Tegelezeni
JF-Expert Member
- Dec 31, 2009
- 268
- 124
Mimi ni kijana mwenye umri wa miaka 37 na nina mke na watoto watatu sasa. Kikazi mimi ni mtumishi serikalini na mke wangu by Professional ni mpishi na pia anao ujuzi kidogo wa ushonaji. Mke wangu alikuwa na ndoto za kumiliki biashara ya Catering wakati namuoa kwa sababu aliwahi kufanya kazi kwa mtu mwenye biashara hiyo alipokuwa kwao Mbeya kabla sijamuoa na kuhamia naye Dar, hivyo alitengetengeneza picha kuwa biashara ya Catering ndio biashara pekee yenye faida kubwa.
Ni kweli kuwa biashara ya Catering ina faida kubwa lakini inategema na mtaji utakaoanzishia biashara hiyo. Kusema ukweli nilikuwa na dhamira ya kumuanzishia biashara hiyo ya Catering na nilianza mchakato wa kutekeleza azma yangu, lakini nikakutana na vikwazo vingi sana, kwani ili kuanzisha biashara hiyo ni lazima uwe na vifaa kama Serving Dishes, maturubai, viti na meza, vyombo vya kupikia, sahani, vifaa vya Mziki na MC.
Kama ukimudu kuwa na vitu hivyo basi na faida yako itakuwa kubwa kwani shuguli utakazokuwa unapata zitakuwa ni kubwa na zenye kulipa faida kubwa. Kwa mfano hapa Dar shughuli kama harusi, Send Off, Kitchen Party, Misiba, na kumaliza misiba wengine huita kumaliza arobaini, Vipa imara achilia mbali semina ndogo ndogo za kidini na za NGO's, zote hizo ni kazi ambazo zinategemea sana watu hawa wa Catering, lakini kutokana na mtaji wangu kuwa mdogo nikajikuta nikikwama kwa sababu nilikuta vifaa hivyo vinauzwa ghali kutokana na watu wengi kukimbilia biashara hiyo kwa kuwa inalipa.
Nilikata shauri kumfungulia biashara nyingine ili japo asikae bure bila kazi na pia kuokoa hizo pesa tusije tukazifuja bure. Kwa haraka, niliamua kuanzisha biashara ya ushonaji, pamoja na duka la kuuza vifaa vya ushonaji. Awali nilipata upinzani mkubwa sana kwa mama watoto na hakupenda hilo wazo langu kabisa, nilipata wakati mgumu sana kumuelimisha mpaka akakubali lakini hakuwa na mwamko wa kuipenda kazi hiyo. Sikukata tamaa, niliendelea kumuelimisha huku nikiendelea kununua vifaa kama vyerehani vitatu na cha kudarizi kimoja pamoja na vifaa vya ushonaji vya kuweka dukani kwa ajili ya kuuza na vifaa vingine muhimu kama makabati na kadhalika na kulifungua duka hilo rasmi. Hata hivyo nilimuahidi kuwa ahadi yangu iko pale pale, nitamfungulia biashara yake ya Catering kama nilivyomuahidi wakati ukifika.
Hata hivyo mwanzoni hakuipenda biashara hiyo na nilikuwa kama vile namlazimisha kwenda dukani kufungua kila siku asubuhi, lakini sikukata tamaa.
MSHANGAO………..
Siku za karibuni biashara ikaanza kukua na wateja wakaanza kuja kwa wingi kununua bidhaa, na mtaji umeanza kukua sasa. Hivi karibuni katika mazungumzo yangu na yeye nikamwambia kuwa mpaka mwezi wa pili mwakani nitakuwa nimemfungulia biashara yake ya Catering kama nilivyoahidi, ili ndoto yake itimie, lakini kwa mshangao aliruka na kukataa kabisa kuwa hataki tena biashara ya Catering kwani ile biashara ya ushonaji ina faida na ameipenda sana. Sikuamini masikio yangu. Unajua wakati nabishana naye kuhusu kuanzisha biashara ya ushonaji nilidhani yeye yuko sahihi kuwa hiyo biashara haifai, na ilikuwa nusura nikubaliane naye, ila kuna kitu huwa tunaita machale au mlango wa sita wa fahamu, ambao huwa nautumia katika kufanya maamuzi magumu.
Baada ya kutafakari sana niliamua kufungua hiyo biashara, na sasa nimepata jibu kuwa nilikuwa sahihi, maana ameuona ukweli kuwa wazo langu lilikuwa ni sahihi. Kuna msemo mmoja unasema kuwa mwanaume ni kichwa cha nyumba, ki ukweli sikuwa nauzingatia huo msemo kwa kuwa niliona ni dalili ya kujikweza na kuwadhalilisha wanawake, lakini nadhani hiyo dhana ina ukweli fulani.
Nimejifunza jambo moja, kuwa kuna wakati mwanaume analazimika kuwa dikteta ili kufikia maamuzi fulani magumu, hasa pale mke anapoonekana kupinga bila kutoa wazo mbadala au kutoa ushauri. Sio kwamba wanawake hawawezi kutoa ushauri au wazo zuri, la hasha, ninachomaanisha hapa ni kwamba kuna wakati kunapohitajika maamuzi magumu, mume anatakiwa kupewa nafasi ili aamue. Ila inategemea tabia za mume huyo.
Inasemwa kuwa nyuma ya mafanikio ya mume kuna mke na nyuma ya anguko la mume kuna mke pia, lakini huwa najiuliza, je utamjuaje mke ambaye maamuzi yake yanakupeleka shimoni?