Nilichoshuhudia safari ya Dar mpaka Mwanza kwa basi

Nilichoshuhudia safari ya Dar mpaka Mwanza kwa basi

hahahahaha kisbo zinatembea mkuu, naifahamu kisbo moja ya tbr-dsm nyuma inabenderea ya tz, yule jamaa hana mshindani ukiwa umepanda bus lingine afu umekaa karibu nadereva utakasirika maana unakua unaiona bendera hyoo inamalizikia utasema dereva wenu anazingua)kama unapenda ligi lkn
 
Maswal Ya Maana Hayo, Lakin Majibu Yake Yapo Wazi Sanaaa....Unaweza Sema Kuuliza Hayo Maswal Ni Kujifanyisha Aujui!!!
Mkuu nisaidie kuna tofaut gan kati ya kuhoji na kuuliza swal maana inaonekana ni mwanafalsafa mzur
 
Akawa anakimbizana na City boy hapo hakuna matuta wala tambarare.City boy mbele sisi nyuma,sikutegemea kwa mwendo ule ilikuja mashine moja inaitwa Kisbo ilitupita sote kwa mkupuo na hatikuiona tena.
Hat stendi hamkuiona mkuu??

Ngoja Wilson Kabwe achunguzwe atakuja kutueleza hapa mikataba yake ikoje?
 
Mkuu hiyo KISBO ndio ile nyuma pana maandishi "kisu cha ngaliba"

Iliwahi nitoa nje ya barabara pale nyuma ya kongowe/kibaha jamaa ana overtake hata kama umemzuia siji kusahau.
 
Nilifika ubungo saa kumi na moja alfajiri,ndani ya kituo mazingira ni mabovu,hakuna sehemu ya kupumzika abiria pindi jua au mvua inapotokea,barabara za ndani ni mbovu mashimo kibao,sijui hizi pesa zinazokusanywa zinaenda wapi.

Nilikata tiketi ya Princess Muro aina ya zhong tong saa kumi na mbili safari yetu ilianza.
Kufika stendi Maili Moja napo vile vile kubovu kupita maelezo na bado wanakusanya pesa kwa mabasi yanayoingia pale kituoni.Nabaki najiuliza hizi pesa zinaenda wapi kama miundombinu ya kituo ni mibovu.

Tukatoka maili moja safari inaendelea kufika Mlandizi nao naona wameweka kituo kule bahati mbaya au nzuri hatukuingia tulinyoosha tu nadhani kule napo wanachangishwa pia.

Safari inaendelea mpaka Chalinze, hapa hakuna kituo cha makusanyo kama vilivopita nadhani ni suala la muda tu ukifika wataunda kituo cha kizushi zikusanywe tena.

Saa tatu kasoro inatukuta Msamvu Morogoro.Kwa kweli kituo hiki kipo katika ujenzi bado lakini kina hadhi kubwa zaidi ya huko nilipotoka.Pongezi ziende kwa manispaa, naamini mpaka kitakapokamilika kitakuwa na hadhi nzuri.

Safari ikaendelea mpaka kuingia Dodoma, bahati mbaya au nzuri tukachepuka pale maeneo ya Bungeni tukatokea Jamhuri na kuanza kuitafuta Manyoni.
Kituo cha Dodoma nacho pia ni cha hovyo ni kidogo sana,labda wakikamilisha kile kipya naona ndio kitakuwa na mazingira mazuri.Safari inaendelea tukaipita Manyoni na kuanza kuitafuta Singida mjini.

Nitamke wazi hili bus lipo poa sana kwanza si la kusimama hovyo,mwendo wa dereva ni wa wastani pale pa kutembeza gari anatembeza kweli kweli na pale pa slow down ni hivyo hivyo ana slow down.Saa kumi tupo Singida.Hiki sio kituo cha mabasi bali ni uwanja wa mpira wa shule ya msingi Tandale,vumbi mwanzo mwisho ,sijui hizi halmashauri zinafanya nini miaka yote.

Pale Singida akaingia dereva mwingine huyu kidogo zilifyatuka maana akaanza kutembeza gari kwa mwendo wa ajabu.Lakini pia nilipata picha fulani hata mavazi ya dereva pia yanaweza kukupa picha umakini wa huyo dereva.Yule wa mwanzo alikuwa kapiga suti safi nyeusi iliyomkaa vyema kama unakutana nae njiani unaweza kuhisi ni boss wa kampuni fulan.Huyu wa pili kapiga tshirt ya kubana kama za baunsa na pia chini kapiga jeans mpauko.

Akawa anakimbizana na City boy hapo hakuna matuta wala tambarare.City boy mbele sisi nyuma,sikutegemea kwa mwendo ule ilikuja mashine moja inaitwa Kisbo ilitupita sote kwa mkupuo na hatikuiona tena.

Kituo cha Shinyanga tuliingia kama saa mbili usiku lakini pia nacho ni kama kituo cha Dodoma.By saa nne usiku tunaingia Nyegezi Mwanza.Naomba wanaokujua wanifahamishe hivi Nyegez ndio kituo kikuu kabisa kwa Mwanza au ni kule Buzurugwa? Kwa sababu kama ni Nyegezi kwa hadhi ya jiji la Mwanza basi tuna safari ndefu katika ujenzi wa miundombinu.

