Nikapigwa ndoa ya mkeka Ununio…! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nikapigwa ndoa ya mkeka Ununio…!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Mtambuzi, Jun 25, 2012.

 1. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #1
  Jun 25, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Nikakabidhiwa mwali niondoke naye.................
  (Picha haihusiani na habari hii)

  Hili ni tukio ambalo lilikimbiza jijini Dar mwaka 1987, ikiwa ni mwaka mmoja tangu nitie timu hapa mjini ili kujiunga na shule ya sekondari baada ya kumaliza elimu ya msingi huko kijijini.

  Nilikuja mjini na kufikia kwa kaka yangu maeneo ya Magomeni Makanya. Pale mtaani kulikuwa na mzee mmoja alikuwa na mziki wa kukodisha na jenereta, ilikuwa kila inapotokea kuna shughuli ya kumtoa mwali au harusi watu wakija kukodi ule mziki, mimi nilikuwa ni mmoja wa vijana ambao tulikuwa tunaenda na huo mziki kama mafundi mitambo.

  Kutokana na kiherehere changu, nilikuwa nimejichomeka na kuwa mmoja wa wadau wa kupigisha mziki mpaka nikajijengea jina kwa yule mzee. Ikitokea yule kijana aliyekabidhiwa hupo mziki na huyo mzee hayupo, nilikuwa napewa mie mikoba ya kwenda kupigisha mziki huko ulipokodishwa.

  Kama mnakumbuka kipindi hicho kulikuwa hakuna CDs, ilikuwa ni kanda za kaseti ambazo tunazirekodi miziki kulingana na uhitaji wa shughuli mbalimbali, hata haya mambo ya jingo na vijembe kulikuwa hakuna zaidi ya kutumia taarabu, au mchiriku kulinga na shughuli yenyewe.

  Ilitokea siku moja mziki ulikodishwa kwenye shughuli ya kumtoa mwali huko Ununio, na hivyo kama kawaida siku ya Ijumaa tukaondoka na pick up yetu hadi Ununio na kufunga mziki wetu, tukiwa na jenereta letu, kwani kipindi hicho Ununio kulikuwa hakuna umeme. Ununio ipo njia ya kwenda Bagamoyo.


  Tulikuwa na mazoea ya kujitwalia vibinti na kuvibanjua tutakavyo kila shughuli ya kumtoa mwali tunayokwenda na hiyo ndiyo iliyonifanya niipende sana kazi hiyo na kusahau shule ambayo ndiyo iliyonileta mjini. Nakumbuka kaka yangu alikuwa ananigombeza sana na kunionya niachane na mambo ya Kiswahili lakini haikuniingia akilini. Kijana rijali damu ilikuwa inachemka na umri wa ubaruaru ndio ulikuwa umeshika kasi, utaniambia nini.

  Ilikuwa kama naenda ngomani mpaka zile siku tatu za shughuli zikiisha naweza kujikuta nimebanjua vibinti visivyopungua vitatu mpaka vitano tena kavu kavu, bila kondom, kitu ambacho ninahisi huenda nimeacha utitiri wa watoto huko Uzaramoni. Nashukuru ukimwi ulikuwa haujashika kasi maana ningeshakufa zamaani na JF msingenijua. Tulikuwa tunagombewa kweli, maana tumetoka mjini na ile kuwa mpigisha mziki ilikuwa ni bonge la CV kujipatia vimwana na kujivinjari utakavyo bila hata kuhonga.

  Tulipofika Ununio tulipokewa vizuri na mwenyeji wetu mwenye shughuli ya kumtoa mwali alikuwa ana uwezo si haba kwani alikuwa na nyumba tatu, pale kijijini na wake zake watatu. Tukapangiwa kila mtu mahali pake pa kulala ambapo, mimi nililala kwenye nyumba ya mke mdogo ambapo ni mbali kidogo na nyumba ambayo ilikuwa inafanyika shughuli hiyo na wenzangu walilala kwenye nyumba ya mke mwingine mdogo wa mzee huyo kwa kuwa ilikuwa na vyumba vingi. Shughuli yenyewe ilifanyikwa kwa mke mkubwa.

