Nigeria yakomesha 'Bring Back our Girls'

Nigeria yakomesha 'Bring Back our Girls'

figganigga

Platinum Member
Joined
Oct 17, 2010
Posts
27,908
Reaction score
63,589
140603020528_polisi_wa_nigeria__512x288_bbc_nocredit.jpg

Polisi wazuia maandamano Nigeria


Polisi nchini katika mji mkuu wa Nigeria, Abuja wamepiga marufuku maandamano ya watu wanaowaunga mkono zaidi ya wasichana wa shule mia mbili waliotekwanyara na kundi la wanamgambo wenye itikadi kali za kiislamu la Boko Haram mwezi Aprili.
10345850_792499207435413_8779609118889510690_n.jpg

Maandamano yamekuwa yakiandaliwa kila siku kwa kipindi cha zaidi ya mwezi mmoja kuishinikiza serikali kutia bidii zaidi katika juhudi za kuwakomboa wasichana hao.
Polisi wanasema maandamano hayo yanamepigwa marufuku kwa kuwa yanazua hatari kwa wenyeji.


Aibu kwa serikali


Kampeini ya 'Bring back our Girls, au warudisheni wasichana wetu,'' ambayo imekuwa ikifanywa nchini Nigeria na hata nje ya Nchi hiyo imeleta aibu kubwa sana kwa serikali ya Nigeria.


Waandamanaji wamekuwa wakikutana hadharani wakiishinikiza serikali hiyo kukoma kuzungumza tu katika vyombo vya habari na badala yake waongeze jitihada na kuhakikisha wasichana hao wamekombolewa.
makosa sio ya serikali


Lakini wiki iliyopita, kundi tofauti lilianzisha kampeini sambamba, na hata kuvuruga ile ilyokuwa ikiendelea ambapo wanadai kuwa hasira zinastahili kuelekezewa hao watekaji nyara na wala sio serikali ya Nigeria.


Kundi hili linatumia nembo 'Release Our Girls Boko Haram'. Wameongeza jina Boko Haram kwa kusudi hapo mwisho.
Polisi sasa wanasema kuwa maandamano haya yanatishia usalama kwa wananchi wa Abuja.


Lakini waandamanaji wanaoendesha kampeini ya 'Bring Back our Girls' sasa wanaona kama hili ni jaribio la serikali kuwanyamazisha na wamewasilisha ombi mahakamani kutaka kutolewe agizo la kuvunja amri hiyo ili waruhusiwe kufanya maandamano yao.

Chanzo;BBC
 
Safi sana serikali ya Nigeria, hizi NGOs zinazojifanya za kudai haki, nyuma yao huwa kuna mikono ya Ujasusi wa West!
 
Back
Top Bottom