Nilichojifunza Leo Kanisani

Nilichojifunza Leo Kanisani

Hiyo ndo teaching aid yake na amefanikiwa sana kufikisha ujumbe.
Dah....Dadeki...akitoa mafundisho kama hayo mara 3 kwa wiki...ameharibu noti zenye thamani ya zaidi ya 1.5m kwa mwaka....ambayo ni zaidi ya 15m kwa kipindi cha JPM tu
 
MASOMO MATATU

SOMO LA KWANZA.

Nilikuwa kanisani nikimsikiliza muhubiri mmoja maarufu, muhibiri alitoa mfukoni noti za shilingi elfu kumi kumi zilizokuwa na jumla ya Tsh laki moja, akauliza, "ni nani miongoni mwenu anataka nimpe hii laki moja?"

Watu wengi waliokuwa mle kanisani walinyosha mikono, kila mmoja alikuwa akishauti mimi! Mimi!. Nikaanza kushangaa ni nani atakuwa na bahati ya kupewa ile pesa kati ya mamia ya watu waliohudhuria ile ibada.

Pia nikajiuliza kwa nini (ambapo bila shaka na baadhi ya wahudhuriaji wengine nao walijiuliza) atoe kitita cha shilingi laki moja kirahisi rahisi hivyo.

Wakati watu wakiendelea kupiga kelele kusema nipe mimi, nipe mimi huku wamenyosha vidole vyao, kutokea nyuma akaibuka msichana mdogo mwenye umri kama miaka 18 hivi, akaenda mbele kule aliko yule muhubiri akafika mbele na kuchukua ile laki moja kutoka mkononi mwa yule muhubiri.

"Safi sana, msichana! Umefanya vema," alisema yule muhubiri.
"Wengi wetu tunapenda kukaa tu na kusubiri mambo mazuri yaje yenyewe. Hii haitaweza kuwasaidia hata kidogo, unatakiwa kuinuka na kutafuta mafanikio. Mafanikio hayawezi kuja kama umekaa tu.

Na maisha yetu ndivyo yalivyo, tunaziona fursa nyingi sana zikiwa zimetuzunguka, kila mtu anahitaji mambo mazuri. Ila tatizo hatutaki kusimama na kuzifuata hzo fursa. Simama sasa na ufanye kitu, usisubiri mafanikio huku umekaa, kamwe hayatakuja. Usijali kuhusu watu watasema nini. Chukua hatua.

SOMO LA PILI.

Baadae yule muhubiri akatoa tena noti ya shilingi 10000 na akainyanyua ili wote tuione. Nikafikiri anarudia kama mwanzo tena. Lakini akauliza swali jepesi. "Noti hii inathamani gani?" Waumini wakajibu "shilingi elfu kumi". "Mko sahihi" akawajibu.

Akaichukua ile noti akaifinyanga finyanga na kuwauliza tena noti ile inathamani ya shilingi ngapi!? "shilingi elfu kumi" wakajibu wale wauminii!

Akaitupa chini ipe noti, akaikanyaga kanyaga sana, akaichukua na kuuluza tena noti hii ina thamani ya kiasi gani? "Shilingi elfu kumi" waumini walijibu vilevile.

Muhubiri akawaambia nataka muweka katika akili yenu hili, "mtu hata aichakaze, aikunje kunje na kuikanyaga noti ya fedha, thamani ya noti itabaki pale pale."

"Maisha yetu ndivyo yalivyo, tunatakiwa tuwe kama noti ya shilingi elfu kumi. Ktk maisha kuna kipindi tutasalitiwa, tutakanyagwa, tutaonewa na kupigwa. Ila usiache thamani yako ipotee, kwa sababu mtu amekuumiza tu, hiyo haimaanishi ndio thamani yako imepotea. Wewe ni wa thamani mno jinsi ulivyo. Usiache thamani yako ipotee kwa sababu ya wapumbavu wachache!

SOMO LA MWISHO.

Njia tofauti, jibu moja.
2+5=7
6+1=7
3+4=7
7-0=7
7+0=7
9-2=7
8-1=7

Pointi yangu iko wapi?

Pointi yangu ni kwamba kuna njia nyingi za kufikia mafanikio yako. Mungu hawezi kukufikisha katika mafanikio yako labda kama mama yako, baba yako, marafiki au ndugu walivyofanikiwa, kila mmoja hua na njia ya mafanikio tofauti Mungu aliyompangia.

Unaweza fikia mafanikio yako aitha kwa kuongeza watu katika maisha yako au kupunguza watu. "kujumlisha na kutoa" marafiki na baadhi ya vitu katika maisha yako kunaweza kusiwe kwa furaha kwa upande wako, ila Mungu ana makusudi yake.

Katika safari yako unaweza ukakumbana na kusalitiwa, kuumizwa kihisia, kuchekwa na kusimangwa! Acha kulia na futa machozi yako kila hali unayopitia ina makusudi yake. Mungu anakutengeneza uwe bora zaidi ya hivyo ulivyo.

Jibu langu ni jepesi tu

TUTAKUA KAMA VILE MUNGU ALIVYOTUPANGIA TUWE!

Na Watakia Jumapili Njema Na

Mwenyezi Mungu awabariki

Mwaaaaaaahhhhh Nawapenda Nyote

Mahubiri murua. Hizi philosophia ndio zinatakiwa kipindi hiki kigumu
 
tunaweza kupata hayo masomo yalikuwa yanatoka kwenye vitabu gani ndani ya bible..?

nimebarikiwa....

kwetu Parukiani na wakatoliki wote dunian, ilikuwa sikukuu ya Bwana wetu Yesu Kristo, na adhimisho la mwaka wa mwisho wa kikanisa (mwisho wa mwaka wa kikanisa wa mwaka C ) nakukaribisha mwaka mwingine wa majirio wa mwaka A...
 
mafundisho ya kitapeli nawe ulivyo mjinga unadhani kuna jambo jipya hapo,

hizo kanuni za maisha hata huku kitaa tunazijua siyo mpaka nyumba za ibaada alafu nikusaidie ufahamu kidogo kwenye nyumba za ibaada tunakweda kufundishwa mambo yatakayotupeleka ulimwengu ujao sio huu, fedha na mali ni vitu vya ulimwengu huu

vyote hivi tumepewa tangu kuumbwa kwa ulimwengu ni akili tu, hata wasio na imani wanayo fursa sawa na wenye imani, tofauti jinsi ya kutafuta kwa haki,

achana na hao wahubiri matapeli la sivyo utaukosa ulimwengu ujao
Hisia zangu nikuwa hujaelewa kuanzia title ya huu uzi mpka contents, soma tena mpka uelewe...!ukishindwa kabisa nifuate inbox nikueleweshe....
hofu yangu usije kujikuta uko peke yako mchangiaji ambaye hajaelewa...

nashukuru
 
Dah....Dadeki...akitoa mafundisho kama hayo mara 3 kwa wiki...ameharibu noti zenye thamani ya zaidi ya 1.5m kwa mwaka....ambayo ni zaidi ya 15m kwa kipindi cha JPM tu
Hakuchana ilaaliikunja kunja. Genuine noti hata ukiikunja inajikunjua ukiona haijikunjui ujue ni fake au ni zile wanachapisha viwanda vya kichina.
 
Kuna rafiki yangu anamaliza mwaka tangu apate uhamisho wa kikazi serikalini,kaipa hi sana hii post. Hajalipwa chochote hadi leo,amekopa hadi chumvi . Leo kapata faraja alipopata hii msg ya mtumishi wa Mungu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom