Nifanyeje mume wangu aniamini tena?

Fact mkuu wangu
 
Una asili ya uchoyo? Au m binafsi? Mficha uchi hazai funguka kweli ili tujue, kama upo fresh basi lipo tatizo ndugu ( mambo ya tamaduni mzee baba wanamnyunyizia maana rizki ipo)
 
Pole.
Huyo mmeo atakuwa na lake jambo hata kama ni kusaidia ndugu kuwe na kiasi sio hadi usahau kwako.
Mwambie tu kila kitu kwamba yuko tofauti na zamani afu muulize tatizo nn.

 
Bora tu kutoshirikishwa kuliko kupitisha bajet kama bunge alafu pesa zinaishia kwingine.
Na wewe c una mikono miwili? Tafuta zako ufanye mambo yako. Siku hizi ndoa nyingi zipo kwa ajili ya kuwa na uhakika wa kupata sex iliyo halali.
 
Mbane wakati wa mechi umuulize kulikoni

Sent from my Iphone using Tapatalk
 
 
Huyo sio mume wako. Angekua mume wako, kwao ni kwenu. Kwenu sio kwenu tena.
Nimemaliza
 
Wewe sema amekuwa anakupa hela uweke kwa ajiri ya maendeleo yenu wewe unazifuja sasa kaamua kusimamia yeye mwenyewe unaanza kulia lia
 
Na wewe unachangia kwa kiwango kipi kwenye hilo pato? Maana usije ukawa mshauri kumbe na wewe hauchangii sasa jamaa kaamua afanye kivyake unalalamika. Anyway ndoa changa zinamatatizo
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna kitu hujajikieleza hapa

Na wewe ulikuwa unaweka mshahara wako mezani au mshahara wake tu?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa tulioa tunajua ambacho huwa kinatokea.

Wanawake huwa wanawishi muwe na maisha ya kizungu(nuclear family).
Sasa hayo maisha wanataka yawe upande wa mwanaume tu. Kwao inakuwa extended family.!!

Yaani ndugu zake wasaidiwe kadiri ya watakavyo ila ndugu wa mwanaume Ni kuwakaushia tu.!! Wameshindwa kulibalance Hilo.

Mimi mambo ya kwetu huwa simshirikishi.
Natunza familia na mambo ya kwetu nayafanya bila kumuambia
Maendeleo yangu binafsi nayafanya.
Kwa hiyo habari za ndugu yangu kuomba visivyokuwa vya maana huwa namalizana nao mwenyewe.!!

Na ili ufanikiwe Hilo mwanaume hutakiwi kumwambia mwanamke Kila kitu unachokipata.
Lazima uwe na mpango wa kando kwa dharula zako.!!

Haya wanayoyafanya mama zetu na dada zetu wameyafanya kwa ndugu wa waume zao.
Mwanaume weka sawa kichwa chako.
Tafuta hela
Tunza familia yako
Usiwasahau ndugu zako(mkeo Ni rafiki tu).

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni mimi ndio nina shida au!! Maana sijaona tatizo lako kabisaaaaa. Hapo bado hamjawa mwili mmoja,mwenzio bado hajaambatana nawe yupo kwaoooo.
 
Cc Extrovert
 
Dada wanaokutetea wengi hawako ndoani, naamini wewe ndo mjuzi wa unachokikosa kutoka kwa mumeo. Nnacho kushauri fanya hivi, ktk hao mashemeji zako mtafute yule ambae jamaa ndo anafocus sana kumsaidia matatizo yake, basi nawewe shiriki hata kwa namna ndogo. Kama huwa anamlipia ada, wewe mpatie nauli nk. Fanya haya bila kuta attention kwake. Naamini atapata mrejesho wa fadhila zako kwa nduguze.

Akisha jua basi ataanza kukuuona unaipenda familia yake na milango mingine itafunguka.
Wanaume hatupendi wake zetu wachukie familia zetu. Inawezekana uwasilishaji wako ulimfanya akutafsiri huwapendi nduguze.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Ushauri wa kijinga sana. Ukiwa na familia yako your family is the priority wengine unawafanyia hisani tu. Huwezi kuacha nyumbani kwako bila kitu kisa unasaidia ndugu zako vinginevyo ungemalizana kwanza na hao ndugu zako ndo ungeanzisha familia yako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…