Nifanye nini nipate ajira 2023

Nifanye nini nipate ajira 2023

Vonnies

New Member
Joined
Feb 27, 2023
Posts
4
Reaction score
9
Nimemaliza chuo tangu 2019, nimekuwa niki apply kazi kupitia ajira leo, na sehemu mbali mbali zinazotangazwa, ila hadi sasa ivi sijabahatika kuajiriwa.

Sasa sijui ni hii course niliyosomea, au ni nini? Nimesomea International Relations, natamani hata nifanye biashara ili niweze kujikwamua shida mtaji nao ni swala gumu,maana familia yangu hatuna uwezo kivile, na nilisomeshwa ili niwasaidie wazazi, ila ndio niko nyumban.

Mwaka huu mwenye kunisaidia hata kwa mawazo tuu ili nipate ajira nitashukuru sana
 
Hiyo program uliyosomea inahitaji koneksheni kuliko hata zile za Jeshi Kwa waliojitolea. Kuna ndugu yangu kamaliza hiyo international relations tangu 2015 mpaka Sasa anasugua benchi tu. Ameamua kuomba kufundisha Somo la kiingereza na anaishi kupitia taaluma ya ualimu sekta binafsi anayoiponda mpwayungu village

Nini ufanye! Tafuta fani yoyote nje ya taaluma Yako Ili upate ajira. Mfano ualimu wa GS au Civics Kwa sekondari au ualimu wa shule za msingi za binafsi. Nje ya hapo basi tafuta vibarua vya kujitolea na kulipwa laki Kwa mwezi.

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Nimemaliza chuo tangu 2019, nimekuwa niki apply kazi kupitia ajira leo, na sehemu mbali mbali zinazotangazwa, ila hadi sasa ivi sijabahatika kuajiriwa.

Sasa sijui ni hii course niliyosomea, au ni nini? Nimesomea International Relations, natamani hata nifanye biashara ili niweze kujikwamua shida mtaji nao ni swala gumu,maana familia yangu hatuna uwezo kivile, na nilisomeshwa ili niwasaidie wazazi, ila ndio niko nyumban.

Mwaka huu mwenye kunisaidia hata kwa mawazo tuu ili nipate ajira nitashukuru sana
Usikate tamaa, there is hope
May Almighty God see you through

Unataka kufanya biashara gani
Na unahisi unahitaji mtaji kiasi gani kuanza?
 
Hiyo program uliyosomea inahitaji koneksheni kuliko hata zile za Jeshi Kwa waliojifolea. Kuna ndugu yangu kamaliza hiyo international relations tangu 2015 mpaka Sasa anasugua benchi tu. Ameamua kuomba kufundisha Somo la kiingereza na anaishi kupitia taaluma ya ualimu sekta binafsi anayoiponda mpwayungu village

Nini ufanye! Tafuta fani yoyote nje ya taaluma Yako Ili upate ajira. Mfano ualimu wa GS au Civics Kwa sekondari au ualimu wa shule za msingi za binafsi. Nje ya hapo basi tafuta vibarua vya kujitolea na kulipwa laki Kwa mwezi.

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app

Nashukuru sana
 
Kuna jambo ambalo linawatesa wahitimu wengi nalo ni kukosa focus. Unapokosa focus unalenga shebaha nyingi. Unapolenga shebaha nyingi unakosa kote.

Kazi zinazofaa kwa sasa kwa fani yako ni kazi za NGOs. Nina uhakika kuanzia 2019 ungeweka kipaumbele kuwa unapambania NGO tano tu ambazo umezichagua na kuhakikisha unajiweka karibu nazo kufuatilia mambo yao, projects zao, kwenda mara kwa mara kuulizia kazi hata za kujitolea. Hii ingekufanya uwe attached to them.

The more you attach yourself to an institution the more you get closer na wataku consider tu zinapotoka nafasi.

Kuna jamaa alimaliza 2019 IT, nikamwambia afanye juu chini aji attach kwa mzee mmoja ana cheo kikubwa jeshini. Dogo alienda home kwa yule mzee akaomba amtunzie bustani. Akaonesha tabia njema sana pale mtaani. Akawa mwalimu wa tuition wa watoto wa mzee.

Dogo akaambiwa amfundishe computer binti wa mzee. Binti wa miaka 17. Binti nae hot akawa anamtega dogo. Sema dogo alicheza kistaarabu sana akawa anampa promise binti kuwa akimaliza shule watakuwa wote asome kwa bidii. Angejichanganya ale abebeshe mimba angekuwa jela.

Akaji attach akapendwa sana na ile familia. Akawa hakosi pesa za bundle, route za shopping yupo, misosi full, mzee simu akiichoka anampa dogo. Dogo akawa kama mwana familia. Kumbuka kuwa dogo kilichombeba ni tabia mana wazee walotumikia muda mrefu na wenye vyeo jeshini wanavutiwa sana na vijana waaminifu, wanaojitambua na wenye adabu.

Dogo akawa anatumwa kwenda mpaka site kusimamia mzee alikuwa anajenga Kigamboni nyumba kubwa ya familia. Dogo alikuwa akitumwa hata ikibaki 500 anarudisha mzee mwenyewe ndo anamwambia chukua nawewe hiyo. Madogo wakirudi shule anawatengenezea chips chap wanakula. Ilikuwa dogo asipoonekana home kwa mzee siku mbili watoto wanakiamsha anko yupo wapi dadii tunamtaka anko.

Mzee akamuunganishia kazi TARURA 2021. Mpaka leo hii jamaa amemuweka yule mzee kuwa kama mzazi wake na anawachukulia watoto wa yule mzee kama wadogo zake. Kabinti nako kapo chuo dogo ndo anajisevia skuizi na wanapanga kuoana.

THEME: Kwenye maisha connection hutafutwa hazijileti kirahisi. Huenda dogo alikuwa na nyota njema pia ila ukiji attach kwa watu wazito hata kama utamuoshea gari kuna kitu ukaonesha cha tofauti atakupenda na kukufungulia fursa.
 
Nimemaliza chuo tangu 2019, nimekuwa niki apply kazi kupitia ajira leo, na sehemu mbali mbali zinazotangazwa, ila hadi sasa ivi sijabahatika kuajiriwa.

Sasa sijui ni hii course niliyosomea, au ni nini? Nimesomea International Relations, natamani hata nifanye biashara ili niweze kujikwamua shida mtaji nao ni swala gumu,maana familia yangu hatuna uwezo kivile, na nilisomeshwa ili niwasaidie wazazi, ila ndio niko nyumban.

Mwaka huu mwenye kunisaidia hata kwa mawazo tuu ili nipate ajira nitashukuru sana
Inasikitisha ,inaumiza ,inachoma sana! Mwenye kumsaidia huyu ndugu kupata shughuli ya kufanya afanye hivyo
 
Back
Top Bottom