Nifanyeje katika hili wadau! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nifanyeje katika hili wadau!

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by buhange, Nov 23, 2011.

 1. buhange

  buhange JF-Expert Member

  #1
  Nov 23, 2011
  Joined: Oct 23, 2011
  Messages: 494
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 45
  Hey! wana-JF
  Mimi ni kijana mwadilifu ktk maswala ya kibiashara, ni mwanachuo ninaesomea maswala ya utawala wa biashara ktk moja ya chuo kikuu hap Tz.Jamani ninishauku sana,ujuzi na taaluma yangu vinisaidie ktk kujikwamua kiuchumi na niifaidishe jamii pia ila tatizo ni mtaji. Sina Fixed assets, wala Securities zozote ila nina knowledge na experience kubwa ktk Business operation,Marketing and Entrepreneurship. Naomba ushauri nitokeje! maana kukosa assets kunanifanya nishindwe kwenda ktk Banks au ktk NGOs kutafuta mikopo nafuu. Tayari nina Business Proporsal kadhaa nimeshaanda ila implementation ina fail coz of Capital
   
 2. CHASHA FARMING

  CHASHA FARMING Verified User

  #2
  Nov 23, 2011
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 6,133
  Likes Received: 2,117
  Trophy Points: 280

  mkuu hongera sana kwa kutambua umuhimu wa kujiajiri na vezuri kuanza kujipanga mapema make chuoni huko ni mahali pa kupit na maisha yako kitaa.

  Kwa kweli swala la mtaji ni gumu sana na si kwako pekee bali kwa kila mtu hata mimi vilevile. Ila ningekushauli vitu vifutatavyo
  .  cha kwanza kabisa unaweza fanya mchakato wa kuweka hiyo idea yako katika vitendo, means kusajili biashara yako na kupata legal docoment zingine- kusajili biashara yako ni moja ya hatua kubwa sana make ukimfuata mtu unawazo pekee atakuona msanii so ukiwa umeisha anza kuweka kwenye vitendo atakuona kweli unajuhudi, make hili la mawao pekee kila mtu ukimfuata atakuambia ana wazo zuri sana but amefanya nini katika kupiga hatua mbili mbele ni hakuna


  a. Cha kwanza ni kupitia hayo mawazo yako ya biashara, your idea is a primary capital, hapa unatakiwa kuwa na mawazo yakio enda shule mkuu na c wazo ambalo tiyali liko mtaani miaka 50 iliyo pita. Ingawa kwa huku bongo wa sanii ni wengi sana ukimshilikisha katika wazo zuri atakataa na ukimpa kiso tu analichukua fasta na kulifanyia kazi. Tafuta watu ambao ni very portenetial kama ndugu zako na rafiki zako

  b. Washilikishe ndugu zako na jalibu kuwaeleza kuhusu wazo lako la biashara na umuhimu wake kwao. Hapa ni katika kuangalia ni kivipi watakuunga mkono.

  C. Washilikishe hata marafiki zako hayo mawazo yako, kwa wale marafiki wenye muelekeo wa kujiajili, ukiwashilikisha mnaweza ona njia za kuunganisha nguvu zenu, hata kama kila mtu atakuwa na laki moja moja bado ni kubwa

  d. Katika mawazo yako jalibu kuanza na biashara ambayo haihitaji mtaji mkubwa sana mfano kutoa huduma( kutumia ujuzi wako wa elimu) biashara za kutoa huduma mara nyingi huanza na mtaji mdogo sana- baadae unaweza unda sbu

  e. Kama uko chuoni na unapata mkopo asilimia 100% jalibu kuserve mkuu, pesa ya loan board ukibahatika kupata 100% halafu ukaserve inatosha kabisa- mkuu haina maana kuishi maisha ya kushindana chuoni wakati unajua fika kwamba mtaani kunakusbilia na historia haitakukumbuka kwamba wewe chuoni ulikuwa unamiliki music systeam kubwa sana. Try kuserve mkuu inaweza kuwa ndo mtaji wako.

  F. Kuna taasisi zinatoaga mikopo na zingine waga zinashindanisha michanganuo mizuri na inayo shinda hutafutiwa wabia wa kuweleza nao kutoka hata nje ya nchi. Jalibu kucheki na huko. Na katika hili la kushindanisha nina ushahidi kuna wabongo wameweza kupata mtaji.
  mtaji usikukwamishe ni bora ukaanza na kile ulicho nacho usikate tamaa, anza na idea yako na mtaji utakufuata tu mkuu. Go on pls

   
 3. c

  changman JF-Expert Member

  #3
  Nov 24, 2011
  Joined: Jul 26, 2011
  Messages: 229
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Fanya haya yafuatayo:

  1. Tafuta idea. Nadhani mpaka sasa una business idea nzuri. Hata kama huna tafuta. Ukishindwa kabisa kuja na idea angalia biashara nyingine zinazofanywa na watu then jaribu kucheki if unaweza kuichukua na kui-modify na kuongezea mambo mengine.

