Nikasome diploma ya Mechanical engineering au NIT au DIT?

Iko hivi inategemea na malengo yako yapoje unataka usome ili upate cheti tu au unataka usome ili kuelewa vema fani yako au unataka usome sehemu ili uwe na jina kutokana na chuo ulichosoma.
1.Tukianza na DIT ni chuo kilichobobea kwenye fani za engineering zifuatazo mechanical,electrical,civil,electronics,computer engineering,mining,lab technology.
2.Kuhusu NIT ni chuo kilichobobea kwenye mambo ya automobile engineering,logistics & transport,clearing & forwarding.
Kuhusu hiyo fani ya mechanical engineering pale haina miaka mingi sana tangu ianzishwe.
3.Ukichagua kusoma DIT inabidi ujipange sana uache mambo yako yote na upige msuli kwelikweli walimu wa pale hawataki masihara huwa wanakamia hawataki watu wafaulu kwa kubahatisha.
Lakini ukiweza kusoma DIT ukamalize kuna heshima kubwa iliyojengeka viwandani kwamba DIT ni chuo bora kwa hiyo cheti chake kina hadhi kubwa ukilinganisha na vyuo vingine vya engineering.
Ukichagua kusoma NIT au MUST kuna urahisi fulani wa kusoma yaani una asilimia kubwa za kusoma vizuri hadi mwisho kwa uhakika.
Walimu wake ni wapole na hawakamii kivile.
Mwisho wa siku ukimaliza kusoma jukumu linabaki kwako kupambana kutafuta kazi na kingine pia ukiwa serious kusoma kitu ukakipenda utakielewa tu haijalishi ulisoma wapi.
Kwa hiyo hapo nimekuchambulia kila kitu kwa hiyo uamuzi ni kwako.
 
Back
Top Bottom