kidunula1
JF-Expert Member
- Apr 2, 2016
- 6,299
- 6,331
Nakumbuka mechi ya Simba 4 Yanga 1 mwaka 1994. Kipindi hiki nikiwa na miaka 9 hv ilipigwa game uwanja wa shamba la bibi. Masatu aliweka kamba ya kwanza kwa upande wa Simba na Kimanda akasawazsha. Kilichofata Simba walipata magoli mengine matatu ambapo mawili kati ya hayo ckumbuki waliofunga.
Goli ninalolikumbuka sana na lililonitia simanzi hadi nikakataa kula ni lile la nne lililofungwa na Dua said. Goli lile liliniumiza kwa sababu mpira walikuwa nao Yanga mara gafla nikiwa nimekaa kwa makini pembeni ya redio, from no where mtangazaji (nimeshamsahau alikuwa ni nani) akaanza kutaja jina "Dua, Dua,Dua,Dua! hadi sauti ikakata. Baada ya sauti ya mtangazaji kukata nikasikia tu kelele tu za washabiki waliokuwa wakishangilia. Sauti iliporudi mtangazaj akasema "Dua bin Said cjui nini na nini.... anaipatia Simba goli la 4"!
Kwa kweli iliniuma sana cz kabla ya kelele za Dua kuanza mpira walikuwa nao Yanga tena kwenye eneo la Simba hivyo niliamini pengine Dua Said alinasa mpira toka kwa mchezaji wa Yanga ila alifanyafanya blunder mwishowe Yanga wakapokonya mpira na kufunga goli la pili. BADALA YA GOLI LA 2 KUMBE LILIKUWA LA 4. HAKIKA SITAISAHAU HIYO MECHI!! Kama kuna mdau anayevikumbuka vikosi vya timu ktk ile mechi atupie tafadhali.