Niende au nisiende?

yello masai

JF-Expert Member
Joined
Jan 8, 2016
Posts
3,917
Reaction score
4,170
Ni hivi: Nimekuwa na matatizo binafsi yanayonisumbua. Sasa mchumba wangu kanishawishi anipeleke kwa mganga (ustaadh) kwamba ana uhakika pale ndo utakuwa mwisho wa matatizo yangu. Huyo mganga wanafahamiana sababu alishawahi kumtibu.
Sasa najiuliza, niende huko kweli?? Au ndo naenda kutengenezwa nipende milele na kukalishwa sijui wanaita.

NB: Nilishaenda nikatanguliza kiasi flani cha pesa lakini hakuna kazi iliyofanyika kutokana na ubize uliokuwepo, hivyo alituahidi turudi siku mbili baadae. Na nilipofika nyumbani ndo nikaijiwa na hili swali la niende au nisiende? Na je nisipoenda nimkwepe vipi huyu mchumba wangu ili asijue kama nimekwepa na tuendelee vizuri.
Niko njia panda wadau.
 
Kwa ushauri wangu na uzoefu wangu katika mambo ya ndumba nakushauri usiende, ukikubali kwenda unaenda kutengeneza maagano ambayo hutaweza kuyatengua
 
Kwa ushauri wangu na uzoefu wangu katika mambo ya ndumba nakushauri usiende, ukikubali kwenda unaenda kutengeneza maagano ambayo hutaweza kuyatengua
Kuna maelezo nimeongeza kidogo mkuu. Haikuwa complete, nitashukuru ukinishauri zaidi
 
Tawire.....

Lete kuku wa kijani na machozi ya samaki nikutibu humu humu jamvini kwa njia ya PM...
 
Reactions: waj
Mi nakusihi sana tafadhari NENDA.
 
Eneo la Mshana hili! fuata ushauri wake.Binadamu umeumbwa na Mungu unaenda kumwabudu mganga wa kienyeji na kazi za mikono yake.sio tu utaingia kwenye maagano bali utajichumia laana kwa Mwenyezi Mungu.
 

Labda nkuulize we unaamini katika haya mambo ya uganga ? Kwanini hukufikiria kwenda Kanisani au Msikitini kuapata utatuzi wa shida yako. Angalia usijepotea kama hutaki mambo haya ambayo mchumba wako anaonekana ni mzoefu temana naye fasta na usitie mguu tena.
 
Kwa ushauri wangu na uzoefu wangu katika mambo ya ndumba nakushauri usiende, ukikubali kwenda unaenda kutengeneza maagano ambayo hutaweza kuyatengua
Samahani mshana kwa usumbufu. Nikuulize tena. Hivi vipi kwa ustadh ambaye anatibia kwa dua na nyota. Sio wale wapiga lamri. Anaweza akafanya kitu kibaya? Au vitu vya kuepuka ili uwe salama? Mfano kuepuka kuchukua baadhi ya sehemu zako za mwili kama kucha au kukupa dawa uoge.
Naomba unisaidie hapo kama nimeeleweka mkuu
mshana jr
 
Mwanzo sikuamini kabisa katika mambo haya. Lakini si unajua ukiwa na shida unatafuta sehemu yoyote ya kuponea. Lakini huyu sio wale wa tunguli na wapiga ramli. Ni ustadh anatumia quran lakini alichosema ni kwamba napaswa nisomewe na nisafishwe mwili na niweke ubani kwa mkono wangu. Nasubiri unishauri zaidi hapo mkuu
 
amtegemeaye mwanadam na kumfanya kinga yake...amelaaniwa
 
Naomba hili Nisikujibu hapa linagusa imani za wengine, na Sitaki kuwapa nafasi wachafuzi wa Post
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…