Stabilaiza
JF-Expert Member
- Jul 11, 2012
- 1,843
- 1,143
- Thread starter
-
- #21
Nilishasema kwa watu wa namna hiyo ni kuwa- ignore. Siwatofautishi na watu kama Nape na Makonda. Aina ya watu hawa wapuuzi nikiwaona kwenye TV nahamisha Channel au nazima TV.Nakuunga mkono mleta uzi...hao wanaotoa comments za kukupinga bila shaka wana lao jambo. Binadamu hatukosi mapungufu na hata Nyerere alikuwa nayo. Lakini Warioba kwa upande wangu namuona kama image ya Mwl. Nyerere!
Katiba ya wanachi, kama ilivyoandaliwa na Warioba inaziba mianya watawala wezi na mafisadi. Wao wameikataa, wakiongozwa na mwenyekiti wao wa taifa wa chama chao cha mafisadi.Hawa wote Presida,Six,Chenge,Werema,Lukuvi na Wabunge waliopewa mshiko walikuwa wanajua wanachokifanya.Sijui kama Cheyo leo yupo mzima,atakuwa ndani yake anajutia usaliti wa nchi yake kama hakupokea yawezekana na yeye alipewa MZIGO.
Ninachotaka kusema ni kuwa Prezida amekosea,tunamuomba asiendelee kukosea kwa kuipigia CHAPUO Katiba ya MAFISADI,hilo tu.
Ndiyo maana nikimtafakari simmalizi kwa uzalendo wake.ni mzalendo aliyetaka miaka ijayo tuendelee kunufailka na keki ya taifa
Katiba ya wanachi, kama ilivyoandaliwa na Warioba inaziba mianya watawala wezi na mafisadi. Wao wameikataa, wakiongozwa na mwenyekiti wao wa taifa wa chama chao cha mafisadi.
Katika ukurasa huu nitakuwa nikileta tafakuri mbalimbali kumhusu Mhe. Sana Jaji Warioba na Waziri Mkuu Mstaafu. Kiini cha kuleta tafakuri juu yake ni nafasi yake kama alama pekee katika nchi yetu kwa sasa ya kiongozi aliyetukuka ambaye bado tunaishi naye.
Yeye ndiye anabaki kuwa alama ya uzalendo kwa nchi yetu, heshima ya nchi yetu, utu, uhuru, uongozi bora na mambo mengine yaliyolifanya taifa letu kupata heshima kubwa ulimwenguni enzi za utawala wa awamu ya kwanza ya baba wa taifa marehemu Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Kama alama, Warioba anatofautiana na wengine wengine (wanaoishi kwa sasa) waliofuatia katika awamu zingine na wanaolitawala taifa letu kwa sasa. Watawala hao wengine wamelifanya taifa letu kuwa la aibu, lisiloheshimika na ambalo linakumbatia udhalimu wa aina mbalimbali.
Nikimtafakari Warioba simumalizi. Anauzalendo wa hali ya juu,utu, msimamia kweli ya wananchi, mkarimu kiasi kwamba anafanya kazi kama mtumishi wa wananchi. Ukianzia katika utumishi wake kama mwenyekiti wa tume ya rais ya katiba mpya unaona utu wake. Warioba amewaongoza wenzake kuachana na ubinafisi na kuwatumikia wananchi wa Tanzania katika kuwaletea rasimu ya katiba (aka Rasimu ya Jaji Warioba) ambayo imesheheni maslahi ya wananchi.
Warioba ameendelea kuwa mtulivu katika kuhakikisha kuwa ndoto ya wananchi kupata katiba yao wanayoitaka inafikiwa. Kwake Warioba, kinachoitwa kudhalilishwa katika kufafanua katiba ya wananchi wanayoitaka ni ushindi, utumishi na alama ya kuwawakilisha vemawananchi. Amejishusha kutoka kuwa kiongozi hadi kuwa mtumishi mvumilivu kwa wananchi, akihamasishwa na ndoto yao wananchi ya kupata katiba wanayoitaka.
Katika tafakuri inayofuata, nitaeleza ninavyomuelewa Warioba, namana alivyoenenda akiwa mwenyekiti wa tume ya katiba na katika kongamano la katiba lililovamiwa na kuvunjwa na mazalio ya utawala uliolifanya taifa letu kuwa kichekesho na aibu kubwa ulimwenguni.
Hapa sizungumuzii ukaribu wa kifamilia wala ki-jiografia. Nazungumzia ukaribu katika uongozi wa nchi. Haujui kuwa Warioba alipata kuwa Waziri mkuu enzi za utawala wa Mwalimu? Nimesema wazi kuhusu CV ya Warioba kama alama ya mtu aliyetukuka ambaye bado tunaishi nae, aliyekuwa kiongozi katika utawala wakati wa Baba wa taifa. Wasira ni mwana mtandao wa CCM maslahi. Ndiyo maana anapigia chapuo katiba pendekezwa ya CCM ambayo imetupilia mbali mahitaji mapya ya wananchi katika katiba mpya. Wasira hataki uwajibikaji, anataka viongozi wafiche pesa nje, hawezi kamwe kutajwa kulinganishwa na Warioba, achilia mbali kufikiriwa kama kiongozi mwenye maadili.Eleza cv yake kwanza yeye hatoki butiama kwao ni nyamuswa ukaribu wake na mwalimu nyerere uko wapi ? Je wasira hakuwa karbu na nyerere?
Hapa sizungumuzii ukaribu wa kifamilia wala ki-jiografia. Nazungumzia ukaribu katika uongozi wa nchi. Haujui kuwa Warioba alipata kuwa Waziri mkuu enzi za utawala wa Mwalimu? Nimesema wazi kuhusu CV ya Warioba kama alama ya mtu aliyetukuka ambaye bado tunaishi nae, aliyekuwa kiongozi katika utawala wakati wa Baba wa taifa. Wasira ni mwana mtandao wa CCM maslahi. Ndiyo maana anapigia chapuo katiba pendekezwa ya CCM ambayo imetupilia mbali mahitaji mapya ya wananchi katika katiba mpya. Wasira hataki uwajibikaji, anataka viongozi wafiche pesa nje, hawezi kamwe kutajwa kulinganishwa na Warioba, achilia mbali kufikiriwa kama kiongozi mwenye maadili.