Nilichoshuhudia safari ya Dar mpaka Mwanza kwa basi

Nilichoshuhudia safari ya Dar mpaka Mwanza kwa basi

fdizzle

JF-Expert Member
Joined
Jul 29, 2015
Posts
1,902
Reaction score
2,405
Nilifika ubungo saa kumi na moja alfajiri,ndani ya kituo mazingira ni mabovu,hakuna sehemu ya kupumzika abiria pindi jua au mvua inapotokea,barabara za ndani ni mbovu mashimo kibao,sijui hizi pesa zinazokusanywa zinaenda wapi.

Nilikata tiketi ya Princess Muro aina ya zhong tong saa kumi na mbili safari yetu ilianza.
Kufika stendi Maili Moja napo vile vile kubovu kupita maelezo na bado wanakusanya pesa kwa mabasi yanayoingia pale kituoni.Nabaki najiuliza hizi pesa zinaenda wapi kama miundombinu ya kituo ni mibovu.

Tukatoka maili moja safari inaendelea kufika Mlandizi nao naona wameweka kituo kule bahati mbaya au nzuri hatukuingia tulinyoosha tu nadhani kule napo wanachangishwa pia.

Safari inaendelea mpaka Chalinze, hapa hakuna kituo cha makusanyo kama vilivopita nadhani ni suala la muda tu ukifika wataunda kituo cha kizushi zikusanywe tena.

Saa tatu kasoro inatukuta Msamvu Morogoro.Kwa kweli kituo hiki kipo katika ujenzi bado lakini kina hadhi kubwa zaidi ya huko nilipotoka.Pongezi ziende kwa manispaa, naamini mpaka kitakapokamilika kitakuwa na hadhi nzuri.

Safari ikaendelea mpaka kuingia Dodoma, bahati mbaya au nzuri tukachepuka pale maeneo ya Bungeni tukatokea Jamhuri na kuanza kuitafuta Manyoni.
Kituo cha Dodoma nacho pia ni cha hovyo ni kidogo sana,labda wakikamilisha kile kipya naona ndio kitakuwa na mazingira mazuri.Safari inaendelea tukaipita Manyoni na kuanza kuitafuta Singida mjini.

Nitamke wazi hili bus lipo poa sana kwanza si la kusimama hovyo,mwendo wa dereva ni wa wastani pale pa kutembeza gari anatembeza kweli kweli na pale pa slow down ni hivyo hivyo ana slow down.Saa kumi tupo Singida.Hiki sio kituo cha mabasi bali ni uwanja wa mpira wa shule ya msingi Tandale,vumbi mwanzo mwisho ,sijui hizi halmashauri zinafanya nini miaka yote.

Pale Singida akaingia dereva mwingine huyu kidogo zilifyatuka maana akaanza kutembeza gari kwa mwendo wa ajabu.Lakini pia nilipata picha fulani hata mavazi ya dereva pia yanaweza kukupa picha umakini wa huyo dereva.Yule wa mwanzo alikuwa kapiga suti safi nyeusi iliyomkaa vyema kama unakutana nae njiani unaweza kuhisi ni boss wa kampuni fulan.Huyu wa pili kapiga tshirt ya kubana kama za baunsa na pia chini kapiga jeans mpauko.

Akawa anakimbizana na City boy hapo hakuna matuta wala tambarare.City boy mbele sisi nyuma,sikutegemea kwa mwendo ule ilikuja mashine moja inaitwa Kisbo ilitupita sote kwa mkupuo na hatikuiona tena.

Kituo cha Shinyanga tuliingia kama saa mbili usiku lakini pia nacho ni kama kituo cha Dodoma.By saa nne usiku tunaingia Nyegezi Mwanza.Naomba wanaokujua wanifahamishe hivi Nyegez ndio kituo kikuu kabisa kwa Mwanza au ni kule Buzurugwa? Kwa sababu kama ni Nyegezi kwa hadhi ya jiji la Mwanza basi tuna safari ndefu katika ujenzi wa miundombinu.

Swali ninalojiuliza hivi hizi pesa zinazokusanywa vituoni huwa zinatumika kufanyia nini? Nijuavyo mimi kama unafanya biashara na inakuletea faida ni lazima utahakikisha unaweka miundombinu mizuri ili kuweza kupata faida zaidi.
 
Ha ha haaa. Mimi sijui kipi ni kipi , nakumbuka nlifika na fastjet nkachukua tax wakanpiga elf 30 hadi stand ambayo nlipanda bus nkaunga Bukoba. Nlimuuliza mtu hii ndio stand kuu? Akanjibu kuna nyingne kule sijui wapi so nkabaki njia panda.

Kilichonfurahisha kwako Mimi ni hizo mashine za KISBO, hizo gari sijui wamefunga engine za jet? Zinakimbia kiasi kwamba hata V8 yaeza subiri.
 
Zote ni stand kuu kwenda ndani na nje ya nchi, CCM haina uwezo wa kujenga nchi hata siku moja itajenga kwa vipande mpaka Yesu aje
 
Ila singida nadhani imelaaniwa kabisa!, ile stendi nahisi hawana mpango kabisa. Dodoma hakuna ujenzi mwingine wa stendi; pale ndio wamejenga kiwango cha mwisho. Walijaribu kufukuzia mabasi kule nanenane lakini wakashindwa, mabasi yakiingia 7 kwa mkupuo jua hapo roundabout magari hayapiti maana njia itakuwa imezibwa. Tanzania yetu wapiga dili wapo wengi sana!
 
Nimecheka tu hapo kwenye Kisbo ilivyowapita kama mmesimama.hayo magari na ya city boy huwa na mwendo mkali sana
Acha tu mkuu hiyo city boy tuliiacha mlandiz stend inapakia abiria sis tulinyoosha,nahis yule dereva aliyeitoa dsm hakuwa fasta sana,tulipotoka singida baada ya kupita mizani kuna tuta jamaa akatupita hapo then akakaa mbele yetu tukawa tunatembea nae mwendo wa maana mpaka utumbo unacheza mara nasikia upepo ndan ya gari umezid kugeuks kulia ni kisbo inapita mpka city boy ikapitwa yan ktk mazngira yale ikitokea ajali ukipona shukuru Mungu
 
Nyegezi ndio stand kuu ya mabasi ya Mwanza kwa kwenda nje ya mikoa/nje ya nchi,ila ile ya Buzuruga ni kwaajili ya mabasi yanayotumia njia ile ya upande ule.
Hili ndilo jibu sahihi kwa swali lililoulizwa. Kama unasafiri kutoka Mwanza kwenda Magu, Nassa, Bunda, Musoma, Tarime na Sirari basi wewe stendi yako ni Buzuruga.
 
Maswal Ya Maana Hayo, Lakin Majibu Yake Yapo Wazi Sanaaa....Unaweza Sema Kuuliza Hayo Maswal Ni Kujifanyisha Aujui!!!
 
Back
Top Bottom