Kama ilivyokuwa kwa rais wa Tanzania Jakaya Kikwete rais wa Nigeria Goodluck Jonadhan naye aingia mitini kwenye debate ya wagombea urais wa nchi hiyo. Inasemekana alitaka apewe maswali yatakayoulizwa in advance lakini waandaaji waligoma kufanya hivyo. Tunajifunza nini kutokana na watawala wetu hawa!
Itakuwa jambo la maana presidential debate ikawekwa kwenye Katiba mpya pia. Ili wanaoomba kuwa Rais wasiweze kukwepa unapofika wakati wa debate.
Hii inaweza kusaidia waomba urais kama watachaguliwa kwa kipindi cha kwanza waweze kuwa accountable kwa ahadi walizotoa au "kuvuliwa nguo hadharani" siku hiyo ya debate.
Simply, wagombea wataogopa kutoa ahadi hewa. Wasipotekeleza wanajua kuwa wataumbuliwa kadamnasi.
Ahadi za kubadilisha mji wa kigoma kuwa Califonia kwa miaka mitano hazitakuwepo.