  Siku ya kwanza ya shughuli sikwenda kulala kule nilikopangiwa kwani nilipata kabinti fulani na nilipata mwenyeji pale pale akanipa ghetto nikajipigia mpaka asubuhi huku wenzangu wakikesha ngomani. Asubuhi nilikwenda kujipumzisha kule nilipopangiwa kulala, na nilipofika nikakuta binti mmoja mzuri kweli. Baada ya kumdadisi aliniambia kwamba ni mdogo wake na mke wa yule mzee. Nilimpenda kweli na nikajisemea moyoni, lazima nimlambe. Alionekana amelelewa kwenye maadili kweli maana alikuwa na ile heshima ya kijijini na pia alikuwa na staha.

  Nilishinda pale nyumbani kutwa nikipiga naye stori na nilitumia muda huo kujifagilia kwamba ule mziki ni wa kwangu nililetewa na kaka yangu aliyekwenda masomoni Japan. Nilimdanganya kwamba ninamiliki nyumba mbili jijini Dra zikiwemo daladala 3 aina ya Isuzu Journey nilizotumiwa na kaka yangu kutoka Japan. Yule binti alionekana kuniamini kweli, na hiyo ikawa na nafasi kwangu kumtongoza na hakuonekana kuwa mgumu nikawa nimemnasa njiwa tunduni.

  Tulikubaliana tukienda ngomani aseme anajisikia vibaya ili arudi nyumbani, iwe ni nafasi nzuri kwangu kwenda kujivinjari naye pale pale kwao. Alionekana kufurahia wazo langu kwani awali alisema ingekuwa ngumu mtoto wa dada yake anachezwa ngoma halafu yeye asiwepo kukesha na dada yake.
  Usiku kama kawaida nilifika ngomani na kuanza kupigisha mziki na niliwadokeza wenzangu kuwa nitaondoka mapema na kwa sababu ilikuwa ni Jumapili siku ya mwisho ya shughuli ilikuwa ina shamra shamra nyingi na kulikuwa na dalili ya kukesha mpaka asubuhi.

  Nilimuona yule binti akipita na dada yake mke wa yule mzee mwenyeji wetu. Yule dada yake aliniangalia sana kisha akawa anatabasamu, sikuelewe ni kitu gani kinaendelea. Niliendelea kupigisha mziki na ilipofika mida ya saa sita usiku kakaja kabinti kamoja na kuniambia kwamba naitwa nimfuate. Nilikafuata hadi upenuni mwa ile nyumba ya shughuli, nilipofika pale nilimkuta yule binti na aliniambie tuondoke.

  Nilikwenda kuwaaga wenzangu na kuondoka na yule binti, tulipofika akanipeleka chumbani kwake ambapo aliniandalia chakula nikala kisha tukalala. Asubuhi nilishtuliwa na mlango ukigongwa kwa nguvu. Nilishtuka sana na nilimuona yule binti akiwa hana wasiwasi. Alijizoazoa pale kitandani na kwenda kufungua mlango na kutoka nje na kufunga mlango kwa nje. Nilisikia watu wakiongea huko nje na mmoja wa watu hao alikuwa ni yule mzee mwenyeji wetu.

  Baada ya muda yule binti alirudi akiwa amejitanda kanga kisha akaniambai nivae kuna wageni wanataka kuingia kunisalimia. Nilishtuka sana na nilivaa haraka haraka. Baaada ya kuvaa yule binti alifungua mlango na mara nikamuona mwenyeji wetu akiingia na wazee wanne na kina mama watatu na mkeka na chetezo cha ubani. Kwa akili yangu ya wanzuki mie sikajua labda wanataka tu kusoma dua kwa ajili ya ile shughuli hivyo nikanyanyuka ili nitoke. Nilizuiwa pale mlangoni na kuambiwa kuna kikao kidogo. Nilikaa na sikuwa na wasiwasi.

  Yule mzee alianza kuwambia wale wenzake aliofuatana nao……

  "Wazee wenzangu samahanini sana kwa kuwakurupusha kuja kukamilisha jambo hili la muunganiko wa watu wawili kati ya mtu mume na mtu mke, kama Kurani tukufu ilivyotuusia kwamba tusiikurubie zinaa, na hivyo basi huyu bwana hapa nimemfuma akizini na shemeji yangu na kwa mujibu wa dini yetu ya kiislamu mimi kama mlezi siwezi kuingia katika dhambi hivyo nimeona nihalalishe kabisa niwafungishe ndoa……"

  Muda wote wakati yule mzee anazungumza mimi nilikuwa kama ninaota na nilikuwa siamini kile kinachotaka kunitokea. Nilianza kuwaza, nitampeleka wapi mimi huyu binti wakati mie kula kulala na bado ninasoma.

  "Samani wazee mimi sijazini wala nini, nililetwa hapa na huyu mzee kwenye shughli ya kuwatoa mabinti zake na baada ya uchovu nilikuja kujipumzisha hapa kama nilivyoelekezwa na mke wa huyu mzee………." Nilijikakamua na kujitetea…

  Yule mzee alinikata kalma na kuwaambia wale mashehe kwamba ni kweli alinipangia nilale pale lakini chumba alichoniandalia ni cha nje na si cha ndani. Hicho chumba nilicholala ni cha shemeji yake ambaye ndiye niliyefumaniwa naye. Wale mashehe wakasema wasipotezewe muda na niliamriwa nikae kwenye mkeka nifungishwe ndoa niondoke na mke wangu.

  "Wazee wangu naomba mnisamehe kwani mie bado mwanafunzi na nikakaa kwa kaka yangu na sina hata uwezo wa kujitegemea….."
  Nilijitetea ili kujinusuru na ndoa ile ya fedheha.

  Yule dada yake na binti niliyefumaniwa naye akadakia……
  "Si wewe ulomwaambia mdogo wangu kwamba una nyumba mbili Dar na daladala tatu, sasa habari ya kusoma na kwamba huna uwezo wa kuishi na mke inatoka wapi? Tena ulimuahidi utamuoa, sasa tatizo liko wapi, wewe ondoka naye utatuletea mahari yetu hata mwakani." Kusikia hivyo, nikajua nkondo igwa. Jasho lilinitoka.

  Wakati wote wa kadhia hiyo nje kulijaa umati wa watu waliokesha kwenye ngoma na wale wenzangu niliokuja nao walikuwa hapo nje wananisubiri ili tuondoke.

  Nikiwa bado nimeduwaa, ubani ulichomwa na ndoa ikafungwa, lakini muda wote mwili wangu ulikuwa umekufa ganzi na sikuelewa kinachoendelea kabisa kwani chaneli zikikata.

  Baada ya dua nilisikia huko nje mdundiko ukipigwa na watu wakicheza kwa kwa furaha na nyimbo za vijembe zikitawala. Mwanaume lilinishuka shuu………

  Nilitolewa nje nikiwa nimefunikwa kwa kanga na mke wangu huku nikisindikizwa na vigelegele. Yule mwenyeji wetu aliagiza pick up yetu isogezwe ili maharusi tupande na safari ya kurudi Dar ianze.

  Niliposikia hivyo nilipata fahamu, nilichomoka hapo mbio hata wale waliojaribu kunikimbiza waliambulia vumbi. Hata sikumbuki nilifikaje barabarani maana kijiji chenyewe kipo mbali kidogo na barabara. Nilipanda basi na kurudi Dar. Nilipofika nilikushanya nguo zangu na kukimbilia Keko Magurumbasi kwa mjomba wangu. Pale nilikaa siku tatu baada ya kupata nauli nilirudi kijijini kujipanga upya…………..
   
 2. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #2
  Jun 25, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 3. MadameX

  MadameX JF-Expert Member

  #3
  Jun 25, 2012
  Joined: Dec 27, 2009
  Messages: 7,847
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  mzee sisi wengine wavivu, naomba sometimes umetuwekea mukhtasar
   
 4. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #4
  Jun 25, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  MadameX ukiona ni ndefu basi ujue haikukusu..................LOL
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 5. Mbimbinho

  Mbimbinho JF-Expert Member

  #5
  Jun 25, 2012
  Joined: Aug 1, 2009
  Messages: 6,027
  Likes Received: 2,868
  Trophy Points: 280
  Hahahahaaaa., Mkuu mbavu zangu, I can imagine the way you ran, so mkeo huyo hujawahi hata kuwasiliana naye hadi leo mkuu?:A S-confused1:
   
 6. lono

  lono Senior Member

  #6
  Jun 25, 2012
  Joined: Apr 28, 2009
  Messages: 123
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  ukome uzinzi
   
 7. Akagando

  Akagando JF-Expert Member

  #7
  Jun 25, 2012
  Joined: May 24, 2012
  Messages: 536
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Kwa hiyo Mzee,Mkeo ulimfuata au ndio ulimpotezea.
   
 8. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #8
  Jun 25, 2012
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,474
  Likes Received: 4,134
  Trophy Points: 280
  Hahahahaaah!! babu Mtambuzi kumbe tangu kijana ulikuwa mtata...
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 9. Gurta

  Gurta JF-Expert Member

  #9
  Jun 25, 2012
  Joined: Sep 17, 2010
  Messages: 2,246
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Swala la msingi hili...
   
 10. Ennie

  Ennie JF-Expert Member

  #10
  Jun 25, 2012
  Joined: Jan 15, 2011
  Messages: 7,145
  Likes Received: 54
  Trophy Points: 145
  Mtambuzi alitisha! Zilimuokoa mbio!
   
 11. Mbimbinho

  Mbimbinho JF-Expert Member

  #11
  Jun 25, 2012
  Joined: Aug 1, 2009
  Messages: 6,027
  Likes Received: 2,868
  Trophy Points: 280
  Angekuwa mwendo wa kobe, shughuli angeiona, kudadadeki, unafanya mchezo na watu wenye asili ya uamsho nini.
   
 12. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #12
  Jun 25, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Mkuu sijarudi tena Ununio, na nikikutana na mtu akiniambia anatokea Ununio namkimbia maana naogopa nisije letewa mke niliyemkimbia................
   
 13. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #13
  Jun 25, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Nimeshakoma mie................
   
 14. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #14
  Jun 25, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Nilimpotezea mkuu, si unajua maisha ya ujana kizungumkuti...............!
   
 15. Mbimbinho

  Mbimbinho JF-Expert Member

  #15
  Jun 25, 2012
  Joined: Aug 1, 2009
  Messages: 6,027
  Likes Received: 2,868
  Trophy Points: 280
  Hahahaha, mkuu huna haja ya kuogopa maana ni kitambo sana sasa, sidhani hata huyo mkeo mwenyewe anakukumbuka.
  Mkuu hivi unajua kuwa yule still ni mkeo halali kabisaa maana you never filed a divorce:dance:
   
 16. platozoom

  platozoom JF-Expert Member

  #16
  Jun 25, 2012
  Joined: Jan 24, 2012
  Messages: 7,325
  Likes Received: 2,317
  Trophy Points: 280
  Hii habari anaijua Mama Ngina?....Kimsingi umemtelekeza mke wako wa kwanza, fanya himahima umtafute....Historia hujirudia yasije yakamkuta Rejao na Cantalisia wako!!
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 17. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #17
  Jun 25, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Kwa hiyo nikikuta kaolewa naweza kum sue mtu kwa kumuoa mke wangu halali wa ndoa ya mkeka eh, yaweza kuwa dili hiyo au?
   
 18. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #18
  Jun 25, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Hii maneno haijui kabisa mama Ngina na ndio maana nimetoa angalizo hao watoto wasije tia neno humu.....................
   
 19. Mnama

  Mnama JF-Expert Member

  #19
  Jun 25, 2012
  Joined: Oct 13, 2010
  Messages: 1,651
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  Ha haaaa hii kali ,ulikuwa mkali sana mkuu ugenini lakini unakomaa nayo mwanzo mwisho mpaka kucheee...
   
 20. Bishanga

  Bishanga JF-Expert Member

  #20
  Jun 25, 2012
  Joined: Jun 29, 2008
  Messages: 15,347
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 0
  akome mara mbili?
   
Loading...