wa hapahapa
JF-Expert Member
- Aug 22, 2012
- 7,460
- 4,404
Jamani hii mifuko ya huduma kwa watumishi inakera sana hasa huu wa bima,unakwenda kutibiwa unaambiwa dawa zimekwisha huende ukanunue kwenye maduka ya dawa lakini kila mwezi nachangia.kwa kweli kama kuna mbinu za kujinasua mimi nitakuwa wa kwanza
Tatizo kubwa hasa kwa watumishi ni kuwa
hakuna hiari kujiunga bali ni lazima maana
viongozi hasa wa idara hunufaika mno.
Utata unakuja kwenye huduma kuwa mbovu
suruhu acha kazi
naamini wapo wengi sana waliochoshwa na shirika hili na wanania kujitoa uanachama, tatizo ni haki/njia ya kujitoa bado hamna taratibu zinazoeleweka.
pia inakera sana pale unapofika ktk ofisi zao zilizopo Dar kwa lengo la kuongeza au kufanya mabadiliko yaani utazungushwa sana ili mradi utoe chochote...,
naamini akili zako zina shida kdg..... hapa ishu sio kuacha kazi, ni haki/hiari ya mwanachama wa bima iko wapi ??,
si suruhu kwa mwanachama kuacha kazi kwaajiri ya NHIF.... hatakuwa CHIZi
shida watz wamezoea kusukumwa/kuburuzwa kama ng'ombe na wenye kufuata mkumbo wa maslahi ya wachache kama bendera ifuatavyo upepo.
naamini wapo wengi sana waliochoshwa na shirika hili na wanania kujitoa uanachama, tatizo ni haki/njia ya kujitoa bado hamna taratibu zinazoeleweka.
pia inakera sana pale unapofika ktk ofisi zao zilizopo Dar kwa lengo la kuongeza au kufanya mabadiliko yaani utazungushwa sana ili mradi utoe chochote...,
kwa sheria namba 8 ya mwaka 1999 CAP 395 R.E 2002,
Mtumishi yoyote wa serikali kwa mujibu wa sheria hii ni mwanachama wa mfuko wa taifa wa bima ya afya. uanachama ni lazima kwa watu hawa. sheria ilipitishwa na bunge la jamuhuri la muungano wa tanzania. bunge ni uwakilishi wa wananchi hivyo mimi na wewe tuliwakilishwa na wabunge wetu wakapitisha sheria hii.
hivyo basi kigezo cha kwanza kabisa cha wewe kuwa mwanachama ni wewe mtumishi wa serikali kama hutaki yafuatayo unatakiwa kufwata
1. kama mtumishi wa serikali acha kazi au jiajiri mwenyewe au ajiriwa katika mashirika binafsi uweze kuchagua bima ya afya unayoitaka.
2. mwambie mbunge wako apeleke hoja binafsi bungeni kutoa sheria hii. ikijadiliwa na kuonekana inafaa kutolewa au kurekebishwa na kuweka uhiari basi itafanyika kuwa hivyo.
Mkuu huduma zile hazitolewi bure si unachanga every month?kwa mantiki hii
1. hakuna haki/fao la kupata mwanachama hakihama ktk huduma za taasisi hiyo ??
2. na je bunge liliunda taasisi hiyo na kuipa madaraka ya kunyanyasa haki za wafanyakazi pasipo ridhaa zao kwa kuwasajiri bila taarifa, kuwanyima haki ya kuhamia ktk kampuni binafsi, pamoja na kutoridhisha kwa huduma za Afya zinazotolewa bure.
mkuu wa hapahapa pole kwa masaibu yaliyokupata,sijui kama wewe ni mwajiriwa wa serikali au taasisi binafsi,kwa sababu kama ni mwajiriwa wa serikali huna uchaguzi,kwa baadhi ya taasisi binafsi mwajiri na mwajiriwa mnaweza kukubaliana kujiunga ama la,na kwa uzoefu wangu tatizo kubwa la NHIF ni kung'ang'aniza watoa huduma wafuate bei zao ambazo mara nyingi huwa zipo chini sana ukilinganisha na bei za soko jambo linalopelekea wanachama wa NHIF kunyanyaswa na kubaguliwa.
Mkuu huduma zile hazitolewi bure si unachanga every month?
asante kaka umenisaidia,maana yeye kaomba msaada sasa watu tunamsaidia ,yeye anatutia vidole vya macho wakati yeye ndio mwenye shida,na huu ni ushauri tu mshikaji usijenge chuki.kwa sheria namba 8 ya mwaka 1999 CAP 395 R.E 2002,
Mtumishi yoyote wa serikali kwa mujibu wa sheria hii ni mwanachama wa mfuko wa taifa wa bima ya afya. uanachama ni lazima kwa watu hawa. sheria ilipitishwa na bunge la jamuhuri la muungano wa tanzania. bunge ni uwakilishi wa wananchi hivyo mimi na wewe tuliwakilishwa na wabunge wetu wakapitisha sheria hii.
hivyo basi kigezo cha kwanza kabisa cha wewe kuwa mwanachama ni wewe mtumishi wa serikali kama hutaki yafuatayo unatakiwa kufwata
1. kama mtumishi wa serikali acha kazi au jiajiri mwenyewe au ajiriwa katika mashirika binafsi uweze kuchagua bima ya afya unayoitaka.
2. mwambie mbunge wako apeleke hoja binafsi bungeni kutoa sheria hii. ikijadiliwa na kuonekana inafaa kutolewa au kurekebishwa na kuweka uhiari basi itafanyika kuwa hivyo.
kifupi, mi naona taasisi hii Efficiency yake ni ndogo sana na wanaonufaika ni wachache
sio wachangiaji wote wanapata huduma na kuridhika nayo ktk taasisi hii.
Wafanyakazi wa serikali nao wanabaguliwa. Mimi nafanya kazi katika shirika la uma (SU) na nililazimishwa kujiunga na NHIF. Lakini nina marafiki kadhaa wanaofanya BoT, wameniambia wafanyakazi wa pale wamekatiwa bima ya AAR.
Cha kushangaza hii bima ya afya kuna dawa ambazo ni lazima mgonjwa alipie, eti hospitali zote zimeandikiwa dawa zitakazolipiwa na NHIF. Kwa mfano dawa za malaria ni mseto, lakini cotexin hailipiwi. yaani itakubidi unywe dawa ambazo hutumii, kisa umekata bima ya afya.
upo sahihi kabisa mkuu wa hapahapa,ufanisi wa NHIF upo chini sana,na kwa bahati mbaya hakuna kiongozi yeyote anayejali,walichofanya hawa viongozi wetu ni kuanzisha card maalum kwa ajili yao na wategemezi wao (NHIF GREEN CARDS) ambazo kimsingi zionawatofautisha wao na wanachama wengine wa NHIF kwa sababu kwa card zao wanapata huduma katika hospitali bora kabisa za binafsi jambo ambalo mimi na wewe hatutaweza kutibiwa!
sisi wa mijini tuna unafuu mkubwa sana maana angalau unaweza kuchagua kituo chenye unafuu,wenzetu hawana uchaguzi huo,wanalazimika kupokea huduma mbovu zilizopo karibu,na pia hata wakipewa fomu maalum ya NHIF ya kwenda kuchukua dawa wanalazimika kusafiri umbali mrefu kuzifuata pharmacy zinazopokea prescription za NHIF na wao pia wanakunyima dawa kwa sababu bei ya NHIF haiwalipi.