Nikimfumania mume wangu siwezi kumuacha kamwe

Miss Natafuta

JF-Expert Member
Sep 16, 2015
26,568
48,701
Sijaolewa wala sijui kama nitaolewa maana sina hata boyfriend!

Huwa nashangaa sana wanawake wenzangu walioko kwenye ndoa wakiwa na mizozo na wanaume zao eti wanajishughulisha na wanawake wengine sionagi tatizo ni nini.

Sijawai kutembea na mume wa mtu tena sipendi kabisa,lakini ikitokea niwe na mume nikimfuma na mwanamke mwenzangu kweli siwezi kuleta shida ataamua tu mwenyewe kuachana nae au vipi mimi hayanihusu si kaamua mwenyewe?

sasa unamsumbua ili iweje?
 
Una uhakika na unachokisema aisee? Kwa taarifa yako, kwa kuzingatia marital na relationship status yako hiyo (kama ni kweli lakini)...then ni mapema sana kwako kusema hivyo unavyosema.

Bado hujavuka mabonde na milima ya kimahusiano bibie. Jipe muda kidogo best
 
Wanaume ni wengi saana ila wanaofaa kukuowa ni wachache! kumuacha ulienae yawezekana ikawa ni gharama sana kuliko kumsamehe na kuendelea na maisha yenu

sijaolewa wala sijui kama nitaolewa maana sina hata boyfriend!
huwa nashangaa sana wanawake wenzangu walioko kwenye ndoa wakiwa na mizozo na wanaume zao eti wanajishughulisha na wanawake wengine. sionagi tatizo ni nini.
sijawai kutembea na mume wa mtu tena sipendi kabisa.lakini ikitokea niwe na mume nikimfuma na mwanamke mwenzangu kweli siwezi kuleta shida ataamua tu mwenyewe kuchana nae au vipi mimi hayanihusu.si kaamua mwenyewe? sasa unamsumbua ili iweje?
 
Usimuache mwaya.......tena Kama kaishiwa CD unamuongezea ili amalizie.......
Hakuna kitu kibaya kama kukatishwa mechi kwa vurugu.......
kweli sister na huwezi mkatisha mtu mechi kwa lazima atii! hadi aamue mwenyewe kuacha sasa kwanini ujitese na mtu?
 
Back
Top Bottom