Nikimkumbuka Ndugai roho yangu huuma sana

Nikimkumbuka Ndugai roho yangu huuma sana

El Roi

JF-Expert Member
Joined
May 29, 2020
Posts
297
Reaction score
537
Katika ulimwengu wa elimu ya uongozi, ukiachana na sifa nyinginezo, moja ya sifa ambayo kiongozi hapaswa kuikosa ni Imani au sema falsafa yake .

Falsafa hapa kirahisi inamaanisha vile ambavyo unayaona nambo na namna yanavyotakiwa kuwa.

Leo nimemkumbuka spika aliyeachia madaraka ya uspika ( simuiti msitaafu) Kwa Sababu hakusitaafu bali alishinikizwa kujiuzuru) Job Ndugai.

1) Nimejiuliza, hivi wakati mbunge wa Ndanda Cecil Mwambe, anahama Chadema wakati huo na kujiunga na ccm na hata bila aibu Spika Ndugai akahararisha ubunge wake na huyo bwana kuendelea kuwa mbunge ambaye hakuwa na Chama ( kumbuka hakuwa awali ameshinda kwa ticket ya CCM bali Chadema) Falsafa ya kiongozi kama spika ya kuyaona mambo katika haki kama alivyokuja baadae kupigia kelele mikopo ya serikali ilikuwa wapi ?

Huyu spika alikuwa under which influence kutotambua jambo rahisi kama Hilo la kumbakiza bungeni, mbunge aliyehama chama chake huku ikiwa wazi kabisa kwamba bila kuwa na chama huwezi kuwa bungeni ?

2) Nilisikitishwa sana pia na matendo ya Ndugai, kumfuta na kumvua ubunge Tundu Lissu.

Hata ujiachana na sababu nyingine zozote kama zilikuwepo, unawezaje kukubali kusimamia maamuzi ya kumvua ubunge mtu ambaye alikuwa anapigania matibabu kuokoa maisha yake baada ya tukio baya alilopata la kuvunjwavunjwa na risasi za moto. Ilikuwa wapi falsafa ya Ndugai walau ya kujua haki inayomhusu mtu na ubinadamu?

Hivi kweli maisha yako binafsi hayakufundishi tu kutendea haki mtu..? Hata kama unashinikizwa Kwa huwezi kukataa kufanya jambo lisilo sawa? Labda niwajulishe thamani kuu ya mtu " Ni pale unapokuwa tayari kufia kile unachoona ni sahihi kwa maana ya usahihi" ( The highest good of any individual is when you are ready to die for what you believe to be true).

Watu wanaoishi falsafa zao huwa tayari hata kupoteza maisha, nafasi nk ili wabaki wakiwa na dhamiri zao.

Ndo maana nchi nyingine , siyo shida kusikia waziri mkuu anaachia madaraka baada ya wiki mbili maana anagundua kwamba hawezi kuishi falsafa au maisha yake anayoyaamini wakati anaona mambo hayako sawa.

Kupitia Ndugai yawe maombi yangu kwamba watu wajifunze kuishi maisha ( falsafa zao). Nakubali kwamba maisha ili yaende Kuna wakati lazima ukubali kupoteza na kupata au win win life, lakini hii haiendi kwa mambo ya msingi ya imani Yako ya kimaisha . Kuna mambo ambayo kama kweli unajitambua huwezi kuyakubali.

Kama Ndugai ange mtoa bungeni Cecil Mwambe wakati huo, akakataa kukubali Tundu Lissu kufutwa ubunge na kunyimwa haki yake, na mengine mabaya kama vile wabunge wanawake Chadema alivyowapokea kinyamela na kuwaapisha, Leo hata bila madaraka angekuwa shujaa, lakini sasa hatakumbukwa kwa sababu kama huishi maisha yako, asili na Mungu pia huondoa kibali kwako.

