Nifanye Nini Ili Nimsahau!!

kaeso

JF-Expert Member
Mar 22, 2011
551
96
Alikuwa ni mpenzi ambaye tulidumu kwa muda wa mwaka mmoja na nusu. Niligundua kanificha mambo mengi muda wote niliokuwa naye. Aliwahi zaa mtoto akafariki, ila mimi alinidanganya kuwa ana mtoto na anaishi na dada yake. Pia nilikuja kugundua baadae kuwa anatembea na mume wa mtu, hii ndio ilikuwa sababu kubwa ya kumuacha. Tatizo nililo nalo hivi sasa ikiwa ni miezi sita tangu tuachane, hanitoki kabisa mawazoni. Naombeni ushauri ni namna gani nitaweza kumtoa mawazoni ili niendelee na maisha yangu?
 
Kuwa busy na ishu zako za maana mkuu pia jichanganye na rafikizo, usikubali kuwa idle muda mrefu itakusaidia!!!
Asante sana inabidi nifanye hivyo maana naona nikiwa bize namsahau japo kwa muda..
 
Dawa ya kumtoa mawazoni ni kupata mpenzi mpya ambaye mtashibana na kupendana kuliko huyo wa kwanza
 
Kumbe wampenda? Kwa nini sasa ulimuacha badala ya kumshauri, kumsikiliza na kumsaidia ili akae katikati mstari unaofaa?
Upendo gani huo sasa? Hakuna asiye na makosa, na hayo ni moja ya makosa yanayofanywa na wanadamu.

Kwa nini usikae naye ukamwelimisha na kumuonya? Na huta msahau manake umekuwa mbinafsi na nakuhesabu makosa yake na kutoa hukumu as if wewe huna makosa.

Ila ungekuwa wewe ungependa USAMEHEWE :(
 
Tatizo ni kwamba ulimuamini na kumpenda kupitiliza.Utamsahau taratibu ila ukipata mbadala utamsahau zaidi.
 
Kwanza kubali matokeo kuwa huyo mwanamke ni muongo,na kama ameweza kukudanganya vitu vya msingi katika kipindi cha uchumba jua kwamba hata mngeingia katika hatua ya ndoa angezidi kukudanganya....la Pili, Move on angalia mbele zaidi..wanawake wapo teeeleee...angaza,chunguza,anza maisha mapya..mfute yule kichwani...mfikirie kama tatizo..ukishindwa kufanya hayo utaishia kuwa msaka ngono mwisho wa siku magonjwa... Songa mbele Bro..
 
Hiyo ni kawaida mkuu kutokana na mazoea. Wapo watu wanakataa kuhama mahali walipokaa kwa muda mrefu kwa sababu ya mazoea, na mara wanapohamia sehemu nyingine na kuadapt mazingira ya mahali huona tena huko ni kuzuri kuliko sehemu nyingine dunia. Kuwa busy na mambo yako, nenda kwenye viwanja vya michezo ili uweze kupata usingizi usiku kwani najua muda wa kuwa idle na kufikiria sana vitu hivyo huwa ni usiku.
 
Khaaa ! Yawezekan ulikuwa humpi vitu vitamu ndiyo maana alikuwa anachakachuliwe na wenzako. Na pia yawezekan siyo mwanamme mmoja anaye mjua ! Pole ndugu yangu kama huwez kumsahau jaribu kumrudia plz.
 
Alikuwa ni mpenzi ambaye tulidumu kwa muda wa mwaka mmoja na nusu. Niligundua kanificha mambo mengi muda wote niliokuwa naye. Aliwahi zaa mtoto akafariki, ila mimi alinidanganya kuwa ana mtoto na anaishi na dada yake. Pia nilikuja kugundua baadae kuwa anatembea na mume wa mtu, hii ndio ilikuwa sababu kubwa ya kumuacha. Tatizo nililo nalo hivi sasa ikiwa ni miezi sita tangu tuachane, hanitoki kabisa mawazoni. Naombeni ushauri ni namna gani nitaweza kumtoa mawazoni ili niendelee na maisha yangu?

kumuwaza tu, mbona kawaida sana!! Tafuta mtu mwingine wa kukudanganya. Maana kudanganyana ndio mapenzi ya kisasa.
 
Alikuwa ni mpenzi ambaye tulidumu kwa muda wa mwaka mmoja na nusu. Niligundua kanificha mambo mengi muda wote niliokuwa naye. Aliwahi zaa mtoto akafariki, ila mimi alinidanganya kuwa ana mtoto na anaishi na dada yake. Pia nilikuja kugundua baadae kuwa anatembea na mume wa mtu, hii ndio ilikuwa sababu kubwa ya kumuacha. Tatizo nililo nalo hivi sasa ikiwa ni miezi sita tangu tuachane, hanitoki kabisa mawazoni. Naombeni ushauri ni namna gani nitaweza kumtoa mawazoni ili niendelee na maisha yangu?
tafuta mtu mwingine wa kukudanganya, vikikushinda rudi uombe ushauri.
Tawire
 
Haya mambo sijui mwalimu wake yuko wapi yanaumiza sana watu!! pole sana mkuu utasahau2!!
 
Pole sana mkuu,
Mapenz ndivyo yalivyo hasa km ulipenda kweli,
Jikeep busy na marafiki,na ukiamin kuwa kuachana naye umeepuka mengi,
Mwombe mungu uweze kupata mwingine mkweli hakika utasahu na yote yatabaki historia tu,
Mapenz hayana mwenyewe hata matajiri yanawatoa machozi!!!
 
Hakuna kisichopita, tafuta demu mwingine maisha yanaendelea. Mawazo yakizidi kula monde, weka heshima bar asubuhi utakuwa anawaza kupunguza hangover na cio yeye mpaka kitaeleweka
 
alikuwa ni mpenzi ambaye tulidumu kwa muda wa mwaka mmoja na nusu. Niligundua kanificha mambo mengi muda wote niliokuwa naye. Aliwahi zaa mtoto akafariki, ila mimi alinidanganya kuwa ana mtoto na anaishi na dada yake. Pia nilikuja kugundua baadae kuwa anatembea na mume wa mtu, hii ndio ilikuwa sababu kubwa ya kumuacha. Tatizo nililo nalo hivi sasa ikiwa ni miezi sita tangu tuachane, hanitoki kabisa mawazoni. Naombeni ushauri ni namna gani nitaweza kumtoa mawazoni ili niendelee na maisha yangu?

unatakiwa umdharau na udharau kitendo alichokifanya then utaweza kumsahau
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom