Hapa Jamiiforums watu wanaona ni sehemu ya kupigia blah blah tu lakini kumbe ukiamua kukaa kufikiria yanayoshauriwa hapa utaona mengi yana umuhimu mkubwa
NJOO USOME HII
Nilikuwa kila nikitoa uzi wa kuomba ushauri mbalimbali kuhusu michepuko nilikuwa nashambuliwa kwa maneno makali sana, tena kama zile thread za yule wa kwenye daladala nilomlipia nauli halafu mume wake akanirudishia elfu 5 na nikaja gundua kuwa kumbe jamaa ana bastola, kwa kweli hiyo nilizongwa kwa maneno makali sana kuanzia hapa hadi wengine wakawa wananifuata PM kunishambulia.
Nikaona ushauri mwingi niliokuwa napewa ni za maana sana achilia mbali zile za waliokuwa wanaombea eti niliwe kiboga, nikapata mbinu sasa kwamba nimdanganye nimesafiri tu kupunguza kuwa karibu, tena basi mimi nipo kanda ya ziwa nikamdanganya eti niko Iringa na nitakuwa huko kwa miezi miezi mitatu nikajifanya pia nina masikitiko sana ya kumkosa kwa kipindi chote hicho yote hayo ili tuache kuonana, maana ilikuwa kila tukionana lazima atake kugegedwa tu.
Basi leo niliongea nae kwenye saa tano hivi asubuhi nikijifanya nalalamikia hali ya hewa ya baridi iliyopo huku akanipa pole huku anasema kanimiss sana, kwenye saa sita na nusu nikaenda kupata lunch kama kawaida na vibia viwili vitatu huku nimebadilisha na hotel maana nikienda ile ile ya siku zote kuna hatari ya kuonana, wakati natoka pale getini nikamkuta nae ndo anapaki gari ili aingie.
Nikajifanya sijamuona akaniita halafu akanisalimia, niliaibika sana.
Yaani hadi kazi hazikufanyika nabaki kujionea aibu mi mwenyewe huku najiuliza inakuwaje siku tukionana tena.