  2. Andika business plan. Wewe unasomea biashara nadhani mpaka sasa unajua jinsi ya kuandika hiyo plan. Hiyo plan unaweza kuipeleka benki wakakupa mkopo hata kama huna asset yoyote ikiwa idea yako ni nzuri sana na wao wakaisimamia hiyo project coz ni hela zao.

  3. Tafuta patner. Matajiri wengi wameanzisha biashara zao kwa kutumia partners. Wewe una elimu na idea, ukimpata mtu mwenye hela mnachangia na kufanya kitu cha maana. Kuna watu wengi wana hela ila wanatafuta ideas nzuri. Na hapa hiyo business plan yako ndo itakapokusaidia coz investor au partner atataka kujua biashara itafanyikaje na usalama wa hela yake.

  4. Kusanya mtaji. Kama ukikosa wawekezaji kusanya hela kwa watu mbalimbali. Kopa hela kwa ndugu, jamaa na marafiki. Si lazima uanzishe biashara ya mamilioni ila unaweza kutumia pesa lidogo uliyoipata na kuanziasha biashara ambayo kwa kutumia elimu yako utaifanya ikue haraka. Tena unabahati unaanzisha biashara ukiwa na elimu yake tayari. Hela unayotumia kunyea pombe unaweza kui save kwa ajili ya investment. Utakapofanikiwa kibiashara utakunywa pombe mpaka utazichoka.

  5. Kuondoa risk ya kupoteza mtaji wako utakapoanza biashara yako, investigate na kufanya research ya maana kujua hiyo biashara unayotaka kuifanya inafanyikaje. Ijue nje ndani.

  Nadhani haya yatakusaidia.
   
 4. b

  butogwa Member

  #4
  Nov 24, 2011
  Joined: Jun 22, 2011
  Messages: 34
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Hongera sana, mimi nadhani ww una idear ya biashara sio experience,watz wengi tunaamini mtaji ni pesa na assets mm naamini ari, nguvu na malengo ndio mtaji mkubwa. Nakushauri utafute pale kwenye biashara unayoiweza ujitolee kufanyakazi kwa bidii.Hapo utapata mbinu nyingi na mpya za kibiashara coz kuna mabadliko ya kasi sana ktk biashara nyingi' ingia kwenye system kwanza kila kitu utapata humo.
   
 5. Masikini_Jeuri

  Masikini_Jeuri JF-Expert Member

  #5
  Nov 24, 2011
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 6,809
  Likes Received: 364
  Trophy Points: 180
  Namuunga mkono Butogwa tafuta nafasi ya kuapata ujuzi zaidi wa kivitendo wakati ukiendelea taratibu sanajari na ahayo maandaliazi mengine; na kwa kuanzia kama unatokea kwenye familia za kiafrika unaweza kuanza hata na kuku wa 5 tetea 4 jogoo mmoja; kuna mana ya kuwafunga kisayansi hao haoa wakakupa mtaji wa kutosha ndani ya miaka miwili hadi mitatu.............muhimu ni malengo ; na kuyafikia tekeleza mipango yako kwa vitendo.
   
 6. HAZOLE

  HAZOLE JF-Expert Member

  #6
  Nov 25, 2011
  Joined: Feb 25, 2011
  Messages: 1,331
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  pia tembelea mitandao mbalimbali ya nje inayotoa fund kwa kuandika proposal kuhusu project za kijamaa na maendeleo ya jamii(charity oriented firms).
   
 7. Jayfour_King

  Jayfour_King JF-Expert Member

  #7
  Nov 27, 2011
  Joined: Nov 15, 2009
  Messages: 1,142
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Vyovyote itakavyoelezwa suala kubwa hapa ni ugumu wa kupata capital kwa mtu anayeanza biashara kwa kweli hili ni suala gumu na hakuna namna rahisi ya kulirahisisha.
   
 8. CHASHA FARMING

  CHASHA FARMING Verified User

  #8
  Nov 28, 2011
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 6,133
  Likes Received: 2,117
  Trophy Points: 280
  mkuu tatizo letu c c tumeishia kwenye mawazo tu, kila mtu ukimuuliza atakumbia ana wazo lake zuri.
  - ni vigumu kupata sapoti ukiwa umeishia kwenye wazo tu.
  - fanya juhudi kuendeleza wazo lako hilo jaribu kulisogeza mbele kidogo,
  - kinacho takiwa ni mtu akukute umeanza kupiga hatua moja mbele na hilo wazo lako.
  - hapa c zungumzii kuandika mchanganuo wa wazo lako pekee.
  - so ukiishia kwenye wazo ukaanza kutafuta sapoti ni vigumu sana kupata sapoti
  - lazima uulizwe wewe umjitahidi mpaka wapi? Onyesha kwamba umejitahidi sana but nguvu zako zimeishia hapo.

