Abraham Lincolnn
JF-Expert Member
- Apr 12, 2018
- 3,168
- 6,089
Dominika hii Kanisa linaadhimisha sherehe ya Pentekoste. Hili ni adhimisho la ujio wa Roho Mtakatifu kwa Kanisa zima siku 50 baada ya Yesu kufufuka.ujio unaoashiria mwanzo wa Kanisa kama jumuiya inayoongozwa na Roho Mtakatifu kukiri,kuishi na kuadhimisha fumbo la Kristo.
INJILI
Yn. 20 :19-23
Ikawa jioni, siku ile ya kwanza ya juma, pale walipokuwapo wanafunzi, milango imefungwa kwa hofu ya Wayahudi; akaja Yesu, akasimama katikati, akawaambia, Amani iwe kwenu. Naye akiisha kusema hayo, akawaonyesha mikono yake na ubavu wake. Basi wale wanafunzi wakafurahi walipomwona Bwana.
Basi Yesu akawaambia tena, Amani iwe kwenu; kama Baba alivyonituma mimi, mimi nami nawapeleka ninyi. Naye akiisha kusema hayo, akawavuvia, akawaambia, Pokeeni Roho Mtakatifu. Wo wote mtakaowaondolea dhambi, wameondolewa; na wo wote mtakaowafungia dhambi, wamefungiwa.
Neno la Bwana... Sifa kwako Ee Kristo.
Mbali na tafakari zingine pia nimejaribu kujiuliza wale wanaohoji mamlaka ya mapadre na maaskofu kuondoa dhambi za waumini ina maana hawasomi wala kufuatilia maandiko? Yesu mwenye alisema
"Wo wote mtakaowaondolea dhambi, wameondolewa; na wo wote mtakaowafungia dhambi, wamefungiwa"
Kwa hiyo unapotubu,kujutia,kulipiza na hatimaye kushiriki Sakramenti ya Kitubio/Maungamo mbele ya Padre yeye amepewa mamlaka ya kukuondolea dhambi zako(kufungua) au kukataa kukuondolea dhambi zako (kufunga) kama jinsi Yesu alivyowaagiza.Hivyo kanisa linapomfungia huduma muumini ni wazi kwamba hata mbinguni amefungiwa na linapofungua hata mbinguni amefunguliwa.
Tumsifu Yesu Kristu
View attachment 2251162