Nifanyaje mwanangu meno yasibadilike kutokana na maji?

SAUTI YAKO

JF-Expert Member
Jan 25, 2014
2,944
2,032
Niko katika mkoa ambayo wakazi wake meno yamebadilika rangi kutokana na maji wanayokunywa.

Mimi nilihamia huku nilipo mwaka jana na mwanangu mwenye umri wa mwaka mmoja hajazaliwa huku alikuja hapa nilipo akiwa tayari ana mwaka mmoja.

Lakini tangu afike nimekuwa nikimpa maji haya ya bomba wanayokunywa wenyeji, je wakuu siku za usonI haiwezi kufanya meno yake yabadili rangi.

Naomben ushauri maana mkoa nilipo nipo kwa muda wamiaka 5 tu natarajia baada ya kipindi hicho kupita nihame sitaki mwanangu tutapohama awe hivyo, je niwe namnulia maij ya chupa au nifanyaje.
 
Mkuu nunua carton ya maji ndogo hata elfu 5 haiishi kwenye maduka ya juml,a hakikisha mtoto anatumia maji hayo tu.

Kama unamuacha nyumbani na housegirl hapo ndo kuna changamoto ya kuhakikisha anampa mtoto hayo maji na si mengine.

Mi nipo kwenye mkoa ambao hakuna tatizo la meno kuharibiwa na maji ya kunywa ila kwa ajili ya kuepuka matatizo yanayoletwa na kunywa maji yasiochemshwa huwa nanunua carton hizo kwa ajili ya watoto wangu na kila asubuhi kama anaenda shule lazima aende na maji ndogo.

Imesaidia saidia kuepuka magonjwa ya matumbo kwa watoto wangu...
 
Mkuu nunua carton ya maji ndogo hata elfu 5 haiishi kwenye maduka ya juml,a hakikisha mtoto anatumia maji hayo tu...Kama unamuacha nyumbani na housegirl hapo ndo kuna changamoto ya kuhakikisha anampa mtoto hayo maji na si mengine...Mi nipo kwenye mkoa ambao hakuna tatizo la meno kuharibiwa na maji ya kunywa ila kwa ajili ya kuepuka matatizo yanayoletwa na kunywa maji yasiochemshwa huwa nanunua carton hizo kwa ajili ya watoto wangu na kila asubuhi kama anaenda shule lazima aende na maji ndogo....Imesaidia saidia kuepuka magonjwa ya matumbo kwa watoto wangu...
Asante kwa ushaur ntautendea kazi
 
Niko katika mkoa ambayo wakazi wake meno yamebadilika rangi kutokana na maji wanayokunywa.

Mimi nilihamia huku nilipo mwaka jana na mwanangu mwenye umri wa mwaka mmoja hajazaliwa huku alikuja hapa nilipo akiwa tayari ana mwaka mmoja.

Lakini tangu afike nimekuwa nikimpa maji haya ya bomba wanayokunywa wenyeji, je wakuu siku za usonI haiwezi kufanya meno yake yabadili rangi.

Naomben ushauri maana mkoa nilipo nipo kwa muda wamiaka 5 tu natarajia baada ya kipindi hicho kupita nihame sitaki mwanangu tutapohama awe hivyo, je niwe namnulia maij ya chupa au nifanyaje.

Mkuu SAUTI YAKO , napenda kuongezea kidogo katika jibu la manuu kama ifuatavyo: Meno kubadilika rangi kutokana na maji kitaalamu inaitwa Fluorosis, hii ni hali inayotokea wakati madini ya fluoride yanapozidi katika maji kuliko kile kiwango kinachotakiwa hasa hasa kwa watoto chini ya miaka 6 ambapo ndipo meno yale ya muda na hata ya kudumu huwa yanaanza kuota. Kuzuia shida hii ni kutumia maji yenye viwango sawa vya madini ikiwemo pia fluoride. Ni rahisi zaidi kuepukana na shida hii kama utahakikisha mtoto wako anapata maji yaliyo salama, kama alivyosema mkuu manuu unaweza kabisa kuwa una nunua maji yanayoaminika na unahakikisha mtoto wako anatumia maji hayo. Maji ya bomba ya baadhi ya maeneo hapa nchini yana fluoride nyingi kupita kiasi!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom