Nilicheza karate mpaka alinitokea babu wa kichina akawa ananinoa usingizini

Kiboko ya Jiwe

JF-Expert Member
Apr 7, 2020
12,967
37,000
Kwa wasiojua ni kwamba karate ni imani(dini) kamili, ina madhabahu zake kama zilivyo dini zingine.
Nilianza karate nikiwa darasa la pili kijijini kwetu huko Lindi. Nilikuwa mkubwa kidogo maana nilichelewa kuanza shule. Kipindi naanza karate nilikuwa na miaka 14, darasa la kwanza nilianza nikiwa na 13 yrs kutokana na mazingira ya shule kuwa mbali.

Binafsi sikuupenda huu mchezo ila niliposikia jirani yangu ambaye tulikuwa tukitandikana sana anacheza nami nikasema nakwenda kucheza . Mchezo tuliucheza free, uwanjani nyumbani kwetu. Yule braza alikuwa anatufundisha weekend anaporudi kijijini akitokea mjini alikokuwa anasoma sekondari.
Sijajua kwanini tulisimama ila ninachojua hatukucheza muda mwingi sana.

Miaka 3 mbele akaja jamaa mmoja sijui ni mpelelezi au jambazi Mimi sijui. Ila kwa ujuzi aliokuwa nao yule mtu kuhusu judo hakustahili kuja kuishi kule kijijini.
Jamaa moto sana, kijiji kizima kikawa kinanuka karate. Huyu jamaa alifikia kijiji jirani ambacho nilikuwa nasoma primary kabla kijiji chetu hakina primary ila kipindi hicho jamaa anafanya maajabu nilikuwa nishahama ile shule na kuhamia primary ya kijijini kwetu. Kuna vijana kama 4 kutoka pale kijijini kwetu walikwenda kuchota ujuzi kwa malipo ya elfu 8 tu.

Walipoiva na kupewa mikanda yao ya walimu wasaidizi wakaja kufungua center pale kijijini kwetu.
Niliingia pia kwa kuwa mhasimu wangu alijiunga. Nikacheza kwa miezi sita nikawa nondo. Mchezo haukuendelea kwakuwa tulishindwa kulipa ada ya elfu 5 kwa mwezi.
Nikamaliza la saba nikapangiwa shule moja ya vipaji vya kati ambayo ilichukuwa wanafunzi kutoka Tanzania nzima.

Nikiwa form 3 nikafungua center ya karate shamba la shule ila sikubahatika kulipwa hata mia, maana wanafunzi karibu wote niliokuwa nawateach walikuwa marafiki zangu na hawana pesa. Nikawanoa kidogo judo likafa kwa sababu za kimazingira.

Nikiwa form four alikuja mwalimu mmoja Mmarekani anaitwa Bryan. Jamaa Taikondo utadhani kaianzisha yeye. Akatufundisha pale shule karibu nusu ya wanafunzi tulijiunga na karate.

Ila mimi aliponiona niko mbali akawa ananifundishia uwani kwake peke yangu. Maana wale wengine ndio kwanza walikuwa wanafundishwa mapigo, kata na mazoezi ya viungo.
Bahati mbaya teacher akarudi US.ghafla kumuuguza mchumba wake aliyekuwa anaumwa cancer.
Hapo ndipo nilipokuwa natokewa na kibabu usingizini akiniteach Judo kwa lugha nisiyoijua, nahisi yule babu ni Mchina, Mkorea au Mjapani.
Hapo nikajua style nyingi.

Baadaye nikaichukia karate maana nilikuwa sioni faida yake zaidi ya kukuharibu akili. Unatamani uvamiwe na vibaka ili uwatwange, muda mwingine unajisahau unakunja ngumi au kuongea mwenyewe. Nikaizika karate rasmi na kuokoka.
Nilijikumbushia karate nikiwa Ruvu JKT , niliwateach ma Private leaders wawili wa platoon yetu ili nipate favor fulani. Siku ninawaaga waliumia sana, maana nilikwenda kwa mujibu wa sheria 2013.
 
Safi sana mkuu.. mimi najiona mzembe mzembe sana kwenye seof defence.

Unafanya mishe gani sahiv? Kwanini usiweke darasa upate pesa

Ukizingatia tunaelekea uchaguzi mkuu na itatubidi kulinda kura zetu
Ahahahaaa.
Mimi ni mwajiriwa serikali sasa.
Nikifundisha karate naweza kutumbukia kwenye matatizo makubwa.
 
Kitambo sana hii kitu hadi nahisi nishasahau. Mtaani kwetu ilikua ndio mtindo vijana kujifujza Shotokan Karate
nilikua na 12/13 sijui..

Tuseme ukweli Karate haina faida.
Karate ipigwe marufuku na serikali.
Kuna jamaa mmoja kaiva mpaka kaungulia, akiitazama taa inayowaka inaungua. Yuko Mwenge muda wote kakunja ngumi.
Jamaa Korea kachukua ufundi judo
 
Haina faida kabisa unabaki na ujuzi wako..Mimi niliacha maana ilikua inachujua muda wa shule sana. Bamdogo zangu wamecheza sana bado kidogo wafike red ila haijawasaidia kitu. Dingi amecheza mpaka sasa anacheza kama moja ya mazoezi hakuna faida. Sana unaweza kua mkorofi tu kisa unajiamini
Huu mchezo unalipa ila Tanzania michezo inayolipa ni michache sana. This is due to poverty
 
Haina faida kabisa unabaki na ujuzi wako..Mimi niliacha maana ilikua inachujua muda wa shule sana. Bamdogo zangu wamecheza sana bado kidogo wafike red ila haijawasaidia kitu. Dingi amecheza mpaka sasa anacheza kama moja ya mazoezi hakuna faida. Sana unaweza kua mkorofi tu kisa unajiamini
Kutokana na Utulivu uliopo nchini kwetu inaonekana haina faida, ila kwa nchi zenye vurugu ni faida
 
Kitambo sana hii kitu hadi nahisi nishasahau. Mtaani kwetu ilikua ndio mtindo vijana kujifujza Shotokan Karate
nilikua na 12/13 sijui..

Tuseme ukweli Karate haina faida.
Usiseme haina faida labda kwako!.. ngoja siku ukabwe roba ndo utajua inafaida au haina.. ule Ni ujuzi tu wa kuweza kujilinda we mwenyewe naona mliopewa huo ujuzi mlikosewa wakati mi nautamani kinyama atakae nizingua ile haswa haswa lazima arudi alikotoka.. hatuwezi kusema jeshi au silaha hazina faida kwasababu hakuna vita ndugu!.
 
Back
Top Bottom