Nilimpenda, akanifanyia mbwembwe hadi akani-block kwenye social media. Sasa anadai ananipenda!

Tiger B

Senior Member
Dec 21, 2016
138
250
Miaka mitano iliyopita nikiwa chuo nilimpenda binti fulani. Nilimweleza azma yangu ya kutaka kumwoa baada ya sisi kuhitimu. But akakataa. Siyo kukataa kwa kawaida, two years ninastruggle kwake but nilichoambulia ni block za social media, dharau, kejeli, eti kwamba mimi siyo wa hadhi yake.

Nilikuja gundua kuwa ana jamaa fulani anayemtegea amuoe, but to her suprise jamaa ameoa mtu mwingine.

Ni miaka mitatu sasa tangu nifute mawasiliano naye permanently but now kupitia rafiki zangu anahaha kwamba eti ananipenda, na yuko tayari nimuoe.

Kiukweli nahisi hii ni demotion, yaani kwamba amekataliwa kwingine ndo aje kwangu, after all those good years? Binafsi nipo single, but sijihisi kabisa kuwa na yeye, though my friends wananisihi sana eti nisimwache, kwamba anaumia sana juu yangu nk..

JF naombeni ushauri wenu. Ahsanteni sana.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom