatizo ya wananchi kwa haraka nilidhani na Samia itamlazimu kuwa hivyo ili kuepusha lawama, nilidhani atakuwa kama Magufuli maana ipo wazi Magufuli alikuwa anaipenda sana Tanzania, na alikuwa anawapenda Watanzania, alikuwa genius mno na mzalendo namba 1 kwa hiyo nilitegemea amemwambukiza Samia hizi tabia

Kitu nilikuwa sikipendi kwa Magufuli ni habari za kuteka na kuwapoteza watu. Huu ilikuwa ni ukatili na moja ya madhaifu yake makubwa, niliamini Samia atakuwa tofauti ila ndio kwanza kaja kuzidisha utekaji mara 4 hata ya Magufuli, huyu mama katili jamani. Magufuli ni cha mtoto

Binafsi naona Magufuli na Tundu Lissu wanatofautiana mitazamo ya kisiasa lakini wote wawili ni wazalendo sana. Ila huyu Samia sio mzalendo hata kidogo

Yani nilimpenda hadi nikaanza kumpamba nikiona watu wanamsema vibaya, hata sikuwa na shaka naye lakini hiki kipindi kuelekea uchaguzi ndio nimeziona rangi zake halisi huyu mama. Dahh, aisee duniani kuna watu wana roho ngumu. Samia amenichukiza mno, nimeacha kumpenda ghafla imefika hatua hata nikiona video zake tu anaongea najisikia vibaya sana, zile video za October 29 zinanijia kichwani. Miezi imepita lakini wale watu waliouawa nikiwafiria moyo wangu unaumia sana. Najisikia vibaya mpaka leo, na hapo ndio kusubiri tu hadi 2030 atoke madarakani lakini bado najisikia vibaya. Kweli unatoa amri watu wengi vile wauawe ili tu ubaki madarakani? Kwa hiyo maisha yao hayana umuhimu kuliko wewe kujitoa madarakani. Kwani huko Ikulu kuna nini, mbona sio lazima uwe Rais kama tunkuna kundi kubwa la watu halikupendi? Huyu mama hadi amepelekea sasahivi mada za dini zimeshika kasi, yupo tayari kuchonganisha Watanzania kupitia dini zao ili tu abaki madarakani.

Mimi sio mpenzi wa siasa ila safari hii zimejua kunikwaza. Najitahidi kusahau tukio la October 29 lakini nashindwa. Wengi wanaonekana wameanza kusahau ila mimi nimeshindwa. Kila nikiamka nakumbuka Samia ndio Rais wa Tanzania na aliamuru watu wauawe kwa kosa la kutaka kuipindua serikali yake, yeye akaona adhabu inayowafaa ni kifo. Dah
 
Dah nikikumbuka ila march 2021 wakiwa dodoma kwenye kuaga mwili wa hayati Jpm
SSH alipotamka kuwa Mimi ndiye Rais wa JMT nilikuwa nimeketi zangu kibarazani nasononeka lkn ghafla nilijawa na furaha na Matumain mapya
Ila sahvi bac tu😢
 
Utaendelea kumpenda tu baada ya muda, pale akili Yako itakapotulia kutoka katika makucha ya haters wa Samia waliojazana humu na kwenye mitandao mingine na kukuteka akili. Kwakuwa watashindana lakini hawatoshinda, basi ukweli utakuwa wazi na utajuta kutompenda angalau kwa mwezi mmoja.
 
Dah nikikumbuka ila march 2021 wakiwa dodoma kwenye kuaga mwili wa hayati Jpm
SSH alipotamka kuwa Mimi ndiye Rais wa JMT nilikuwa nimeketi zangu kibarazani nasononeka lkn ghafla nilijawa na furaha na Matumain mapya
Ila sahvi bac tu😢
Endelea kusononeka lakini hakuna kiongozi ambaye angevumilia nchi kiwashwa moto na kundi la kina ,ange, maria na chadema.
 
Hapana, sasahivi namuona muuaji tu. Hivi unajisikiaje kutoa amri ya kuuliwa watu wengi kikatili vile. Kwani angejiuzulu angepungukiwa nini 😔
 
Dah nikikumbuka ila march 2021 wakiwa dodoma kwenye kuaga mwili wa hayati Jpm
SSH alipotamka kuwa Mimi ndiye Rais wa JMT nilikuwa nimeketi zangu kibarazani nasononeka lkn ghafla nilijawa na furaha na Matumain mapya
Ila sahvi bac tu😢
Endelea kusononeka lakini hakuna kiongozi ambaye angevumilia nchi kiwashwa moto na kundi la kina ,ange, maria na chadema.
 
Hapana, sasahivi namuona muuaji tu. Hivi unajisikiaje kutoa amri ya kuuliwa watu wengi kikatili vile. Kwani angejiuzulu angepungukiwa nini 😔
Tulia ndugu, Kuna siku akili Yako itatulia na utajua kuwa mnyororo wa usalama wa hii nchi ni mrefu mno na si wa kispotispoti na utagundua kuwa Samia huyo mnamuohea tu sababu ndiyo mnyonge wenu. Jikuulize kidogo, hivi alikuwa amirijeshi mkuu wakati ule Hadi atoe hiyo amri uliyosema?!!! Unafikiri ungekuwa wewe ni Raisi basi lile suala lingeisha tu kwa wewe kujiuzulu?!!! Tafakari vizuri sana sana, hata usikurupuke.........mambo hayapo kabisa unavyofikiria hapa kwetu. Hata huyo warioba anaelewa vizuri tu, usimuone mitandaoni humu akivizia mgao wa tone tone wa chadema
 
Ungemtolea posa mapema,sahivi kikwete kakupiku
 
She's a Bloodthirsty kaffir, abductor and shameless killer.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…