Nifanyeje nisimchoke mpenzi niliyenaye?

artesunate

Member
Mar 20, 2016
6
0
Jamani natumaini wazima wote,

Ushauri wenu ni muhimu sana nikijumlisha na mawazo yangu.

Nimekuwa mtu ambaye nashindwa kumpenda mwanaume muda wote nimekuwa nampenda mda mfupi tu alafu nakuwa bize na mambo yangu kila nikijaribu kuwa naye karibu najikuta nashindwa.

Hadi sasa nimekuwa na mahusiano ya watu 4, japo nahitaji mwenza lakini wote hao sijisikii kuwa nawo sasa nimechoka hii hali ya kubadili wanaume.

Naombeni ushauri nifanye nini niweze kutokumchoka huyu niliyenaye, siipendi hii hali. Msaada tafadhali.
 
Hahahaha huyo uliye nae ni wa NNE na bado na yeye yuko hatihati kuachwa; vitu gani huvipendi kwake ambavyo mwanzo hukuviona? Aidha utakuwa hujawa tayari kukaa au kuishi na Mwanaume tambua kuwa ndoa ni uvumilivu tu wala hakuna kungine.
 
Kuna Fupi-nene na Ndefu-nyembamba
Sijajua ni ipi ambayo angalau inayoweza kukutuliza
 
Lol huezi kumpata mtu perfect...

Huezi kuletewa ulimwengu mzuri miguuni pako

Kwanza hayo

Pili tambua wewe ni nani aka jitambue

Hii itakusaidia ku identify ur requirements n needs

Once ukishatambua hayo then believe in working on urself..


Then when u start working on urself it is when you will glow super self esteem...


Lastly kama haujaelewa mtafute councellor...

Do the home work on looking for the best councellor...

All the best
 
jamani natumaini wazima wote
ushauri wenu ni muhimu sana nikijumlisha na mawazo yangu, nimekuwa mtu ambaye nashindwa kumpenda mwanaume muda wote nimekuwa nampenda mda mfupi tu afu nakuwa bize na mambo yangu kila nikijaribu kuwa naye karibu najikuta nashindwa hadi sasa nimekuwa na mahusiano ya watu 4 japo nahitaji mwenza lakini wote hao sijiskii kuwa nawo sasa nimechoka hii hali ya kubadili wanaume,naombeni ushauri nifanye nn niweze kuto kumchoka huyu niliyenaye .....siipendi hii hali msaada tafadhali
Labda unavutiwa na jinsia yako (lesibian) jichunguze vizuri
 
Relax..wala usikurupuke,when the right person comes we mwenyewe mbona moyo utakuwa unadunda dunda na ubize utaisha. Don't forget to pray.
 
Wanne bado hujapata unayempenda.

mapenzi haya. Hebu jitafakari shida nini kwako.

Je mambo yako yakuwa bize sana au kingine?
 
Endelea kubadilisha mpaka upate usiyemchoka then kapime na ukimwi...!
 
Unawakubalia mahusiano bila kuwapenda au? Angalia vigezo vyako halafu uwasubirie wenye vigezo ivyo... Japo unapaswa kupunguza vigezo mana mwisho wa siku itaishia chaguo bovu kupita yote ulopitia
 
Back
Top Bottom