Kuna jambo la ajabu ambalo sijui ni Kwa nini inatokea hivi.
Kwamba ninapohitilafiana na mke wangu nikikasirika mara nyingi mvua inanyesha ni jambo ambalo limenitokea zaidi ya Mara tatu sijui nini maana yake wataalam msaada wenu Juu ya tukio hili.
ha ha haHiyo ni mvua gani?
Au ni kwamba unatoa sana mate unapoongea ukiwa umekasirika.?
hahahahahWewe una ngiri,.. Kwa hiyo mawingu yakifunga ngiri inauma unamkasirikia kila mtu. Na Kama wingu limefunga unategemea nini zaidi ya mvua? Pata ushauri wa daktari.
hahahahahahha..Hiyo ni mvua gani?
Au ni kwamba unatoa sana mate unapoongea ukiwa umekasirika.?
Hahahaa ngachokaWewe ni hazina kwa taifa,kwa uwepo wako bwawa la mtera haliwezi kukauka so tumeshapata suluhisho la kudumu la umeme,kilimo pia kitapiga hatua hata kama si kwa kasi lakini angalau sasa tutakuwa na uhakika wa mvua.Kitu kilichobaki sasa ni kuongea na mke wako na kuona jinsi gani anaweza kukukasirisha angalau kwa masaa 14 kwa siku.