Nilipokuwa shule ya msingi kuanzia la 4 hadi la 7 maksi zangu za hesabu kwenye mitihani zilikuwa zinacheza kwenye 03%hadi 08%.Matokeo yalikuwa yanatangazwa mbele ya darasa! yanapotangazwa mwalimu anaanza kuwaita wanafunzi kwa kuanzia maksi za chini kwenda juu (0-100), kwa hiyo darasa lote linajua makaratasi yakiletwa lazima niitwe kama si wa kwanza basi wa pili.Siku moja mwalimu akaanza kuita majina,mpaka akafikia kwenye maksi 30%,40%,50%,60% ,70% bado tu mi hajaniita. Watu wakaanza kuniangalia waliokuwa karibu wakaanza kuniuliza...."" eeeh umepasua hujaitwa, ilikwaje??"Nili anza kuvimba kichwa, huku mwalimu anaendelea kugawa tu makaratasi. Yakabaki makaratasi ya waliopata 80%-90% bado mi sijaitwa tu. Mara akabaki na karatasi moja mkononi, darasa lote macho kwangu hawaamini kinachotokea maana bado sijapata karatasi. Mwishoni mwalimu akaangalia juu,kisha akasema"Kuna ng'ombe hajaandika jina kapata 0% aje achukue karatasi lake...