Nijuzeni kuhusu vita vya Biafra!

mpenda arage

JF-Expert Member
Nov 10, 2015
1,673
3,792
Habari zenu wakuu. Nimekuwa nikisikia habari kuhusu hii vita na jinsi Tanzania ilivyolisapoti hili jimbo katika kujitenga kutoka Nigeria. Nimepata kusoma mahali kuwa vita hivi vimepiganwa kwa muda wa miaka miwili na miezi nane, 1967-1970!! Ndipo ilipofikia tamati. Lakini kinachonipa shauku ya kufuatilia zaidi ni baada ya kugundua kuwa vuguvugu la kujitenga kwa jimbo la Biafra bado linaendelea hadi sasa!! Sababu kubwa ya kutaka kujitenga hapo mwanzo ilikuwa ni manyanyaso na mauwaji ya watu wa kusini wa Igbo, lakini kwasasa naona hii hali haipo ila bado wanataka kujitenga tu! Je kuna sababu nyingine za kujitenga, au tamaa tu za madaraka kwa waafrika?
Na Je, jimbo moja dogo limewezaje kumudu kupambana na nchi nzima kwa muda mrefu wa miaka miwili na miezi nane?
Pia nimeskia kuna mataifa ya kikristo yaliisaidia Biafra kijeshi, hii imekaaje? Au Biafra kuna wakristo tupu?!
Ni hayo tu!
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom