Nilikua sijui wengine huku wanalipwa

nusuhela

JF-Expert Member
Jan 26, 2014
5,824
7,111
Kumbe wanaobishana mitandaoni kuhusu siasa wanalipwa na ndo kazi zao za kuwaingizia kipato?.

Nilikua nachoma mafuta yangu bure siku zote hizo? . Ndio maana nilikua nashangaa!.

Kwanini watu wanatetea mpaka uozo? Kumbe wenzangu wapo kazini. Laiti ningejua, nisinge maliza vocha zangu bure. Maana wenzangu wanabill ya vocha. Mimi nilijua kampeni zikiisha basi sisi wananchi wakawaida tunakua wasimamiaji wakuu wa serikali.

Badala yake tumegeuka na kuwa mashabiki! Kusema kweli watanzania, moja kati ya vitu vinavyosababisha sisi kuumizwa na viongozi wa serikali, ni yale mahaba tuliyonayo kwenye vyama vya siasa. Hatujui wajibu na haki zetu ndio maana tunayafanya haya. Leo ningependa tuelezane nini tunapaswa kufanya.

Kutokua mashabiki wa vyama vya siasa. Hii itatusaidia sana maana chama kitakachotuangusha, hatutasita kukiadhibu. Lakini kama tutaelekeza mapenzi kwenye chama cha siasa, basi hata kikiharibu basi sisi wenyewe ndio tutakaosimama na kukitetea wakati tunaangamizwa.
 
Tunatofautiana katika tofauti zetu na tunafanana katika ufanano wetu. Mungu ni mkubwa that's why some people are alive simply its illegal to kill them
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom