Nielimisheni Kuhusu Escrow

Mlachake

JF-Expert Member
Oct 13, 2009
4,412
4,559
Naomba niwape pole kwa majukumu yenu ya kila siku na Nitoe asante kwa wengi wenu mnaotumia muda wenu kutoa Elimu/Ufanannuzi wa mambo mbali mbali hapa Jumvini.

Nimekuwa katika wingu zito sana kuelewa hili sakata la escrow hasa katika ile mijadala ya pesa ni za uma au sio za uma,

Ninachoelewa account ya escrow ilifunguliwa kutokana na mgogoro wa Tanesco na IPTL, Ina maana malipo ya Tanesco kwa IPTL yapitie kwenye ile account ya Escrow mpaka pale Mgogoro utakaopo sulihishwa ndio ijulikane kiasi halisi alichostahili kulipwa IPTL.

Swali langu ni kwamba, huu mgogoro ulishakwisha? Na kama mgogoro ulikua umeisha nani wa kuruhusu zile pesa zitolewe katika ile account?

Naombeni kutolewa tongo tongo nimechoka kuburuzwa na haya magazeti na kelele za wanasiasa.
 
Back
Top Bottom