Ndo maana hata alipojaribu kurudi kwenye falsafa yake kwa maana ya kujaribu kuishi maisha yake kwa kupinga mikopo ya nchi mara moja alionekana msaliti maana hakuwahi kuishi falsafa yake hapo nyuma. Na kwa sababu hiyo viongozi na hata watu wengineo tuishi Yale tunayaamini sahihi suala la kukubalika ( Approval) na watu au kikundi chochote huja baadae. Hofu ya kuogopa kukataliwa na watu au kutaka sifa za watu hata pale dhamiri yako inapokuonyesha vinginevyo ni kutoishi maisha yako ( Falsafa) na Mwisho wa siku Huwa fedheha .

Nampenda Ndugai maana anaonekana bright na kwa viwango vyake hata vya shule lakini Kuna wakati nauona hakuishi falsafa yake.
 
Hoja makini sana
Kila mtu huwa analo la kukumbukwa

Naweka kambi hapa kuelimika zaidi kuhusu Ndugai
 
Hoja makini sana
Kila mtu huwa analo la kukumbukwa

Naweka kambi hapa kuelimika zaidi kuhusu Ndugai
Wana CCM wote huzichopoa akili zao wanapotaka kupambana na CHADEMA. Leo watu wanajisahaulisha kauli ya Samia Suluhu pale Nzega akiwa mgombea Mwenza wa Magufuli alipozungumzia kuhusu kushambaliwa kwa Lissu.
 
Roho isikuume.. sasa hv niwakawaida kabisaaaa....
 
Mungu wetu aliye hai alipokasirishwa na vitendo vya Magufuli na Ndugai baada ya kulewa madaraka aliwapiga fimbo yenye maumivu makali na kuvunja hila walizokuwa nazo za kujifanya masultani wa mile wa Tannzania
 
Wewe nae pumbavu sana,tunateswa na ukosefu wa maji,umeme,mfumuko wa bei ya bidhaa zote nchini halafu unatuletea hadithi za Ndugai?,
emoji706.png
emoji706.png
emoji706.png
emoji706.png
kabisa wewe,au mmetumwa kutuondoa kwenye issue ya katiba??????
 
Kuna siku alimtoa yosepher komba kibabe bila hata kusikilizwa
 
Wewe nae pumbavu sana,tunateswa na ukosefu wa maji,umeme,mfumuko wa bei ya bidhaa zote nchini halafu unatuletea hadithi za Ndugai?,[emoji706][emoji706][emoji706][emoji706]kabisa wewe,au mmetumwa kutuondoa kwenye issue ya katiba??????
Wazagamba, ha ha ha ha
Umenifurahisha japo kwa matusi.

Kwa taarifa Yako, unacholalamikia wewe, maji, umeme nk hayo ni matawi tu.

Mie nimekuonyesha chanzo Cha hayo matatizo. Ni viongozi kutojielewa na badala yake wanaishi maisha yasio Yao
( Falsafa sahihi) . Wanakula pesa ya miradi ya maji, wanahujumu wengine miundo mbinu ya umeme, hawajali haki za watu wadogo nk.

Nadhani kama ungekuwa na kufikiri kidogo tu ungeona umuhimu wa hoja yangu.

Anyway hata hivyo jina lako ni Nzagamba nashiwishika kuamini kwamba dini yako ni ya asili.

Ungeelewa dini nyingine, zingekwambia * haki huinua taifa". Kufanya vinginevyo kunaondoa baraka Fulani katika nchi.

Mola Nzagamba!
 
KARMA, malipo NI hapa hapa Duniani. Bosi wake alishaoza Chattle.

TUISHI KWA UPENDO
Hata kama hakuna ninachoshabikia hapa, ukweli umeusema. What goes around comes around.
 
Wana CCM wote huzichopoa akili zao wanapotaka kupambana na CHADEMA. Leo watu wanajisahaulisha kauli ya Samia Suluhu pale Nzega akiwa mgombea Mwenza wa Magufuli alipozungumzia kuhusu kushambaliwa kwa Lissu.
tukumbushe hiyo kauli mkuu
 
Back
Top Bottom