Katika harakati za kutafuta maisha na kujipatia pesa ya mkate nilibahatika kufungua frame yangu ambayo ilikuwa inahusika na ICT services kama kufunga networks nk ,pia kwa pembeni frame iliyofuatia niliwaajiri vijana 3 ambao walikuwa ni mafundi Ac na fridge hivyo tukipata dili aidha ya kufungia majumba za watu,kutengeneza,kusafisha nk kazi inakuwa inaendelea kama kawaida..
Kuna tabia nilijiwekea na imekuwa kama mazoea pale ofisini kuna miti imetuzunguka hivyo ndege hujazana mida ya jioni ,wakati wa kufunga ofisi na kuondoka huwa nachukua mchele na kuwarushia na wale ndege kwa furaha hulia na kuimba na kula zile punje za mchele,wale ndege mpaka wamenizoea ikifika jioni lazima utawakuta mtini na kama muda ukichelewa utawasikia wakilia basi naenda duka la jirani na kuchukua punje kadhaa na kuwarushia.Hakika urafiki wangu na hao ndege pamoja na njiwa umekuwa mkubwa mpaka wamenizoea nahisi siku nisipokuwa ofisini huwa wanasikitika na kuhudhunika
Sasa kumbe waswahili walikuwa wananichunguza na wakanikariri na maneno yakaanza mara mimi ni mshirikina ,mchawi ,nimepewa masharti na mganga na biashara yangu inategemea nyota na masharti na kitendo ninachofanya ni matekelezo ya masharti ya mganga.
Hayo maneno walikuwa wakiyazungumza chini chini na kusambaziana na kila ikifika jioni wakawa wananichunguza kama nitawarushia mchele hao ndege au laa.Bahati nzuri kuna msamaria mwema ananiheshimu na akanitonya na kunieleza hali halisi na kwa utafiti wangu nimehakikisha ni kweli naitwa mshirikina ,wale ndege eti ndio wanavuta watu kwenye biashara.
Mie nimebaki nacheka tu sababu siku zote nilikuwa sifahamu kama kuna watu walikuwa wananihisi mshirikina mpaka sasa hivi kisa tu kuwapa mchele ndege ..
Sasa waungwana mie nilikuwa ninafanya fair tu kuwapa chakula ndege na urafiki tu wa kawaida na hao viumbe ile nikiwaona wanaruka ruka na kufurahi wakila,na tukirudi nyuma mimi nilikuwa mfugaji mzuri tu wa Njiwa haswa aina ya fantail tausi,spidi ,vibwenzi,chotara nk labda athari ya ufugaji na mahusiano hayo yameniathiri.
Nataka kusitisha kuwarushia ndege hao mchele ili vijimaneno yamalizike na taswira yangu isiharibike lakini pia nataka niendelee tena nizidishe maradufu kama maneno izidi kusemwa,kuwarushia mchele ndege imekuwa nongwa khaa
Sema waTanzania wenzangu tubadilikeni ,vijimaneno,umbeya haufai tena wengine vidume kabisa wana ndevu hata mshipa wa haya hawana