Nijibu matusi? Hapana, najibu hoja tu!.

Nijibu matusi? Hapana, najibu hoja tu!.

Kuna kila dalili kuwa yaliyotokea 2015 yatatokea 2020 kwa upande wa wapinzani. Miezi michache kabla ya kura 2015 Prof aliweka mpira kwapani akakimbilia Rwanda kupumzika na mwenzie alifanya hivohivo kwa kuwakandia Lowassa na Duni kwa hiyo upinzani ukakosa kuchukua dola, kwanza hamna dalili hata ya kupata wabunge (Ten)10 Tz Bara baada ya kushindwa wakati chama tawali kilikuwa hoi bin taabani, Ifikapo September 2020 mchezo huo utajirudia kwani wapinzani (Chadema & ACT Wazalendo) wana ubinafsi kama ilivyoonyeshwa viongozi wa ACT 2015!!!!
Kama wapinzani wenyewe ndio hawa kina Yeriko acha tu CCM iongoze milele na milele
 
Nyendo zipi hasa za Zitto zinahatarisha usalama/uwepo wa CHADEMA?
Lissu ni mtu mzima na ana utambuzi/uelewa wa kiwango kinachoridhisha. Kwa vigezo vipi unasema analishwa uongo? Inamaana Lisu hawezi kuchanganua kati ya urongo na ukweli?
Kwa hoja zipi unaiona ACT kama Wapinzani wa CHADEMA? Maana Maalim alivyohamia tuu ACT uliweka bandiko la kuponda kitendo hicho.
ila we jamaa una akili fupi "think out the box siasa ni zaidi ya mbowe lisu au zito
alichokifanya zito cha kupitia mlango wa uwani kinaaribu reputation ya chama (chadema)
 
HIVI KUNA HAJA GANI KU QUOTE UZI MREFU NAMNA HII??!!!!
 
Yericko with all due respect Zitto hakutweet hiyo tweet kama independent tweet alikuwa anajibishana na Absalom Kibanda ila nashangaa kila mara kuitumia hiyo tweet kama ndo ushahidi maana unaitumia out of context, Zitto alijibu kuringana na mjadala wa Kibanda sasa wewe ndo umeamua kutumia hiyo tweet kama fimbo.Be hfair kama kweli unajibu hojav inginevyo utaonekana wewe unachuki binafsi maana CHADEMA nzima unaongea wewe tu hata Lissu mwenyewe jana kakazia uhusiano wake na Zitto.
Yukosahihi ,zito alitoa mifano hivyo itumike mojakwamoja
 
Napokea sms nyingi kwamba nijibu mapigo kwa mashambulizi ninayofanyiwa na baadhi ya vijana wachanga katika siasa za kiswahili, lakini nataka kuwajibu wale wanaonishauri nijibu kwamba, huwa sijibu mashambulizi binafsi yanayolengwa kwangu, bali huwa najibu mashambulizi ya HOJA zangu tu. Siku wakijibu hoja zangu watapata bahati ya mtende nitawajibu kwa hoja pia.

Hoja zangu za tangu juzi ziko wazi na hazihitaji mishipa ya kichwa ikutoke kujibu, hoja hizi zilitokana na tweets mitandaoni za Ndugu na Kaka yangu Zitto Kabwe baada tu ya kufika Ubelgiji kumjulia hali Mwanasheria wa Chadema Wakili msomi Mh Tundu Lissu, na katika moja ya tweet alisema, Tanzania inawanasiasa wawili tu ndio watakaoleta mabadiliko, ambao yeye Zitto na Lissu. Tweet nyingine ikasema, "what a pair? What more Tanzanians need? The pair will Transform economy and reform criminal Justice system". Tweet hii ikaambatana na video akiwa na mh Lissu huko Ubelgiji na huku akitamka "we are coming"

Baada ya tweet hiyo nikamwambia haya,

Nanukuu.

