Nilichoshuhudia leo asubuhi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nilichoshuhudia leo asubuhi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mohammed Shossi, May 28, 2012.

 1. Mohammed Shossi

  Mohammed Shossi Verified User

  #1
  May 28, 2012
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 3,986
  Likes Received: 123
  Trophy Points: 160
  Nimeshuhudia ajali mbaya sana kwenye mataa ya Chang'ombe na Mandela iliyohusisha magari mawili Toyota Coaster na Suzuki Grand Vitara mali ya serikali.

  Mimi ni mtumiaji wa barabara hii (makutano) mwezi uliopita waliwasha taa ambazo zimefungwa muda mrefu kabla ya hapo kuanza kuwashwa kwa mara moja. Taa zile zilikuwa kama mapambo tu na nadhani kilichowasukuma kuziwasha ni ajali zilizokuwa zikitokea na kuathiri taa za kuongozea magari (ambazo hazikuwa zikitumika) Ajali za mara kwa mara zilipelekea taa zile kuwa zinagongwa mara kwa mara na kuwekwa upya.

  Ajabu kubwa ni kuwa mita chache baada ya junction hii kuna kituo cha polisi na kituo cha polisi wa usalama barabarani mkoa wa Temeke! Wameshindwa kusimamia/kuongoza magari kwenye junction hii! utawakuta wamekaa kwenye vivuli kwa wauza maua huku watu wakionyeshana ubavu kupita!

  Kabla ya junction kuna zebra cross kwenye barabara zote ushauri wangu kwa Trafic wa mkoa wa Temeke waombe tochi ya kuangalia speed maana pale speed inatakiwa isizidi 30 km/hr lakini utakuta semi trailler inatoka bandari inapita na 120 km/hr.


  Na sisi tunaotumia hizi barabara tuwe wastaarabu tusiwe watu wa kuwahi unaweza kushindwa kufika kabisa huko unapowahi.

  Source Mimi mwenyewe picha na habari as reported on MICHUZI: Breaking Nyuzzzz: Ajali mbaya yatokea chang'ombe asubuhi hii
   

  Attached Files:

 2. mathematics

  mathematics JF-Expert Member

  #2
  May 28, 2012
  Joined: Feb 21, 2012
  Messages: 3,290
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 145
  Majeruhi walikuwa wangapi? Walionusurika?
   
 3. P

  Penguine JF-Expert Member

  #3
  May 28, 2012
  Joined: Nov 29, 2009
  Messages: 1,226
  Likes Received: 390
  Trophy Points: 180
  kweli hiyo mbaya!
   
 4. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #4
  May 28, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,345
  Likes Received: 19,529
  Trophy Points: 280
  asante kwa taarifa naushauri mzuri ...
   
 5. Watu8

  Watu8 JF-Expert Member

  #5
  May 28, 2012
  Joined: Feb 19, 2010
  Messages: 47,333
  Likes Received: 2,641
  Trophy Points: 280
  duh! kweli kuendesha dar kunahitaji ulinzi wa Maulana
   
 6. Mohammed Shossi

  Mohammed Shossi Verified User

  #6
  May 28, 2012
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 3,986
  Likes Received: 123
  Trophy Points: 160
  Nilipofika eneo la tukio hakukuwa na mtu hata mmoja ila nilimsikia mtu akisema aliekuwa nyuma ya Suzuki Vitara ameumia vibaya sana na ukiangalia chini utaona damu ni nyingi sana ilimvuja. Haijulikani kama amepona au la ila namuombea Mungu ampe afya.
   
 7. mizambwa

  mizambwa JF-Expert Member

  #7
  May 28, 2012
  Joined: Oct 8, 2008
  Messages: 4,409
  Likes Received: 568
  Trophy Points: 280
  Mungu ndiye anayetulinda na hawa Askari wala mlungula kutoka kwa madereva.

  Hapo ukiwakuta wamekaa pembeni ujue wanasubiri magari yagongane ili wakapate kidodogo toka kwa madereva.


  MUNGU AWALAANI Wote ASKARI PAMOJA na MADERVA WASIOKUWA MAKINI BARABARANI.  MIZAMBWA
  INANIUMA SANA!!!
   
 8. M

  Mkwe21 JF-Expert Member

  #8
  May 28, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 1,843
  Likes Received: 460
  Trophy Points: 180
  In this country no one is answerable!! - Abiria Chunga maisha na Mzigo wako!!
   
 9. sinafungu

  sinafungu JF-Expert Member

  #9
  May 28, 2012
  Joined: Feb 13, 2010
  Messages: 1,406
  Likes Received: 569
  Trophy Points: 280
  nawachukia traffic police wooote. hela mbele ubinaadamu nyuma.
   
 10. stephot

  stephot JF-Expert Member

  #10
  May 29, 2012
  Joined: Mar 1, 2012
  Messages: 5,023
  Likes Received: 2,641
  Trophy Points: 280
  Yaani hata mimi ma-askari Traffic siwapendi hawa ndio chanzo cha ajali kwani hamna wanachowaza kila kukicha zaidi ya rushwa.
   
 11. Tripo9

  Tripo9 JF-Expert Member

  #11
  May 29, 2012
  Joined: Sep 9, 2009
  Messages: 2,168
  Likes Received: 65
  Trophy Points: 145
  Leo nilikua roadini Arusha-Moshi road. Mishale ya saa kumi na nusu alfajiri.
  Barabarani imelala maiti iliyoonekana imegomgwa. Yebo yebo moja ipo huku nyingine kule. mwili ulinisisimka
  Na kwa kua tulipokua tunakwenda tumechelewa, dere wa gari yetu akakwepa ile maiti. Almanusra amgonge maana tulikua spidi.
  Na uhakika gari kubwa likipita lazima limeukanyaga ule mwili.

  Yaani nilisisimka kuona mtu kapoteza maisha yake kirahisis hivi hivi kwa uzembe ama wa kwake mwenyewe au wadereva.

  Watembea kwa miguu jamani tuweni makini. Angalia kwanza kushoto then kulia then kushoto then vuka kama usalama uko. Usivuke barabara ukiwa unakimbia pia ni hatari. Subiri magari yapite.

  Waendesha magari chondechote, mwendo wa kasi unaua waenda kwa miguu hasa kwenye maeneo ya makazi ya watu.

  DRIVE AND WALK SAFE FOLKS!
   
 12. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #12
  May 29, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,873
  Likes Received: 6,225
  Trophy Points: 280
  taa za hapo chang'ombe, za uhasibu na buguruni nadhani wameziweka kupamba mji tu.....
   
 13. rushanju

  rushanju JF-Expert Member

  #13
  May 29, 2012
  Joined: Nov 3, 2011
  Messages: 2,340
  Likes Received: 1,046
  Trophy Points: 280
  Siku moja nilisikia kiongozi mkubwa serikalini anaongea kwenye simu. Aliuliza hivi..... '' Unasema uko machinjioni uko machinjio gani maana temeke kuna machinjio matatu sokota Chang'ombe aU uasibu?'' My take... kama viongozi wenyewe wanaita machinjio na wakijua ni machinjio ya binadamu sisi wananchi tufabyeje?. .. Hizo taa ukifuatilia vema ilikuwa mradi wa wakubwa.
   
 14. ERIC JOSEPH

  ERIC JOSEPH JF-Expert Member

  #14
  May 30, 2012
  Joined: Aug 10, 2011
  Messages: 570
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  tunawapa pole sana wote wahanga wa ajali vp wamepona.madereva tuwe makin na maisha ya binadamu wenzetu
   
Loading...