  -
  usimwambie mtu kwamba nguvu zako ziliishia kwenye wazo pekee, hapo atakuona msanii.


  KiLicho baki sasa ni kufanya juhudi za one step mbele na hayo mawazo yetu na si kila mtu kuishia kusema nina wazo zuri, wazo pekee hujafanya chochote, hujaonyesha juhudi zozote.

  -TATIZO CC TUNAPENDA TUFANYE BIASHARA YA KUTOKA HARAKA SANA, ILA UKIAMBIWA KUNA MTU ALIANZA BIASHARA NA MTAJI WA SH 700 BUT LEO HII NI MILIONEA HUTAAMINI.

  -
  ANZA BIASHARA NA KILE ULICHO NACHO WEWE, NA SI KILE WALICHO NACHO WENZAKO , UNA SH 100000, ANZA NAYO, UNA MILIONI MOJA ANZA NA BUSINESS YA MILIONI MOJA,

  - MTU UNAKUTA UWEZO WAKE NI KUPATA LAKI 3 LAKINI ANAPIGA MAHESABU YA BIASHARA YA MILIONI 200,

  - SO ANZA NA MTAJI WAKO MWENYEWE , UZA BADHI YA VITU VYAKO FANYA MTAJI,
  -UZA MUSIC SYSTEAM YAKO,
  - UZA HATA KITANDA LALA SAKAFUNU,
  -UZA FRDGE LAKO BADALA YA FRDGE LAKO KUISHIA KUTUNZA MAJI YA KUNYWA PEKEE WAKATI YA WENGINE YANALEMEWA NA VITU.
  - SIMAMISHA STAREHE ZOTE, ACHA KUCHANGIA HARUSI, SEND OFF, KITCHEN PARTY NA BARIKIO
  - PUNGUZA KUPIGA SIMU ZISIZO KUWA NA MAANA, ETI UTAKUTA WABONGO KUTWA NZIMA KUPIGIANA SIMU NA HAMNA CHA MAANA WANACHO ELEZANA ZAIDI YA UMBEA TU'
  NA ZANI KUNA ILE EQUATION OF WEALTH NILIIPOST HAPA ONE DAY SO UKITILIA MAANANI EQUATION OF WEALTH HAKIKA HUWEZI KOSA MTAJI.

  -WAKUU UTAKUTA MTU ANALALAMIKA HANA MTAJI LAKINI ANAMILIKI VITU VYA ANASA CHUNGU NZIMA.

  BIASHARA NYINGI DUNIANI HUANZA NA MTAJI WA MTU BINAFISI NA BAADAE NDO MTU ANAANGALIA KUKOPA BENKI NA KWINGINEKO.

  - VI
  NGINEVYO TUTABAKIA KUSEMA A NINA WAZO ZURI, KILA MTU ANA WAZO ZURI, HAMNA MWENYE WAZO BAYA LA BIASHARA, ILA JIULIZE UKIKAA NA HILO WAZO LAKO MIAKA NENDA RUDI UNAFAIDIKA VIPI?

   
 9. A

  Arkad Member

  #9
  Nov 29, 2011
  Joined: Jan 16, 2011
  Messages: 25
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Most books prove that the term Capital comes from greek words which means BRAIN. Ideas yako inaweza ikawa super1 bt unatakiwa uwe na vi subideas vitakavyokufikisha ktk hiyo idea kubwa..Ushauri anza na biashara ambazo hazihitaji mtaji au zinahusisha mtaji mdogo ili kukusanya mtaji kukufikisha ktk lengo kuu..Mfano Udalali,Usimamizi wa kamari (legal 1), n.k

  Marafiki na ndugu kama unao hawa wanaweza kukusaidia kwa kiasi kikubwa . WATUMIE. Kila la heri.

  TELL THE WORLD YOU INTEND TO DO BUT FIRST SHOW IT..
   
 10. buhange

  buhange JF-Expert Member

  #10
  Nov 29, 2011
  Joined: Oct 23, 2011
  Messages: 494
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 45
  Asante kaka! nipo makini na kila kinachowekwa hapa, mchango wenu ni wa dhamani sana ktk kukamilisha ndoto zangu. Pamoja brothers and sisters
   
 11. P

  Prime Dynamics JF-Expert Member

  #11
  Nov 29, 2011
  Joined: Dec 30, 2010
  Messages: 524
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  Mkuu, you can only become a successful business owner once you have a business to practice on.
   
Loading...