Nigeria wanaye mpiganaji mwingine a.k.a mfia timu Victor Moses

Messi Lionel

Senior Member
Jan 11, 2018
170
159
Nigeria ni moja kati ya mataifa ambayo yamefanikiwa sana katika masuala mbalimbali hasa uchumi barani Afrika,elimu hata utamaduni..
Lakini watu wengi wanapoliskia jina la Nigeria hujikuta wakilitafakari taifa hilo kama taifa la kisoka Afrika..
Hii hutokana na mfumo wa ukuzaji wa vijana katika vituo vya watoto vya soccer(Academies) walivyonavyo ambavyo vimeleta mapinduzi katika soka lao..


Tangu enzi za kina Tijan Babangida,Celestine Babayaro,Austin Jayjay Okocha,Taribo West,Finidi George,Julius Agahowa,Emanuel Amunike,Nwanko Kanu mpaka kizazi cha kina Vincent Enyeama,Joseph Yobo,Yakubu Aiyegben,Obafemi Martins,Odemwingie na sasa hichi cha kina Kelechi Iheanacho,Obi Mikel,Alex Iwobi na sasa bado wana mpiganaji mwingine a.k.a mfia timu Victor Moses..
Chelsea au The Blues au kama wanavyojiita Fahari Ya London(The Pride of London) wamevuna mali tena kutoka Afrika kama ambavyo waafrika wengi wamekuwa wakiibeba chelsea na wengi tunawafahamu kina Didier,salomon Kalou,Michael Essien na wengi wengi..


Katika kampeni yao ya ubingwa msimu uliopita kama kuna mtu aliyekuwa chanzo cha mfumo wote wa timu ni Victor Moses..kadri anapokuwa uwanjani ndipo Antonio Conte anavyopata ahueni..Jamaa katika mfumo wa 3-4-3 alikuwa moto kupita kiasi,mipira ya kushambulia unampata..mipira ya kuzuia unampata.
Ukitaka kufahamu Moses hayupo uwanjani basi utaiona spidi ya upande wa kulia wa chelsea inavyoshuka..


Tangu alipozaliwa Disemba 12 1990 jamaa amepita katika historia ngumu sana..Kwanza kabisa Baba Yake Mr.Moses alikuwa Mchungaji wa kikristo huko Nigeria na jamaa akiwa na umri mdogo kabisa unaambiwa wazazi wake waliuawa huko Nigeria hivyo ndugu zake kuamua kumchangia kiasi flani cha pesa ili aende kusoma huko uingereza..
Ni huko shuleni ndiko Maskauti wa Crystal Palace walipoamua kumchukua na kumpeleka katika majaribio katika timu yao Crystal Palace wanaotumia uwanja wa Selhurst Park..
Alifanya vizuri sana akiwa na Palace hivyo mwaka 2010-2012 akafanikiwa kusajiliwa na kuitumikia klabu ya Wigan Athletic ambapo ndipo aliponga'a zaidi akichukua nafasi iliyoachwa na Charles N'Zogbia..


Mwaka 2012 the blues wakaona dodo chini ya mnazi na kufanikiwa kumsainisha mapema ambapo walimpeleka timu mbalimbali kwa mkopo kama Liverpool(the kops),Stoke city(the potters) na Westham united(the hummers) lakini alipoichukua timu Muitaliano Conte ndipo kufufuka kwa Moses kulipoanzia maanake kwa nishati yake yeye na mwenzake wa kushoto Marcos Alonso walisababisha mfumo wa Conte uonekane bora zaidi huku viungo kama Kante,Matic,Fabregas wakicheza nao sambamba..
Moses amefanikiwa kucheza timu ya Taifa ya England kwa ngazi zote za chini kama chini ya miaka 16,17,20,21..lakini timu ya wakubwa (Senior Team) hakufanikiwa kucheza na ni kwasababu aliamua kucheza katika taifa lake Nigeria ambapo amefanikiwa kushinda ubingwa wa Kombe la Mataifa ya Africa(Afcon)..kucheza kombe la dunia 2014...


Chelsea imekuwa na wapambanaji wengi hata msimu huu lakini wengi wamefanikiwa kuyaweka majina yao midomoni mwa mashabiki wa soka kama Eden Hazard,Willian,Pedro Rodriguez,Diego Costa,Cesc Fabregas,Thibaut Curtois,Gary Cahill,David Luiz,hata John Terry aliyeondoka Lakini kwangu mimi Hero wangu amekuwa ni Victor Moses mtoto wa Pastor..

[HASHTAG]#footballaddicted[/HASHTAG]
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom