Kwan we ulipompokea una lengo gani nae na hali unajua tayari ni mke wa MTU???
Na amekimbilia kwako nawe ukampokea kwani we ni mjumbe wa nyumba kumi??au mzazi wake?
Kama ulizaa nae na hukumuoa badala yake ukagomboa mtoto kwa nini kama na yeye anakuhusu usimgomboe awe mkeo??
Na we we mkeo kaenda kwao na watoto kwa sbb gani?
Inaonesha we we na huyo mwanamke mlipanga njama tu ya we we kufukuza mkeo na yeye kumtoroka mumewe kwa visingizio vya uongo mana hata huyo mwanamke anajua una mke na watoto kwa nini akimbilie kwako wakati mkeo hayupo???kwani kwenye ndoa watu huwa hawagombani na wake zao wakaenda kwao kwa muda na baadae hasira zikiisha wakarudi??
Halafu unasema walioana bila mahari na we we ulioa bila mahari,mbona kauli yako kama inataka kulazimisha uhalali wa we we kumpokea huyo mke wa MTU wakati nawe ni mume wa MTU!!
kwani we hujui kukaa na mwanamke au mwanaume kwa muda Fulani ndani ya nyumba moja na watu wakajua,hata kama hamkutoleana mahari au kufunga ndoa kisheria mnakuwa mume na mke hujui hilo???
Nahitimisha kwa kusema huyo ni make wa MTU na we we ni mume wa MTU,hivyo hakuna cha kunywa sumu wala nini rudisha mke wa mwenzio,usione vyang'ara vimegharamiwa!!!
kama ulikuwa unampenda toka mwanzo ungemchukua enzi hizo ulipomzalisha,sio mpaka wenzio wampendezeshe ndo ujifanye kurudisha majeshi,shauri zako UTALIWA KWELI watu wana uchungu na Mali Zao!!!