NIDA na TCRA wanatumia utashi wa binadamu wa kawaida?

GODZILLA

JF-Expert Member
Dec 26, 2014
5,902
10,503
Baada ya watu milioni kadhaa kuzimiwa laini zao za simu kwa kile kinachodaiwa kutosajili laini hizo kwa "alama za vidole", nikajiuliza maswali yafuatayo:

1. Ufahamu wa TCRA kuhusu maswala ya vitambulisho vya Taifa ni wa kiwango gani?

2. Wanaosimamia hii taasisi ya TCRA ni binadamu wa kawaida?

3. Vitambulisho vya taifa vinapatikana katika mazingira yapi?

4. Ni kweli watu hawataki kusajili laini zao?

5. Kwanini zoezi la kusajili limekuja ghafla ghafla mara watu wanashtukia tu simu zimeshazimwa? Eti "deadline"?

6. Kulikuwa na ubaya gani kuhakikisha watu wote wameshapata vitambulisho vya Taifa na kutoa muda mrefu kusudi watu wote wapate fursa ya kusajili laini zao kisha wazime?

7. Hii haraka haraka ya kukimbilia kuzima simu imesababishwa na nini hasa? Kulikuwa na tishio au uharaka kiasi hicho?

8. Rais magufuli ni mmoja wa wajumbe wa TCRA? maana hakuwa nyuma kutoa rundo la matamko asubuhi na jioni! Rais magufuli ni mjumbe wa hii Taasisi?

9. Sheria inasemaje kuhusu usajili wa laini za simu? Kitambulisho cha Taifa ni takwa la lazima?

10. Hatima ya waliozimiwa laini zao ni ipi? Waendelee kusubiri huruma za NIDA au HISANI za mkombozi wao Rais wa wanyonge?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hawa umbwa wanakela sana sijui kwa nini waziri nditiye hakutwanga ban ya kuingiza pumbu zake US kwa sababu na yeye anadhurumu haki ya kuishi
 
Back
Top Bottom