Nilikuwa teja sasa ni mchungaji

Nilikuwa teja sasa ni mchungaji

Winner80

Member
Joined
Feb 9, 2021
Posts
20
Reaction score
19
Mara nyingi ninapo kaa chini, na kutafakari safari nzima ya maisha yangu,

kule Mungu alikonitoa, mpaka hapa aliponifikisha, naishiwa maneno ya kumshukuru.

Ndio maana hata sasa ninasema ya kwamba Yeye ni Eben-Ezer, nikimaanisha ya kuwa Mungu ndiye amenisaidia, kufika hatua hii niliyofikia.

Maneno ya kitabu cha Zaburi 119:17 yanayosema; "Ilikuwa vema kwangu kuwa naliteswa, ili nipate kujifunza amri za Mungu” yanaelezea sana ushuhuda mzima wa maisha yangu.

Magumu, shida na mahangaiko yote niliyopitia vimetumika kama daraja la kunivuta karibu sana na Mungu.

Zaidi ya mimi binafsi kuokolewa, ninaamini ushuhuda wa maisha yangu unaniweka kwenye nafasi ya kuwa msaada kwa wengi walio katika changamoto kama nilizopitia mimi.
 
Karibu ujipatie nakala ya kitabu changu kinachokwenda kwa Jina la #NILIKUWA_TEJA_SASA_NI_MCHUNGAJI

Kitabu hiki kinapatikana kwa bei nafuu kabisa ya shilingi 7,000/= za kitanzania.

Unaweza kununua nakala yako kwa

Tigo Pesa
0659-409447

M-PESA 0767 879406

Airtel Money 0789 795435

Hakikisha unanitumia na majina yako kamili.

Kwa huduma ya (delivery) utachingia nauli kidogo.
Barikiwa
@pastorwinner80
Ukonga
February 12,2021View attachment 1701077View attachment 1701078
Ungeshusha hata page mo1 ktk hicho kitabu ili kutuvutia

Anyway nakutakia safari njema ya uuzaji vitabu vyako
 
Ndio utumbo gani huu umetuletea hapa
Jifunze kuheshimu kitu cha mwenzako mkuu, iwe mawazo au kazi yake

Usimzarau mtu mkuu hii Dunia, na uwezi jua nani atakusaidia
Nina ushuhuda wa watu niliowadharau lakini leo hii wameniacha mbali sana ingawa naamini ilikua ni akili isiyo komaa hivyo sikupaswa kuhukumiwa

Mkuu haya maisha tuu, jamaa katumia muda wake na gharama zake kuandaa hicho anachosema kina mafundisho ndani yake

Wakati mwingine jifunze kupita kimya si lazima ukomenti
 
Baba mchungaji huna haja ya kujibu watu kama hao halafu leo jumapili
 
Ni hatua nzuri ni muhim kwa watu wanaoshinda hii vita wakasema wameshinda vpi ili kuwasaidia wengine
 
Sasa ndugu Mchungaji usisahau ukifanikiwa kutoa charity najua mateja wengi watakaotaka kupata motivation hizo buku saba watazitumia kwa jambo lingine..., hence kwa kusaidia jamii, ukishapata za kutosha tengeneza pdf (haina gharama) wape wadau vijiweni bure (ingawa watakupiga mawe) ila ndio utumishi wenyewe huo

Addiction ni mbaya sana bora wawe addicted kwenye Imani (no matter hata kama imani hio ni ya ukweli au hapana, so long as haidhuru wengine)
 
NILIKUWA TEJA SASA NI MCHUNGAJI SEHEMU YA KWANZA: (1)
PASTOR WINNER MAGERE 0659-409447
MWANZO WA YOTE;-
KUKATALIWA NA UCHUNGU

Kwa mara ya kwanza nikiwa darasa la nne nilitaka kujiua kwa kunywa sumu. Nilifika katika hatua ya maisha ambayo niliona ni heri kufa kuliko kuendelea na maisha ya mateso na uchungu.

Pamoja na umri wangu mdogo, nilikuwa nimeshapitia mambo magumu yaliyonifanya nione kwamba hakuna jema lolote ninaloweza kulitarajia katika maisha.

