GoodluckyGodlisten2
Member
- Jan 24, 2017
- 10
- 2
Habari zenu ndugu zangu nimeamua kuja na Id mpya kulingana na unyeti wa swala langu, Natumai kuwa humu kuna watu wazima na walionizidi mawazo ndo maana nikaja kuomba msaada wa mawazo kwenu .Iko hivi mwaka 2012 nilifunga ndoa ya kimila huko shinyanga ila binti ni muha japo mimi ni msukuma, kutokana na mimi kazi zangu zilikuwa dar nikaamua kuja nae dar ili tuish pmj, alipofika alibeba ujauzito vitimbi vikaanzia hapo ila nikajipa moyo nikiamin kuwa ujauzito ndo sabb. Vitimbi viliendelea licha ya kujifungua nikashindwa kuvumilia nikamrudisha kwao sabb ilifikia kipindi nyumba nikaiona kama jehanamu,alikaa kwao kwa muda wa miaka mitatu kwao akaniomb msamaha na kukili kuwa hatorudia ujeuri wake. Nikamfuata nikaja nae dar ila vituko ndo vikawa maradufu ya mwanzo nikashindwa kuachana nae sabb nilijua huenda atabadilika,akapata ujauzito alivyoenda kujifungua likanijia wazo kuwa nipange nyumba mbili ili akirudi nimfikishie sehemu nyingine na mm niishi sehemu nyingne na sehem niliyokuw nimepanga nikahama ili asijue makazi yangu mapya kusudi nimpe mahitaji yake yote akiwa kwake na mm nikiwa kwangu.. Alivyotoka kujifungua alikuta nimempangia nyumba nzima na kila kitu nimeweka,, cha kushangaza hataki kukaa pekee yake anadai anataka kuishi ninapoishi na katishia kama nikikataa ataondoka aniachie watoto wote wa kwanza miaka minne na wa pili ana miezi miwili. Hapa niko njia natamani Kuendelea kuishi nae ili niwe karbu na watoto wangu ila nikikumbuka jeuri yake na na kashifa zake kwangu mwili unapata ganzi. Nikifikilia napo kumuacha huko nilikompangia nyumba nimhudumie nikiwa siishi nae naona kama nawatesa watoto kwa kukosa malezi yangu japo wote tupo dar.. Naombeni ushauri nikubali kuishi nae au niendelee kumhudumia tukiwa hatuishi pamoja?? Naombeni ushauri wenu maana niko njia Panda.