"Huu ni uchonganishi na ufitinishi unaoufanya ndugu @zittokabwe ama unajua unachokifanya au hukijui unachokifanya,
Lengo lako ni kumgombanisha Mh Lissu na Chama chake, Na hili kwa siku kadhaaa umekuwa na juhudi za kumtenganisha Lissu na chama chake, juhudi za kubomoa chadema kwa staili ya kumremba huku ukimtoa kwenye mitazamo ya chama chake.

Hii tabia acha mara moja, acha haraka mkuu, upinzani nchini unahitaji umoja lakini umoja wenye nia ovu ya kuvunja chama kingine haukubaliki.
Chadema itatoa mgombea, Chadema itasimamisha mgombea wake, kushirikiana na vyama vingine ni suala la chama kama taasisi kukaa vikao na kuamua sio suala la mtu mmoja, Chadema ina mtaji mkubwa wa watu wenye sifa ya Kugombea urais, ukianza na Mwenyekiti Mbowe, Lissu, Nyalandu, Sumaye, na mifano mingine kedekede, hawa wanaweza kusimama bila kuhitaji msaada wa Ziito ikibidi,
Zitto tunakuhitaji kama mwanachama tunakuhitaji kama kiongozi, lakini hatukuhitaji utugawe kwa maneno ya aina hii, jenga chama chako, usibomoa chama chetu, Nenda muone mgonjwa lakini usianze kumtenganisha ama kumgombanisha na chama chake. Lissu ni Chadema, huwezi kumpenda Lissu kisha ukachukia chama chake.

Nyendo zako zinafahamika hatua kwa hatua, unaihitaji Chadema sawa na chadema inavyohitaji vyama vingine lakini mwenendo wako na mipango yako inaondoa uaminifu wako kwa wapinzani wenzako. Kumlisha uongo Lissu kwa maslahi yako kisiasa hii haitakubali.

Hii tweet yako ni kipimo muhimu sana na alama ya tabia yako kuwa haujabadilika licha ya kujutia kwako mara kadhaa. Nakushauri kijana mwenzangu, pitia njia sahihi ya chadema kufikia malengo yako na yetu ya Umoja wa Upinzani nchini.

Njia unayopita sio sahihi, si njia ya kutupeleka kwenye umoja wa Upinzani, bali ya kutugawa na kuinufaisha ccm juu ya mgawanyiko wetu. Njia sahihi ni moja tu, peleka maombi rasmi ya kichama mezani pa Chadema, chadema itayachakata na kukusikiliza ama kukubali ama kukataa, Hii lobbing yako ni ya kisaliti. Tutaizuia". Mwisho wa kunukuu.

Hoja za mjadala zilikuwa kama hivi hapo juu, hivyo wanaojaribu kujibu hoja hizi wazijibu sio kunitukana mimi, mie nilishatukanwa tangu nikianza balehe hadi leo nimezeeka na ndevu za shaba na situmii vumbi la kongo, hivyo hakuna tusi ambalo sijawahi kutukanwa na huwa sijibu kabisa,

Labda niwafafanulie kwanini niliamua kumshauri na kumkanya Zitto kwa kuweka hoja hapo juu. Kimsingi wote tunataka muungano ili kurahisisha kuiondoa ccm, lakini hoja inakuja tunaungana ili kufurahisha watu waone muungano au tunaungana na chama kilichomakini chenye commitment kama yetu Chadema?

Chama hicho ni kipi? TLP? Cuf? NCCR? ACT?
Hulka za wakuu wa vyama hivyo hapo juu zinachakatika?

Baada ya Uchaguzi Zitto ameleta maombi katika chama akitaka kurudi, chama hakikukurupuka kumpokea kikaamua kumtafakari kwanza, na baadae akageuza kibao kati ya 2016 hadi septemba 7, 2017 akawa anatushambulia kuliko tunavyoshambuliwa na ccm, Baada ya Lissu kushanbuliwa kwa risasi, akaleta maombi kwamba anaomba asije yeye bali aje kwanjia ya muungano kichama yaani ukawa mpya,

Maombi hayo yakasikilizwa katika kikao cha viongozi na wadau wa siasa kilichofanyika Hoteli ya Verde, na baadhi ya viongozi walioshiriki walimwambia Zitto kwamba maamuzi yanayohusu muungano au mashirikiano yanafanywa na vikao vikuu vya chama, hivyo wao kama wawakilishi wa chama hawana mamlaka ya kuamua hilo jambo, wakampa kazi Zitto kwamba kwa sasa kila chama kijenge chama chake na kueneza sera zake, muda wa uchaguzi ukifika kama kutakuwa na ulazima basi chama kupitia vikao vyake kitatafakari maombi hayo kwakutathimini kwa umakini faida na hasara za mashirikiano hayo,

Chama chetu kiko kwenye mchakamchaka wa kujenga mtandao wake, huku kikiwa bado hakijampa nafasi ya maombi bwana Zitto, na hili sio kwa bahati mbaya bali ni kutafakuri athari zake kwa sasa kulingana na malengo ya uanzishwaji wa chama hicho cha ACT na tabia ya kiongozi wake. Wakati maombi yake yakisubiri mjadala wa kichama kivikao, mwaka jana chama kikamkaribisha kama mshirika kwenye mambo madogomadogo hasa kufungua kesi ya kikatiba kupinga sheria ya vyama vya siasa, kikao kilichokalika makao ya chadema na ikaamuliwe iwe siri, ajabu kikao kikiwa kinaendelea ni zitto huyohuyo akatangaza mitandaoni juu ya kikao hicho na picha juu,

Chama kikaona huyu bado ni walewale, kikaamua kusubiri kidogo maombi yake, wakati subira hiyo ikiendelea, yeye akapanda ndege kwenda Ubelgiji na kujaribu kupeleka "uongo" flani ambao ungekubalika ungetugawa, akiwa palepale ubelgiji akijua kua ni uchonganishi, akaposti mitandaoni na kutangaza ushirikiano kuelekea 2020 akimtaja mwanachama wetu Lissu katika tweet zake jambo ambalo ni kuingilia mamlaka ya taasisi nyingine, amefanya haya kama njia ya kushinikiza maombi yake yajibiwe na chama, kwamba cc ikikaa isiamue tofauti na alichokitangaza mitandaoni na umma ukamshangilia..

Hivyo kitendo chochote cha sisi watiifu kwa chama tungekaa kimya ilikuwa ni kubaliki shinikizo la Zitto kwa chama chetu, maana chama kingeamua tofauti watu wengi ambao wanamwamini Zitto na ambao waliona tangazo lake la Muungano na video akiwa na Lissu wangetuona sisi CHADEMA hatufai. Ndio sababu ya sisi wanachama wa kawaida kumjibu zitto on the spot. Hivi ndivyo siasa zinavyotakiwa, matamanio yako yasiyumbishe maamuzi ya taasisi.

Kwa sasa Zito ana cheza michezo miwili kwa wakati mmoja, moja, Zitto anataka afanikiwe kuinasa Chadema/Lissu ili abebwe kisiasa bara angalau apate wabunge kadhaa na kisha ACT kuja kuwa chama kikuu cha upinzani akiwa na uhakika kuwa Zanzibar hakosi wabunge 20 hivi akijulimsha na viti maalumu basi atakuwa na wingi wa viti bungeni.

Pili ni kujaribu kuiblackmail ccm kwamba sasa Zitto anaunga na Chadema watakuwa na nguvu ya kuiondoa ccm, hivyo anaitongoza ccm ikae nae chini ifanye nae biashara ile aliyokuwa akifanya nayo utawala uliopita...hili anacheza kamari zaidi hana uhakika kulingana na misimamo ya mwenyekiti wa ccm.

