Nijibuni ajuaye

Nijibuni ajuaye

mahirtwahir

JF-Expert Member
Joined
Jan 12, 2013
Posts
614
Reaction score
322
Keki kavu hupendeza sio yenye maji ndani, Utaila unacheza ngoma haionekani, Kama utajilegeza utaomba hadharani, Haikwami ukimeza mambo hua burudani, Kwa kweli yanishangaza utamu hadi ndotoni. Kisu ukikipenyeza kitafika hadi chini, wala hutakikwaruza kwa keki ilivyo laini. Wengi wataka jifunza wajilie majumbani. Lakini inawatatiza hawajui kipimo nini. Hivi unafikiri ni keki gani? hebu nisaidie Jibu. Tafadhali
 
Mh! Umenikumbusha wimbo wa Solo Thang:
Mambo ya Pwani yananichanganya,
Vitu flani wanavyofanya,
Mambo ya Pwani yananichanganya,
Vitu flani wanavyofanya,
Raha ya ubwabwa tandu,
Raha demu chachandu,
Utamu ukizidi sana sema bandu bandu,
Kuna walofata nyuki wakatokwa na manundu,
Waloitaka sukari wakaipata shubiri,
Ana hamu ana hamu lakini ana gundu,
Kalilia bakora kakutana na kirungu...
 
Sasa mafumbo yanatusaidia nini humu! Halafu unataka tukuite great thinker. Kayadiscuss na great fool wenzako
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom