Nielimisheni wanajf! Tafadhalini sana

Nielimisheni wanajf! Tafadhalini sana

king khalfan

Member
Joined
Feb 5, 2013
Posts
70
Reaction score
21
Habari zenu!
Nina maswali machache juu ya Rais J. M Kikwete yanayonisumbua ambayo kwa mtazamo wangu nahitaji kuelimishwa zaidi:
1. Ni kwa nini Rais anasemwa ni mdini? Nini maana ya mtu mdini? Dalili zake ni zipi?
2. Kama ni kweli Rais ni mdini, je hii ni kutokana na yeye binafsi ana hulka ya udini au ni sera za chama kilichomweka madarakani?
3. Na kama ni mdini anapendelea dini gani? Kwa sababu si Waislam wala Wakristo Wote wanalalamika anapendelea dini mojawapo?
4. Kwa nn kabla ya utawala huu suala la udini ktk nchi yetu halikuwa lenye kusikika sana kama sasa ambapo limejitokeza hadi ktk matukio mbalimbali km vl padri kuuwawa, sheikh kumwagiwa tindikali, misikiti na makanisa kuchomwa moto, kila dini kugombania kuchinja wanyama n.k
5. Taratibu au mifumo ipi ilitumiwa na viongozi tangulizi ktk kutatua matatizo haya hususani Mwl. JK Nyerere?
6. Je huu udini unaosemwa upo ktk utawala huu wa Kikwete una mkono labda toka nje? Kama ndiyo ni kwa malengo gani? Kwa faida ya nani?
7. Nini kifanyike kuuondoa udini huu? Nani anawajibika zaidi katika suala hili?
Nawasilisha! Nategemea kupata elimu kwenu.
 
Mko wapi sasa?, njooni basi mtujibie haya maswali ni muhimu sana kupata majibu!
 
kama hujui sema unachojua kuhusu kiwete kwa mfano aliwahi kuiba wali.
 
Rais akiwa Muislam ndiyo huitwa mdini!huku waislam hawana chochote cha kujivunia kwa uwepo wa JK,bora hata Mzee Mwinyi kina dada kupewa ruksa ya kuvaa nikab!
 
Back
Top Bottom