Kama ni mtu ambaye umeishi kwenye familia yenye upendo, amani, maelewano na malezi mazuri kutoka kwa wazazi, unaweza usielewe sana kuhusu roho ya kukataliwa na uchungu.

Leo tuna watoto wengi wapo mitaani siku siyo kwa
sababu wao ni wabaya na watukutu, bali ni kwa sababu mioyo yao imejawa na uchungu unaotokana na kukataliwa na watu wao wa karibu.

Ndivyo ilivyokuwa kwenye maisha yangu ya utotoni. Tangu utoto wangu, nilijifahamu kuwa ni mtu nisiyependwa, niliyekataliwa na ninayeonekana kuwa mzigo kwa watu wangu wa karibu.

Baba yangu mzazi ni miongoni mwa watu walionifanya nione kuwa maisha ni magumu na nidhani kwamba duniani hakuna kitu kinachoitwa upendo.
Mara kwa mara nilikuwa nikipokea kipigo kisicho hata na chembe ya huruma kutoka kwa baba.

Binafsi niliona kwamba baba ni mtu anayenichukia sana kutokana na uzito wa vipigo alivyokuwa akinipatia bila ya kujali umri wangu mdogo. Jambo hili

lilinifanya nione kifo kipo karibu nami kama nikiendelea kukaa nyumbani. Kwa sababu hiyo, mawazo ya kutoroka nyumbani yalianza kuniingia. Zaidi ya yote, moyo wangu ulijawa na uchungu mwingi sana kutokana na mateso na taabu nilizokuwa nikizipata nyumbani itaendelea......
 
Kwa takribani masaa kumi na moja nilitembea kwa miguu nikiwa peku peku.

Hii ilikuwa ni safari yangu ya kutoroka nyumbani ili kwenda kutafuta ahueni mjini.

Nilitembea kutoka kijiji cha Kiagata wilaya ya Musoma Vijijini hadi Musoma Mjini kwa muda wote huo.

Hadi nafika Musoma Mjini, vidole gumba vya miguuni vilikuwa vimejaa maji kwa sababu ya mwendo mrefu.

Jambo hilo liliniachia alama ya kudumu ya kupoteza kucha kwenye vidole gumba vya miguuni.

Taarifa zangu zilikuwa zimeenea kwa ndugu zangu mbalimbali, waliopo mkoani Mara na Mwanza. Hazikuwa taarifa njema sana, bali ni maneno ya kuonyesha kuwa mimi ni mtoto mtukutu, mkorofi, mwenye kiburi na niliyeshindikana.

Hili lilisababisha nisiweze kupata msaada, pamoja na kuwa na ndugu wengi wenye uwezo.

Mtazamo hasi waliokuwa nao kuhusu mimi uliwafanya ama wanikatae, au wanigeuze kuwa mtumwa wao.

Niliwachukia sana baadhi ya ndugu ambao walikuwa wakieneza uongo huo kuhusu mimi. Siyo kwamba walikuwa wakieneza habari za uongo tu, lakini pia walikuwa wakiwaonya ndugu na jamaa zetu wasinipokee kabisa na wasikubali kuishi pamoja nami.

Ukweli nilikuwa naonekana kama ni laana inayotembea. Kuna baadhi ya ndugu waliamua kunipokea, japo kwa lengo la kunigeuza mfanyakazi wao wa nyumbani.

Nilitumikishwa katika shughuli mbalimbali za nyumbani hadi za kwenye hoteli. Muda ambao watoto wenzangu walikuwa wanakula, mimi nilikuwa napewa kazi. Muda ambao wenzangu wanaenda kulala, mimi nilikuwa napewa kazi.

Ilikuwa ni mfululizo wa kazi zisizoisha asubuhi hadi usiku, moja baada ya nyingine. Mbaya zaidi ni kwamba, kuna wakati nilikuwa napewa kazi muda wenzangu wanakula. Hadi namaliza kazi, nakuta chakula kimeisha na watoto wenzangu wapo wanaangalia luninga.

Hakika, nilikuwa na wakati mgumu sana itaendelea.

Pastor Winner Magere
Ukonga
+255 659-409447
February 15,2021

IMG_20210112_233546_475.jpg
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom