Nigerians defame african's reputation india | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nigerians defame african's reputation india

Discussion in 'International Forum' started by RUSHAMAWE, Jan 9, 2011.

 1. R

  RUSHAMAWE Member

  #1
  Jan 9, 2011
  Joined: Oct 10, 2010
  Messages: 7
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mimi ni mwanafunzi wa MA(masters degree) ktk chuo kimoja hapa New Delhi nchini India. Majuzi tulipata tour ya kutembelea mji muhimu wa India (Mumbai) kwa ajili ya kujifunza mambo mbalimbali ya kihistoria yahusuyo India. Baada ya kumaliza tour yetu tulihitajika kurudi New Delhi, kwa vile kilikuwa kipindi cha sikukuu ilituchukua muda kupata tiketi ya treni kutoka Mumbai mpaka New Delhi. Niliamua kuomba msaada kwa dada mmoja wa kihindi(my classmate) ambaye kwa kipindi hicho alikuwa Mumbai ili kutusaidia kupata tiketi ya kurudi Delhi, nilikuwa mimi na rafiki yangu kutoka Sudani ya Kaskazini.

  Bila hajizi huyu dada alitusaidia na tukapata tiketi ya kurudi Delhi( ya tarehe 1/1/2011) kwa bahati mbaya treni ilichelewa kwa masaa 18, yaani ilitakiwa tuondoke kesho yake saa kumi na moja na nusu alfajiri. Kwa vile tulikuwa na mizigo tuliamua kutafuta hoteli ya bei rahisi ili tuweze pumzika mpaka kesho yake alfajiri. Tulimwomba huyu dada wa kihindi atusaidie kutafuta cheap hotel.

  Cha kushangaza kila hoteli tuliyokuwa tukienda walitukatalia!! tulitembea zaidi ya hoteli nne na zote hatukuruhusiwa kuingia, tulipomtizama yule dada usoni alionesha sura ya huzuni. Mwishowe tulimuuliza kwa nini wanatukatalia kupata hifadhi wakati wameandika "rooms available"!! alitujibu " wanaogopa kuwahifadhi waafrika kwa sababu hawana leseni , waafrika wengi na hasa kutoka NIGERIA wamekuwa wakihusishwa na kesi za madawa ya kulevya hapa India!! hivyo inahitajika leseni maalumu ili kuwahifadhi waafrika!!!""

  Jambo hili lilitusikitisha siku nzima, hata safari yangu yote ilikuwa ya huzuni mpaka jirani yangu(mhindi) aliniuliza "unaumwa"...!!nikamjibu nope...ni uchovu tu!! Hili jambo si mara ya kwanza kutokea, wanafunzi wengi wa kiafrika wanaosoma India wanahistoria tofauti. Jamaa yangu mwingine kutoka Sudani ya Kusini alikuwa anatafuta chumba cha kupanga hapa delhi, ilibidi atembee na passport!! kila walipomwona walidhani ni Mnaigeria hivyo hawakumruhusu hata kuzungumza nao.

  TAFADHALI NDUGU ZETU WANAIGERIA(WACHACHE) JIREKEBISHENI....MNATUPA WAKATI MGUMU SANA WANAFUNZI WA KIAFRIKA TUNAOSOMA NCHINI INDIA!!
   
 2. The Dreamer

  The Dreamer JF-Expert Member

  #2
  Jan 9, 2011
  Joined: Feb 2, 2009
  Messages: 1,280
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Pole
   
Loading...