Nifanyeje mwenge ukija wilayani kwangu?

mgeni wenu

JF-Expert Member
Jan 2, 2012
3,664
1,730
Jeshi la Polisi baada ya kuruhusu mkutano wa kisiasa wa wapinzani wetu, UKAWA na kutoa masharti juu ya kuzuia maandamano, kuviongelea vyama vingine, mapokezi, lugha za kashfa na matusi, waliruhusiwa kuendelea na mkutano kwa mujibu wa Barua ya OCD Kahama.

Lakini yalitoka maelezo ngazi za juu, kuwa hawaruhusiwi kabla hawajaondoa vyombo vyao uwanja, mabomu ya machozi, maji ya kuwasha na vurugu zikaleta sintofahamu katika mji wa Kahama, licha ya kuwa na Barua ya OCD.

Kwa kile kilichoelezwa na ngazi za juu Mikusanyiko kwa sasa hairuhusiwi kwa kuwa hali ya usalama ni tete, ikiwemo watu kuuwawa kila baada ya muda fulani maeneo tofauti ndani ya nchi, kwa kuwa hali haijatulia na mwenge ni kusanyiko na ni mkutano wa kisiasa, naomba ushauri nijitokeze kwenda?

Maana pia hukesha sio mchana tu, nimeshindwa kabisa kupambanua hili wa CCM wenzangu na mliopo humu nisaidieni ili nisije jikuta napata wakati mgumu
 
Mama nyani akitaka kujua kama mwanae amekua humchanganyia mahindi na mawe. Mtoto akichambua tuu. Anapigwa akajitegemee.......changanya na zako
 
Back
Top Bottom