Ni uamuzi wa Chadema kama itaamua itumike kuwa daraja la siasa za ACT au ilinde mtaji wa wanachama iliovuna vya kutosha toka Chadema ni msingi ambao hado leo inakadiriwa kusajiri wanachama milioni 36.
Kwa dalili hizi za Zitto ni wazi huyu hajabadilika bado ubinafsi ni mkubwa na unamtesa sana na njia sahihi kwa Chadema iachana na kushughulikia maombi yake, isimame kwa kutumia mtaji wake wa kisiasa, raslimali zake, na mgombea wake muhimu ambae dunia inamjua na itasimama nae daima. Tuendelee kumuombea Lissu wetu apone haraka.

Na Yericko Nyerere
View attachment 1206101

Kwani na Wewe huwezi Kuishi maisha nje ya Siasa au harakati za Kisiasa hadi kila mara uwe katika Mikwaruzano ya mara kwa mara na Wanasiasa? Mbona nakuona Wewe bado ni Mtu ambaye hata ukisema uachane na hizi Kelele za Kisiasa ila ukiwekeza vyema katika Kipaji chako, Uweledi wako na Fikra zako bado unaweza Kuishi maisha mazuri, ya raha na amani tele kuliko kila Siku kupigizana Kelele na Wenzako ambako pia kunakupunguzia Hadhi fulani kwa wanaokuamini japo pengine kwa Ujeuri tu na Kiburi chako unaweza ukawa bado hujaligundua hilo.
 
Wanaumiaxwasioelewa siasa na tweet ya zito.
Malisa gj uko sahihi.
 
Una wivu sana na Zitto
Yericko anajisahaulisha kwamba Zitto ni kiongozi wa ACT, na wajibu wake ni kuijenga ACT. Ni Yericko huyuhuyu aliyepiga mayowe Maalim Seif alipohamia ACT.

Kama Zitto anaona Lisu anaweza kumsaidia kuinua chama chake, si dhambi kufanya naye mazungumzo. Kuweweseka kwamba Zitto analenga kuibomoa chadema ni kijidhalilisha kwa kuwa Lisu ni mtu mwenye akili timamu anayeweza kufikia maamuzi bila kurubuniwa na mtu yeyote, vinginevyo utuaminishe kwamba naye ni bidhaa inayojiuza kirahisi kama ilivyotokea wakati Ngoyai anapewa ugombea urais chadema.
 
Nakumbuka jamaa alitupiga changa la macho kuwa Yeye ni mtoto wa Nyerere halisi! Mpaka alipoumbuliwa na mtoto mkubwa wa mwalimu Nyerere humu JF! Tangu siku hiyo simuamini tena huyo mtu!
Hebu tuwekee huo uzi alioumbuliwa na kijana mkubwa wa nyerere
 
ila we jamaa una akili fupi "think out the box siasa ni zaidi ya mbowe lisu au zito
alichokifanya zito cha kupitia mlango wa uwani kinaaribu reputation ya chama (chadema)
Hongera nyie wenye akili ndefu ambao mnaudunisha uwezo wa akili wa Wakili msomi mwenye uzoefu TL Kwamba anapigwa kamba na kijana ZK
 
Swali zuri
ila kwa sisi wenye kadi 3 bado tuko imara

Wewe ni msemaji wa chadema Yericko Nyerere ?
Chama hakina utaratibu wake wa kujisemea pindi kikiona misingi yake inavurugwa?
Au na wewe ni mwanaharakati huru wa kukitetea chama na mwenyekiti mbowe kama alivyo musiba?
 
Shikamoo Yericko, kama ingekuwa nyoka basi umegonga kichwa. Hongera sana babaaaa.
 
Umeongea mambo mengi yakiwemo ya kwenye vikao! Ningependa tu kufahamu cheo chako kwenye hicho chama chako. Umeongea kama Tumaini Makene hivi, msemaji wenu wa chama.
Cheo chake ni mng'arisha viatu wa DJ.
 
Yericko ana wivu sana! Kisha nmemdharau sana alipowataja Nyarandu na Sumaye kwamba ni wagombea wa urais wanaofaa ndani ya chadema[emoji23][emoji23][emoji23]

Yericko angekaa tu kimya maana ataumbuka sana siku Lisu anaenda ACT
 
Back
Top Bottom