Kunguru Mjanja
JF-Expert Member
- Aug 22, 2012
- 2,047
- 3,980
Mamlaka ya vitambuisho vya taifa (NIDA) inaendelea na zoezi la Usajili na Utambuzi wa watu nchi nzima ambapo kwa sasa wanafanya kwa awamu na wameanza na mikoa 11 ambayo ni Njombe, Mbeya, Songwe, Geita, Mwanza, Simiyu, Shinyanga, Singida, Manyara, Arusha na Kilimanjaro.
Afisa msajili NIDA mkoa wa Mbeya Bi Alavuya Mtalima amesema kuwa zoezi linaendelea vizuri na tayari wamesajili zaidi ya watu laki moja mkoani Mbeya. Pia anasisitiza wananchi kujitokeza kwa wingi zaidi kusajiliwa kwani ni haki yao ya msingi kupata kitambulisho cha taifa kwa maendeleo ya kiuchumi na usalama. Ameongeza kuwa kwa sasa wanafanya usajili wa mkupuo (mass registration) ambapo wanaenda mitaani kuwafuata wananchi hivyo ni nafasi ya pekee kwa wananchi kuhudumiwa. Wale wote ambao bado hawajasajiliwa wafike kwenye ofisi za serikali za mitaa ili kuanza mchakato wa usajili na wale ambao tayari wamekamilisha kujaza fomu wajitokeze kupiga picha na kuchukuliwa alama za vidole ili kukamilisha zoezi.
Nae afisa Mchambuzi wa Mifumo ya Kompyuta na mwakilishi wa kitengo cha Habari NIDA HQ Bw. Deodatus Alexander Mchaki amesema zoezi hilo ni fursa kwa wananchi ili waweze kutambuliwa, nani ni nani? anaishi wapi? na anamiliki nini? Hivyo wananchi waendelee kujitokeza kwa wingi na kusajiliwa kuunga mkono jitihada za serikali kuleta maendeleo. Kwa wale ambao mikoa yao bado haijafikiwa na usajili wa mkupuo (mass registration) waendelee kujitokeza kwenye ofisi za NIDA ambazo zipo katika kila wilaya nchini.
Amesisitiza kuwa Zoezi hilo ni BURE hivyo Mwananchi hatakiwi kuchangia garama yoyote. Ili kusajiliwa ni lazima Mwananchi afike na nakala (copy) ya nyaraka/viambatanisho muhimu vya kuweza kumtambulisha uraia wake, umri na makazi. Mfano wa nyaraka hizo ni; Kadi ya mpiga kura, cheti cha kuzaliwa, leseni ya udereva, ID ya Mzanzibar mkazi, TIN, Pasi ya kusafiria, vyeti vya elimu nk.
Pichani: Wananchi wakiwa katika foleni ya zoezi la kuandikishwa
Pichani: Mwananchi akiendelea na uandikishwaji na hapa akiweka saini ya kielectroniki
Pichani: Mwananchi akiendelea na uandikishwaji na hapa akichukuliwa alama za vidole
Wananchi wanaweza kuwasiliana na NIDA kwa kupitia njia zifuatazo;

- Kupiga simu huduma kwa mteja namba 0673333444/0687416666
- Kuwaandikia S.L.P 12324
- Barua pepe nida.tanzania@nida.go.tz
- Kutembelea tovuti www.nida.go.tz
- Pia kupitia mitandao ya kijamii. facebook; Nidatanzania, Twitter; @NIDA_Tanzania, Instagram; nidatanzania, Chaneli Youtube; Nida Tanzania.