Nigeria yamwita Obafemi Martins | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nigeria yamwita Obafemi Martins

Discussion in 'Sports' started by MziziMkavu, Sep 25, 2009.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Sep 25, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,617
  Trophy Points: 280
  Nigeria yamwita Obafemi Martins
  [​IMG] [​IMG]
  Obafemi Martins ameitwa tena kuchezea Super Eagles Nigeria imemuita tena mshambuliaji Obafemi Martins kujiunga na timu ya taifa ikijiandaa kwa mchuano muhimu wa kufuzu kwa kombe la dunia dhidi ya Msumbiji mjini Abuja mwezi ujao.
  Mara ya mwisho ambapo Martins mwenye umri wa miaka 24 alichezea Super Eagles ilikuwa dhidi mara ya Msumbiji miezi mitano iliyopita.
  Martins amejiunga na klabu ya Wolfsburg ya Ujerumani baada ya Newcastle kushushwa kutoka ligi ya Premier ya England.
  Hajakuwa akiitwa mara nyingi kuichezea timu ya taifa, kutokana na tabia yake ya kukataa kwenda anapoitwa, lakini anasisitiza kwamba anakosa kueleweka.
  Ameambia kitengo cha BBC cha michezo kwamba majeraha ndiyo yaliyomtatiza.
  Kocha Shaibu Amodu pia amemwita mlinzi wa klabu ya Charlton Sam Sodje , pamoja na Peter Utaka anayecheza soka ya kulipwa Denmark na Chibuzor Okonkwo wa Klabu ya Bayelsa United.
  Super Eagles tayari wanamkosa mshambuliaji Ikechukwu Uche aliyepata jeraha majuma mawili yaliyopita akichezea klabu yake ya Real Zaragoza huko Uhispania.
  Uche ndiye aliyefunga mabao mengi zaidi katika michuano ya kufuzu kombe la dunia mwaka 2010 akiwa na mabao manne , na jeraha lake ni pigo kubwa kwa Nigeria ambayo inakabiliwa na kazi ngumu ya kuweza kufuzu kwa kombe la dunia nchini Afrika Kusini.
  Nigeria iko katika kundi B ikiwa na pointi 7 na inashikilia nafasi ya pili nyuma ya Tunisia ambayo ina pointi 9.
  Super Eagles wanahitaji kushinda mechi zao mbili za mwisho , na pia waombe Tunisia ipoteze mechi dhidi ya Kenya au Msumbiji, ili kushika nafasi ya kwanza.
  Mechi inayofuata ya Super Eagles ni dhidi ya Harambee Stars ya Kenya tarehe 14 mwezi November.
  Kikosi kamili cha Nigeria:
  Makipa : Greg Etafia (Moroka Swallows, South Africa), Vincent Enyeama (Hapoel Tel Aviv, Israel), Dele Aiyenugba (Bnei-Yehuda, Israel)
  Walinzi : Onyekachi Apam (Nice, Ufaransa), Elderson Echiejile (Rennes, Ufaransa), Sam Sodje (Charlton Athletic, England), Taye Taiwo (Olympique Marseille, Ufaransa) Joseph Yobo (Everton, England),Danny Shittu (Bolton, England), Chibuzor Okonkwo (Bayelsa United), Dele Adeleye (Sparta Rotterdam, Uholanzi), Yusuf Muhammed, Obinna Nwaneri (wote wawili FC Sion, Uswizi), James Okwosah (Lobi Stars), Adefemi Olubayo (Boulogne, Ufaransa)
  Viungo : John Mikel Obi (Chelsea, England), Sani Kaita (Lokomotiv, Urusi), Yusuf Ayila (Dynamo Kiev, Ukraine), Seyi Olofinjana (Hull City, England), Dickson Etuhu (Fulham, England), Oluwafemi Ajilore (Groningen, Uholanzi), Nwankwo Kanu (Portsmouth, England),
  Washambuliaji: Chinedu Ogbuke Obasi (Hoffenheim, Ujerumani) Osaze Odemwingie (Locomotiv Moscow, Urusi), Obinna Nsofor (Malaga, Uhispania), Michael Eneramo (Esperance, Tunisia), Obafemi Martins (Wolfsburg, Ujerumani), Yakubu Ayegbeni (Everton, England), Peter Utaka (Odense, Denmark), Joseph Akpala (Club Brugge, Ubelgiji)
  http://www.bbc.co.uk/swahili/news/story/2009/09/090924_obafemi_nigeria.shtml
   
Loading...