Swali ninalojiuliza hivi hizi pesa zinazokusanywa vituoni huwa zinatumika kufanyia nini? Nijuavyo mimi kama unafanya biashara na inakuletea faida ni lazima utahakikisha unaweka miundombinu mizuri ili kuweza kupata faida zaidi.

Kwanza Mkuu ubarikiwe kuwa umefika salama huko Mwanza ila kuhusu usafiri wako ulivyokuwa nadhani mwenzetu Wewe una bahati kwani kwa sisi wenzako tuliokuwa tukisoma huko Mwanza miaka kati ya 2006 hadi 2009 hakyanani tulikiona cha moto hasa kwa aina ya magari yaliyokuwepo.

Sisi mlikuwa mkitoka tu Ubungo Dar abiria wote mnaambiwa musali kwa dini zenu huku mkikumbushwa je mmeshaacha wosia kwa Watoto zenu? Mkimaliza hapo Dereva anaanza kuwasha moto ( safari inaanza ).

Abiria tulikuwa tunaridhika tu kwa mwendo wa KINAFIKI ( wa pole pole ) wa kutoka tu pale Ubungo hadi Mizani ila kutoa Mizani hadi Chalinze kila mtu alikuwa anashika roho yake na kutoka Chalinze hadi Morogoro Msamvu ni hivyo hivyo roho mkononi.

Sasa hiyo ilikuwa ni tisa Mkuu ila kumi ni mkianza safari ya kutoka Morogoro hadi Mwanza nakuambia kwa Wewe ninavyokuona ulivyo mwoga ungeshakufa kwa presha. Huo mwendo wa haya mabasi mawili ya Allys na Zuberi ilikuwa ukisikia tu AJALI inayowahusu basi jua akipatikana Mtu mzima basi katika abiria 45 au 55 ukiwapata wengi ni 5 tu na hao nao wanapumulia masikioni kwa aina ya majeraha waliyoyapata ila waliobaki utasikia tu kuwa wenye Ndugu wakahakiki miili yao mortuary ya hospitali fulani.

Mtafute Mtu yoyote akupe SIMULIZI la hayo Mabasi mawili ya Dar - Mwanza miaka hiyo ujue kuwa Wewe hiyo gari uliyoipanda ilikuwa ni ya KILOKOLE tupu! Kikawaida tu Safari ya kutoka Dar hadi Mwanza huwa ni Saa kati ya 16 hadi 18 nikimaanisha kuwa mnatoka Dar Ubungo alfajiri Saa 12 na mnafika Mwanza usiku Saa 4 au Saa 5 ila kwa haya magari mawili Allys na Zuberi mnatoka Dar Saa 12 mnafika Dodoma Saa 5 au Saa 6 ila huko njiani mmeua sana Mbuzi na Ng'ombe za Watu zilizokatisha mbele yenu na Mwanza stendi mkichelewa sana mnafika Saa 1 ila ilikuwa Saa 12 jioni Mwanza hii hapa.

Ili uone kuwa haya Mabasi LAANA yake ilianzia mbali unaambiwa Wamiliki wao wakiwa wanatafuta Madereva wa kuendesha hizo basi Tangazo lao la Kazi lilikuwa kama hivi :

AJIRA AJIRA AJIRA

Kampuni ya Mabasi ya Allys na Zuberi inatafuta SIFA za Dereva kwa MSHAHARA mnono.

SIFA ZA DEREVA ANAYEHITAJIKA ni kama zifuatazo :

  1. Awe na UMRI wa kuanzia miaka 18 hadi 33.
  2. Awe na uwezo mzuri wa kuona ( hapa utadhani labda walikuwa wanatafuta pilot wa ndege ila nikagundua kuwa maana yao kubwa ya kutaka dereva aliye na macho mazuri ni kuwa awe na uwezo wa kuwaona Matrafiki kwa umbali mrefu ili aweze kuwakwepa ).
  3. Asiye MLOKOLE na awe mnywa Pombe ila siyo Saa za Kazi.
  4. Awe na uzoefu ama wa kusabisha ajali au kukoswakoswa au ameshawahi kuangusha Basi / Gari.
  5. Awe mbunifu na mwepesi wa kutambua njia za panya kwa uharaka ili kuwakwepa Matrafiki.
  6. Awe na uwezo wa kuendesha gari mwenyewe kwa Saa 20 bila kuchoka.
  7. Awe na uwezo wa kuendesha Basi kwa spidi ya 160 kama spidi ya hilo Basi mwisho wake ni 180 au awe na uwezo wa kuendesha Basi kwa spidi ya 180 kama spidi ya hilo Basi mwisho wake ni 200.
Sasa Mkuu kwa hizo SIFA za Dereva waliokuwa wakihitajika unadhani mortuary na kwa Bibi Cheza pale Muhimbili au Bigando au Dodoma au Shinyanga Maiti na Majeruhi wasingejaa? Haya Mabasi sitayasahau na sijui kama bado yapo ila kama yapo nasema Shikamoo Allys na Zuberi.
 
Saa tatu kasoro inatukuta Msamvu Morogoro.Kwa kweli kituo hiki kipo katika ujenzi bado lakini kina hadhi kubwa zaidi ya huko nilipotoka.Pongezi ziende kwa manispaa, naamini mpaka kitakapokamilika kitakuwa na hadhi nzuri.

Kuna vigogo wametumbuliwa hapo... ehee endelea
 
Back
Top Bottom