Nilichojifunza uchaguzi wa Arumeru | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nilichojifunza uchaguzi wa Arumeru

Discussion in 'Chaguzi Ndogo' started by Kigarama, Mar 22, 2012.

 1. Kigarama

  Kigarama JF-Expert Member

  #1
  Mar 22, 2012
  Joined: Apr 23, 2007
  Messages: 2,479
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Kuna mambo mengi nimejifunza kutokana Kampeni za uchaguzi mdogo wa Jimbo la Arumeru, Haya ni baadhi yake.

  Tume ya uchaguzi bado haiaminiki na vyama vya Upinzani. Na kadri siku zinavyokwenda ndivyo shaka za tume hiyo kutumiwa kuipa ushindi CCM inavozidi kuongezeka. Na CCM nayo imeanza kuwa na shaka na Tume hiyo.

  Vyama vikubwa viwili kwenye kampeni hizo (CHADEMA na CCM) vinatumia mbinu za kuhama na mashabiki wake kutoka sehemu moja kwenda kwingine. Kutokana na Jimbo hilo kuwa karibu na Arusha mashabiki wa vyama hivyo wanaoishi Arusha wanahudhuria kwa wingi kwenye mikutano ya vyama hivyo.

  Vyombo vya habari vimeshachukua upande kwenye Kampeni hizi na ili upate ukweli wa hali ya mambo Arumeru ni lazima uwasiliane na watu wasio na upande wowote walioko Arumeru. Vyombo vya habari haviaminiki TENA.

  CCM ina uwezo mkubwa sana wa kutumia taasisi za dini kuendeshea kampeni zake kuliko wapinzani wake.

  Wapinzani wa CCM wanalalamika CCM inatumia rushwa kwenye kampeni lakini hawaziamini taasisi za kupambana na Rushwa na matokeo yake hawaripoti tuhuma hizo kwenye taasisi hizo zaidi ya kuzisema kwenye majukwaa ya Kampeni.

  Lowassa bado ana ushawishi chanya au hasi kwenye siasa za Tanzania, ndiyo maana kila mtu anatamani afanye kampeni Arumeru ili ama "amalizwe" au "awaonyeshe kazi" wapinzani wake.

  Kwenye kampeni hakuna ushindani wa sera au ubishani wa tofauti za kutatua matatizo ya wana Arumeru badala yake kumejaa tambo nani atashinda, kuumbuana, kampeni za kifahari, uzushi,kutukanana, kudhalilishana, kutishana, na mwisho wa yote sintofahamu isiyo na lazima.

  Nafasi ya mwanamke kwenye Kampeni bado ni kama haipo kwenye siasa za Tanzania. Kwenye Kampeni ya vyama vyote hakuna hata chama kimoja ambacho msemaji wake mkuu ni mwanamke. Wanawake waliopo Arumeru ni wapasha joto Microphone kabla "wenyewe" hawajapanda jukwaani.

  Na la mwisho na muhimu,ni kwamba mwaka 2015 mtu atakaye tumia falsafa za Mwalimu kuombea kura ndiye atakayekuwa Rais wetu.
   
 2. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #2
  Mar 22, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Unategemea kweli kampeni za akina Vicent Nyerere , Lema , Sugu ziwe za kistaarabu kweli?
   
 3. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #3
  Mar 22, 2012
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Immature brain synthesis
  [​IMG]
   
 4. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #4
  Mar 22, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Mkuu nakuunga mkono hapo kwenye namba 2 ila sijakuelewa kwenye namba 1 na 3, singuka zaidi kwa ufafanuzi.
   
 5. M

  Mpanzi JF-Expert Member

  #5
  Mar 22, 2012
  Joined: Jan 11, 2011
  Messages: 767
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  Kama Wasira na yule mzee anyeongoza vijana Shigela ni wastaarabu naomba maana ya siasa za kistaarabu
   
 6. Dijovisonjn

  Dijovisonjn JF-Expert Member

  #6
  Mar 22, 2012
  Joined: Nov 14, 2011
  Messages: 450
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Kwa 99% umenena kweli mkuu.
   
 7. OLESAIDIMU

  OLESAIDIMU JF-Expert Member

  #7
  Mar 22, 2012
  Joined: Dec 2, 2011
  Messages: 19,193
  Likes Received: 182
  Trophy Points: 160
  Recommendations???....................
  Hapo kwenye red mkuu ndo vipi hapo?????
   
 8. p

  politiki JF-Expert Member

  #8
  Mar 22, 2012
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 2,356
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  mbona umemsahau Baba wa UONGO Benjamin Mkapa
   
 9. p

  politiki JF-Expert Member

  #9
  Mar 22, 2012
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 2,356
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  "Wapinzani wa CCM wanalalamika CCM inatumia rushwa kwenye kampeni lakini hawaziamini taasisi za kupambana na Rushwa na matokeo yake hawaripoti tuhuma hizo kwenye taasisi hizo zaidi ya kuzisema kwenye majukwaa ya Kampeni".
  mjomba unataka waripoti nini kwenye taasisi ya rushwa wakati unajua wazi ni kupoteza muda ukitaka kujua sababu uliza ktk uchaguzi wa mwaka 2010 viongozi wangapi wa CCM walikamatwa live wakigawa rushwa mfano mzuri BETTY MACHANGU na MARGARETH SITTA je uliza kati yao wangapi licha kufungwa walifikishwa hata mahakamani ? zero unataka ushahidi gani tena.
   
 10. Kigarama

  Kigarama JF-Expert Member

  #10
  Mar 22, 2012
  Joined: Apr 23, 2007
  Messages: 2,479
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Watanzania wengi wanatenda kibepari lakini wanafikiri kwa kijamaa. leo hii watanzania bado wanafikiri wanaweza kuishi kwenye ardhi isiyopimwa na ikaendelea kuwa yao. Kuna kundi kubwa na wasomi wakiwemo ambao wanafikiri ajira ni lazima itoke serikalini. Watu wetu bado wanataka afya zao zitunzwe bure na serikali kwa gharama za kodi zao.

  Kwa mantiki hiyo ni mtu atakayewaambia watanzania kwamba yeye akichaguliwa kuwa Rais basi ataishi kijamaa ndiye atakayepata kura nyingi mwaka 2015. Moja ya kauli zilizompa sana Slaa umaarufu mwaka 2010 ni ile aliyosema kwamba yeye akichaguliwa akiingia Ikulu basi atakula Mihogo na kuhakikisha nyumba zote za serikali zilizouzwa zinarejeshwa kwa wenyewe!!

  Watanzania wanapenda kuishi kijamaa ingawa matendo yao ni ya kibepari!!
   
Loading...